Matukio Tisa yaliyomdhalilisha Rais Kikwete 2006-2010

Status
Not open for further replies.
Kuna lile la kumteua mtu kuwa mkuu wa wilaya wakati ana kesi ya jinai mahakamani. Kama sikosei huyu alikuwa mbunge wa zamani wa Biharamulo. Uteuzi ulisitishwa baadae wakati anakwenda kuripoti.

Hii ilisahaulika.
 
Hotuba yake kwa ajili y a kujibu wafanyakazi akieleza mgomo ni Fake kisheria; yeye ni hakimu au mahakama; au yuko juu ya sheria; au ndio double standards; anatishia watu kuwapiga na virungu au hata anaweza kumaanisha kuua kwa ajili ya kudai haki zao; mie naona kajidhalilisha kabisa hapa kuliko mahala pengine popopte tena iingizwe na kuwa 10 maana hii ina nguvu sana
 

Pole sana we memba wa TUCTA nini,ha ha ha.Uko sahihi.
 

Mkuu hivyo ndivyo ilivyo kujiuzulu hua kunamuondolea heshma fulani mteuzi kama huna khabari ndio maana wakati mwingine mteuzi huwa anakataa maombi ya kujiuzulu ili asipatwe na aibu hiyo. Hivi kama JK angekubali maombi yote ya waliotaka kujiuzulu leo hii wangekua wamemuabisha wangapi? Kujiuzulu humaanisha mtu aliyeteuliwa si sahihi na alikubali uteuzi akijua kua yeye si sahihi lakini baada ya kuvurunda na kuonyesha kuwa haku-fit ktk uteuzi wake ndo anajiuzulu sasa mpaka hapo anayeumbuka nani? MKUU KUJIUZULU NI AIBU KWA MTEUZI SIKU ZOTE. Hata raisi akijiuzulu ni aibu kwa wapiga kura wake.
 

Ni full time ipi unayomaanisha? kama hujui kuwa alizidiwa AR basi usiseme full time, na kuhusu kuzidiwa mara kwa mara nadhani umethibitisha matukio ww mwenyewe. Hebu nipe Raisi mwingine aliyepatwa na masahibu kama hayo ktk historia ya Tz na maraisi watatu waliomtangulia.
 

Asante kwa kunisadia kuelewesha.Ndio maana viongozi wetu wengi wakiambiwa wajiuzulu huwa wagumu sana.
 
Alishawahi kusema eti hadi leo hii hajui kwnini Tanzania ni maskini kiasi hicho, shame on him!
 
Inasikitisha!, I know he has to make some tough decisions on his own but, he has advisors who could've done or say something to prevent some michemsho. This's ridiculous, and uzembe usio na akili.
 
Inasikitisha!, I know he has to make some tough decisions on his own but, he has advisors who could've done or say something to prevent some michemsho. This's ridiculous, and uzembe usio na akili.

Ni kweli kabisa.Lakini JK ana fursa ya kuwawajibisha na kuachana na hawa washauri wake ambao mpaka sasa naamini ameshatambua kwamba hawamsaidiii kwa kiwango kinachotakiwa..Kwanini aendelee kuwa kumbatia?
 
Kama uteuzi wenyewe anaufanya zaidi kwa misingi ya ushemeji, ujomba, uwifi, ukwe, na family friends wategemea kuna kuwajibishana kokote kwa dhahiri kutaja tokea kweli hapo?
 
Kama uteuzi wenyewe anaufanya zaidi kwa misingi ya ushemeji, ujomba, uwifi, ukwe, na family friends wategemea kuna kuwajibishana kokote kwa dhahiri kutaja tokea kweli hapo?
Nakubaliana na wewe.Uko sahihi kabisa na haya ndio mdhara ya neportism,huharibu kabisa utendaji kazi.Neportism ilikuwa na mojawapo ya sababu za kufa kwa viwanda vyetu vingi kipindi cha Nyerere na Mwinyi.
 
Bila kusahau akamteua shahidi wa serikali na mkuu wa kitengo cha EPA kuwa Mkuu wa TIB! Akifikiri watanzania hawajui 1 + 1 = 2. Ndo huyu ataleta agricultural revolution? tuache utani!!
 
Bila kusahau akamteua shahidi wa serikali na mkuu wa kitengo cha EPA kuwa Mkuu wa TIB! Akifikiri watanzania hawajui 1 + 1 = 2. Ndo huyu ataleta agricultural revolution? tuache utani!!

Jamani kama aliweza kumanage alipokuwa EPA kwanini ashindwe TIB,ha ha ha?Alifanya vizuri kule alikokuwa mwanzo,kuwezesha KAGODA kujichotea vijisenti na kuwezesha uchaguzi 2005.Ni mtendaji mwaminifu.
 
Kuna hii aliyofanya,immediately baada ya kuchaguliwa alianza kuzurura huku na huko kujitambulisha huku utambulisho ukiandamana na kuomba misaada.It was like tulichagua mtu mzuri zaidi wa kuombaomba out of the rest
 
Kusaini mkataba wa Afrika Mashariki kunapiku matukio yote ya kumdhalilisha Rais Kikwete, kwani anasaini kujiondolea mamlaka yake mwenyewe. Inasemekana Nyerere alitumia mbinu kumsainisha Karume mikataba ya muungano, kwa kumwachia Karume mkubwa misafara na jina la Urais ili ajione bado ni mtawala, na kwamba, Muungano 'utaishia Chumbe', kwa kile kinachosemekana kwamba Nyerere alikuwa mwerevu kumzidi Karume. Leo miaka hamsini baadaye, Kikwete anasaini mikataba ya kumnyang'anya madaraka yeye mwenyewe, na haoni tatizo, kwa kile kinachoonekana ni mbinu ileile ya zamani ya kumuachia aendelee na misafara na kutandikiwa mazulia mekundu, mpaka pale atakapobaini kwamba amebaki rais jina (hata Tenga ni rais wa TFF) bila madaraka ('power is nothing without control' -- tangazo).
 

Mmh.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…