Matumizi Bora ya Friji

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275

Friji hutumika kuhifadhi vyakula vya aina mbalimbali ili visiharibike mapema. Friji ikitumiwa vyema husaidia sana katika uhifadhi wa vyakula lakini isipotumiwa vizuri huweza kusababisha hasara na magonjwa kwa mtumiaji.

Joto la Friji
Joto la friji halitakiwi kuwa zaidi ya nyuzijoto 5 za centigrade. Bakteria wanazaliana upesi ikiwa joto ni zaidi ya nyuzijoto 5 na ni hatari kwa vyakula vilivyohifadhiwa. Usiweke vyakula vya moto kwenye friji maana vitaongeza joto ndani ya friji.

Mahali pa Kuhifadhi
Kuna tofauti ya ubaridi kati ya ndani ya friji na kwenye mlango wa friji. Mlango wa friji unajoto zaidi hivyo usiweke vitu vinavyoharibika upesi kama maziwa au mayai. Vitu vinavyofaa kwenye mlango wa friji ni kama siagi, soda, jam n.k. Maziwa, mayai na vyakula vilivobaki baada ya mlo vihifadhiwe ndani ya friji kwenye shelfu. Matunda na mboga viwekwe kwenye container za friji ila njegere ili ziweze kukaa muda mrefu weka kwenye friza maana ukiweka kwenye shelfu zitaanza kutoa mizizi.

Nyama, samaki, kuku, sausage na vyakula ambavyo umechemsha uje upike siku nyingine vinapaswa kuwekwa kwenye friza maana vinahitaji baridi kali. Pia kama maziwa hutayatumia kwa siku moja au mbili yaweke kwenye friza.

Usafi
Safisha uchafu mara tu unapomwagika na usiache hadi ukaukie hapo. Usiweke chakula hadi kikaharibika, kama ni chakula kimebaki kisikae zaidi ya siku nne. Angalau mara moja kwa mwezi uwe na siku ya kutoa vitu vyote kwenye friji na kuizima na kisha kusafisha kila sehemu. Zaidi kuhusu usafi wa friji soma Usafi wa jokofu kwenye link ya jikoni hapo kulia.


Women of christ
 
Kwanini nyanya zinaoza nikiweka ndani ya friji, nimepata somo kuhusu njegere niliziweka chini nikakuta zinamizizi ya kutosha..
 
Hata mimi nyanya zinaoza sijui kwanini
Ukitaka kuhifadhi kwa muda mrefu ,zisage na blender , halafu unaweka kwenye freezer ,
Unanunua viplastic fulani kama vile vya kutengenezea ice cubes ila ni vikubwa, kidogo kiumbo, kwa ajili ya single serving ukihitaji kutumia kwa mapishi
 
Back
Top Bottom