Matumaini ya mzee Lowassa yageuka kuwa shubili

Matumaini ya mzee Lowassa yageuka kuwa shubili

Kumekuwa na kila dalili ya matumaini ya mzee Lowasa kugeuka kuwa shubili, mara baada ya uchaguzi mkuu ikiwa ni kutokana kutojua nini hasa atakachofanya mara baada ya kushindwa uchaguzi huu japo kuna kila dalili za kushitakiwa kwa matumizi mabaya ya mali za serikali pamoja na ufisadi.

Washauri wake wa karibu pamoja na marafiki wake wakuu wamezidi kumpa moyo japo ukweli wa mambo wanaufahamu fika jinsi gani mzee huyo anavoshabikiwa na watu wasiostahiki kumpigia kura, hata hivo mara baada ya Dr Magufuli kuingia ikulu kuna uwezekano Mzee akatokomea kusipojulikana jambo linalozidi kutia shaka familia yake pamoja na watu wanaomzunguka.

Aidha kwa mujibu wa vyanzo vinavyoaminika vinasema Mzee Lowassa si rahisi akapewa nafasi ya mwenyekiti wa CHADEMA japo yeye mwenyewe hiyo ni miongoni mwa plan B yake, jambo ambalo si rahisi Mboye kumwachia nafasi hiyo kwa sasa.

Wadadisi wa maswala ya kisiasa wanazidi kutabili kwamba ujio wa Dr Magufuli ktk nafasi ya urais inaweza kuwa ni mwanzo mzuri wa kuzaliwa CCM imara itakayodhibiti vitendo vya rushwa na ubadhilifu wa raslimali za Taifa uliokuwa ukifanywa na viongozi wachache ndani ya chama chake.

Kwa mazingira hayo ukilinganisha na sera ya uadilifu waliyokuwa nayo CHADEMA hapo awali wadadisi na wafuatiliaji wa siasa wanandai chama hicho kinaenda kubakia ktka historia ya vyama vya upinzani vilivyoibuka na kuzama ghafla.

Robojosoni
1. Ugonjwa
2. Udini
3. Shubili
4. .....
5. ......

Kachukue book 7 yako Lumumba, leo umeongoza kwa propoganda
 
Kwani hao "wadadisi"wa mambo ya kisiasa ndio kina nani?
Huo ni uchwara tu...unakaa kijiweni unaandika ujinga humu...njaa itakuua!
Kachukue hela ya msokoto na kiroba pale Lumumba
 
Hata kwenye jf,mchezo wa kupakizana kwenye malori kusababisha mafuriko inatumiwa na wana lumumba,Mtu mmoja ID nne,tunawagundua kwa namna mtu anavyo argue,unakuta mtu anaanzisha uzi mwenyewe then anaanza kuchangia,anajiuliza maswali na kujijibu,duh!!! Mna hali ngumu aisee
 
kumekuwa na kila dalili ya matumaini ya mzee lowasa kugeuka kuwa shubili, mara baada ya uchaguzi mkuu ikiwa ni kutokana kutojua nini hasa atakachofanya mara baada ya kushindwa uchaguzi huu japo kuna kila dalili za kushitakiwa kwa matumizi mabaya ya mali za serikali pamoja na ufisadi.

Washauri wake wa karibu pamoja na marafiki wake wakuu wamezidi kumpa moyo japo ukweli wa mambo wanaufahamu fika jinsi gani mzee huyo anavoshabikiwa na watu wasiostahiki kumpigia kura, hata hivo mara baada ya dr magufuli kuingia ikulu kuna uwezekano mzee akatokomea kusipojulikana jambo linalozidi kutia shaka familia yake pamoja na watu wanaomzunguka.

Aidha kwa mujibu wa vyanzo vinavyoaminika vinasema mzee lowassa si rahisi akapewa nafasi ya mwenyekiti wa chadema japo yeye mwenyewe hiyo ni miongoni mwa plan b yake, jambo ambalo si rahisi mboye kumwachia nafasi hiyo kwa sasa.

Wadadisi wa maswala ya kisiasa wanazidi kutabili kwamba ujio wa dr magufuli ktk nafasi ya urais inaweza kuwa ni mwanzo mzuri wa kuzaliwa ccm imara itakayodhibiti vitendo vya rushwa na ubadhilifu wa raslimali za taifa uliokuwa ukifanywa na viongozi wachache ndani ya chama chake.

Kwa mazingira hayo ukilinganisha na sera ya uadilifu waliyokuwa nayo chadema hapo awali wadadisi na wafuatiliaji wa siasa wanandai chama hicho kinaenda kubakia ktka historia ya vyama vya upinzani vilivyoibuka na kuzama ghafla.
chadema au ccm b/makapi wamejikoroga kumpokea el sasa waache wapate kitakacho wapata kama yaliompata mrema....
 
Kwa mfumo uliopo hapo kwa watawala hata aje malaika awezi kuufumua/kuubadili hata huyu aitwae fisadi asingeitwa fisadi iwapo angeamua kubaki.si mmeona wale wa escrow wakinyanyuliwa na kunadiwa.
 
Hata kama mgombea wa urais kupitia ChADEMA/UKAWA atashindwa, CHADEMA kitabaki kuwa chama kikuu cha upinzani
 
Mimi ningependa kuwatahadharisha sasa hivi hapa jamii forum imevamiwa watu wa propaganda tatizo hawana hoja zaidi ya kumshambulia Lowassa tuwe makini.
 
Kamwe usidharau nguvu ya watu "Wapumbavu,malofa na mbumbumbu" hususani katika masuala yanayohusu mustakabali wa Maisha yao!!..Hakika nakuambia CCM inaondoka madarakani mwaka huu 2015!!Lowassa ndiye Rais mpya Tanzania.
 
unatakiwa kuwa na muda gani ndio uchangie au upost

jiandae kisaikolojia - safari ndio inaisha isha hio - for your information hata babu Duni atarudi CUF baada ulofa kumtoka
TATIZO LAKO LIKO HAPO CHINI
Junior Member Array
Join Date : 12th September 2015
Posts : 3
Rep Power : 0
Likes Received0
Likes Given0
 
kwa kigezo gani Lowasa ataingia Ikilu? wananchi 90% know his weakness
Kamwe usidharau nguvu ya watu "Wapumbavu,malofa na mbumbumbu" hususani katika masuala yanayohusu mustakabali wa Maisha yao!!..Hakika nakuambia CCM inaondoka madarakani mwaka huu 2015!!Lowassa ndiye Rais mpya Tanzania.
 
bado lowasa ni tishio kubwa sana huko ccm. ccm hawalali wanatumia mpaka dola kujaribu kutisha wafuasi wa mabadiliko. mabango ya lowasa yanahujumiwa pia. vilevile tbc na star tv vinatumika sana kufanya propaganda ya ccm. ccm mwaka huu wajiandae...
 
Waonee huruma wanywa viroba mkuu make ukisema hivyo tu tayari wÃ-nafura wanakuwa kama anaconda ..babu yao kijeba anashindwa hata kuhesabu moja mpaka 50
 
Back
Top Bottom