Matumaini ya mzee Lowassa yageuka kuwa shubili

Matumaini ya mzee Lowassa yageuka kuwa shubili

Magufuli kudhbiti ufisadi ni ngumu maana hao hao mafisadi ndio wanajitahidi ili aende ikulu..mabadiliko ndani ya ccm ni ngumu..

Wacha utani mkuu! Unaongea kinyume sio! Wote tunamjua fisadi ambaye ana back up kubwa ya mafisadi wakubwa behind the scene ambao wanamsapoti fisadi papa ili aende Ikulu!
 
Mmh kweli lkn lazima mh Lowassa ataikimbia nchi yani hio ni lazima
 
Ata Ukiangalia In deep mzee Lowassa kam vile kaanza kakataa tamaa vile nanavojua lzm itakua ashaandaa wp atakimbilia na maybe kikwete itakua ashanwandalia nchi ta kukimbilia
 
Kamwe usidharau nguvu ya watu "Wapumbavu,malofa na mbumbumbu" hususani katika masuala yanayohusu mustakabali wa Maisha yao!!..Hakika nakuambia CCM inaondoka madarakani mwaka huu 2015!!Lowassa ndiye Rais mpya Tanzania.

Inzi atatengeneza asali !
 
  • Thanks
Reactions: chk
Unpozungumzia wadadisi wa siasa kwa msiofahamu ni watu wanaofatilia siasa za nchi hii kwa ukaribu, wenye uzoefu na utaalamu katika uchambuzi wa masuala ya kisiasa.
 
Kumekuwa na kila dalili ya matumaini ya mzee Lowasa kugeuka kuwa shubili, mara baada ya uchaguzi mkuu ikiwa ni kutokana kutojua nini hasa atakachofanya mara baada ya kushindwa uchaguzi huu japo kuna kila dalili za kushitakiwa kwa matumizi mabaya ya mali za serikali pamoja na ufisadi.

Washauri wake wa karibu pamoja na marafiki wake wakuu wamezidi kumpa moyo japo ukweli wa mambo wanaufahamu fika jinsi gani mzee huyo anavoshabikiwa na watu wasiostahiki kumpigia kura, hata hivo mara baada ya Dr Magufuli kuingia ikulu kuna uwezekano Mzee akatokomea kusipojulikana jambo linalozidi kutia shaka familia yake pamoja na watu wanaomzunguka.

Aidha kwa mujibu wa vyanzo vinavyoaminika vinasema Mzee Lowassa si rahisi akapewa nafasi ya mwenyekiti wa CHADEMA japo yeye mwenyewe hiyo ni miongoni mwa plan B yake, jambo ambalo si rahisi Mbowe kumwachia nafasi hiyo kwa sasa.

Wadadisi wa maswala ya kisiasa wanazidi kutabili kwamba ujio wa Dr Magufuli ktk nafasi ya urais inaweza kuwa ni mwanzo mzuri wa kuzaliwa CCM imara itakayodhibiti vitendo vya rushwa na ubadhilifu wa raslimali za Taifa uliokuwa ukifanywa na viongozi wachache ndani ya chama chake.

Kwa mazingira hayo ukilinganisha na sera ya uadilifu waliyokuwa nayo CHADEMA hapo awali wadadisi na wafuatiliaji wa siasa wanandai chama hicho kinaenda kubakia ktka historia ya vyama vya upinzani vilivyoibuka na kuzama ghafla.

Lowasa ameingia chadema akiwa anajua kuna kupata na kukosa ndiyo maana amejipanga na plan B ambayo ipo kwenye makubaliano kuwa endapo atakosa Urais atakuwa mlezi wa chama na mwana bodi ya Udhamini atakuwa akilipwa fungu fulani kama mzee Mtei, Lowasa anatambua kuwa kwenye kutafuta kuna kupata au kukosa amejipanga kwa hali zote. Pia endapo magufuli ataleta visasi zipo mahakama za ICC watamshitaki huko na ujue uhasama wa siasa huwa ni wa kipindi cha uchaguzi tu na pindi uchaguzi ukipita uhasama huyeyuka na maisha ya kawaida kuendelea
 
Ata Ukiangalia In deep mzee Lowassa kam vile kaanza kakataa tamaa vile nanavojua lzm itakua ashaandaa wp atakimbilia na maybe kikwete itakua ashanwandalia nchi ta kukimbilia

Lowasa haendi popote atakuwepo hapa hapa atakuwa Mlezi wa chama kama mzee Mtei endapo Ukawa watakosa kuingia ikulu na endapo watataka kumkomoa atalindwa na mawakili wa kutosha pia ICC ipo kwani hata wale ambao watakuwa wakimkomoa Lowasa wana madhambi yao ambayo nao wanastahili kuwa mahakamani hata leo.
 
Wacha utani mkuu! Unaongea kinyume sio! Wote tunamjua fisadi ambaye ana back up kubwa ya mafisadi wakubwa behind the scene ambao wanamsapoti fisadi papa ili aende Ikulu!

EPA, escrow, kivuko cha 1978, mabehewa feki, chenji ya rada, kuua ATC, mashirika ya Reli, kuuza viwanja, nyumba za serikali na wizi mwingineo mwingi vimefanywa na Lowasa?
 
chadema au ccm b/makapi wamejikoroga kumpokea el sasa waache wapate kitakacho wapata kama yaliompata mrema....

Dua la kuku halimpati mwewe, mrema na Lowasa ni Vitu viwili tofauti kipindi kile Mrema hakuwa na plan B aliingia kichwa kichwa lakini Lowasa ameingia akijua kuna kupata na kukosa.
 
Kumekuwa na kila dalili ya matumaini ya mzee Lowasa kugeuka kuwa shubili, mara baada ya uchaguzi mkuu ikiwa ni kutokana kutojua nini hasa atakachofanya mara baada ya kushindwa uchaguzi huu japo kuna kila dalili za kushitakiwa kwa matumizi mabaya ya mali za serikali pamoja na ufisadi.

Washauri wake wa karibu pamoja na marafiki wake wakuu wamezidi kumpa moyo japo ukweli wa mambo wanaufahamu fika jinsi gani mzee huyo anavoshabikiwa na watu wasiostahiki kumpigia kura, hata hivo mara baada ya Dr Magufuli kuingia ikulu kuna uwezekano Mzee akatokomea kusipojulikana jambo linalozidi kutia shaka familia yake pamoja na watu wanaomzunguka.

Aidha kwa mujibu wa vyanzo vinavyoaminika vinasema Mzee Lowassa si rahisi akapewa nafasi ya mwenyekiti wa CHADEMA japo yeye mwenyewe hiyo ni miongoni mwa plan B yake, jambo ambalo si rahisi Mbowe kumwachia nafasi hiyo kwa sasa.

Wadadisi wa maswala ya kisiasa wanazidi kutabili kwamba ujio wa Dr Magufuli ktk nafasi ya urais inaweza kuwa ni mwanzo mzuri wa kuzaliwa CCM imara itakayodhibiti vitendo vya rushwa na ubadhilifu wa raslimali za Taifa uliokuwa ukifanywa na viongozi wachache ndani ya chama chake.

Kwa mazingira hayo ukilinganisha na sera ya uadilifu waliyokuwa nayo CHADEMA hapo awali wadadisi na wafuatiliaji wa siasa wanandai chama hicho kinaenda kubakia ktka historia ya vyama vya upinzani vilivyoibuka na kuzama ghafla.
Kama mimba ikitoka je?
 
Akili yako haijakomaa ukizingatia wewe ni junior member humu jamvini. Nenda kachukue buku tano lumumba huna jipya! Hili ni jamvi la Great Thinkers! Watu wenye akili ndogo kama yako hawahitajiki humu! Acha kukurupuka kwa mambo usiyayajua. Inamaana wewe unaakili kuliko Lowassa. Mbona JF ipo siki zote leo ndo umeona uje kueneza umbea wako humu. Umekula maharage ya wapi wewe?
tatizo la nyie mazombie wa mbowe kila mkielimishwa mnadhani watu wamekula maharage au kinywa viroba; na hapo ni kama wakinusurika matusi.
 
Back
Top Bottom