NGAYANIMO
Member
- Feb 17, 2026
- 43
- 61
MATUMAINI:
katika mambo yanayokwamisha mtu kuweza kuendelea ni pale anapokutana na changamoto mbalimbali za maisha hasa pale unapokuta unashindwa kufikia malengo uliyoweka kwa wakati,hali hii moja kwa moja watu huweza kumlaumu Mungu.
Inawezekana umeshapitia magumu fulani na kama hujapitia basi jiandae maana lazima yaje hakuna namna unaweza kuzuia.wengi sana huwa wanaomba Mungu naomba nifanikishe katika jambo fulani.lakini sijawahi kusikia mtu akisema Mungu naomba jaribu hili ili nifanikiwe,hii ni sawa na mwanafunzi kutaka kupanda daraja la kimasomo pasipo kuomba mtihani.
kiukweli ukikuta mwanafunzi ameomba mtihani ujue huyo mwanafunzi yuko vizuri sana.sio kwamba nasema tuombe majaribu lakini yanapotupata tusivunjike moyo maana kuna daraja ambalo Mungu anataka uvuke.
SIKILIZA HAYA MASHAIRI YA KITOA USHAURI KWA JAMII KUHUSU UPENDO NA KUPEANA MATUMAINI KWENYE NYAKATI NGUMU KWENYE MAISHA YETU YA KILA SIKU.
Nyimbo hii inaitwa "Tumaini" ( Afande sele,fid Q,Mwana Fa,Dudu baya na Dogo ditto lakini hapa nimeleta baadhi ya verse zilizopatikana katika Wimbo huo.
Afande sele.
"Kwa mwenye shibe kumkumbuka mwenye njaa/
Naona ni Zaidi ya Upendo Duniani mpaka kwa jah/
Inanifanya niamini wewe na mimi Sambamba/
Ukimshirikisha na Muumba kwa kumuomba aliye juu/
Meli Yetu Haigongi mwamba..!!
Na ndo maana ukipata shida Kila unaponiambia/
Naona sio Yako Tu, Hata mimi inanihusu pia/
Utanzania ndo Nguzo,uzalendo kama utawekwa mbele wakati wa matatizo/
Ndo mwendo ,.!!
Kubwa litakuwa ndogo mi na wewe Tunauwezo/
Kwa kishindo..!!
Udungu sio kufanana, udungu ni kusaidiana kumpa mwenye uhitaji ni kumkopesha molana/
Atalipa Bwana..
Dudu baya :
"Pole Bibi na Babu/
Pole Baba na Mama/
Pole Uncle na Auntie/
Ni kawaida Duniani/
Ni shida na Raha /
Furaha na Huzuni/
Wenye Uwezo tuwatazame Wenzetu/
Msaada wahitaji/
Mvua tunaomba/
Bila wewe hatuna Ujanja/
Mtoto ni mtoto na Baba bado ni Baba/
Walala njaa mola wetu hatuondolee...
Professor jay:
"Upendo ndio kitovu cha Imani ninavyo Amini/
Kama hivi ndivyo ilivyo kwako basi uko na Mimi/
Mwenzako anateseka sharti umthamini/
Jirani analia njaa japo mpe matumaini/
Matumaini..!!
Ufukara na Utajiri zote hali
Nionavyo tuwachangie wezetu hali na mali/
Pesa makarasi mtani Hasara Roho/
Basi tuchangie kidogo mwenyezi Atakupa More/
Tunajali nini..? Utu Au vitu/
Usiruhusu ubadhirifu ilimradi ipite siku/
Nini..? Unachekelea wenzako wanateketea/
Usipochangia wewe kizazi kinapotea/
Yeah..!!
End.
Kila mmoja, basi, na atoe kadiri alivyoamua, kwa moyo na wala si kwa huzuni au kwa kulazimishwa, maana Mungu humpenda yule mwenye kutoa kwa furaha.
Kasikilize wimbo huu..
Lakini pia tuendelee kumuombea Godfrey Tumaini a.k .a Dudu baya ili aweze kukaa sawa kiafya .
Dudu Baya yuko nchini India kwa zaidi ya wiki moja kwa ajili ya matibabu ya pingili za mgongo.
Taarifa hii inafuatia hali yake ya afya ambayo imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu na mashabiki wake na familia
Ukwaju wa kitambo