Matukio Tisa yaliyomdhalilisha Rais Kikwete 2006-2010

Status
Not open for further replies.

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864
Katika kipindi cha Uongozi wa Rais Kikwete kuna matukio kadhaa yaliyotokea na kusababisha minong'ono ,mijadala kwenye vyombo vya haabri na hata sehemu mbalimbali ambapo watu hukaa na kujadili.Matukio haya mengine yamesababisha baadhi ya watu kuhamishwa maeneo yao ya kazi na wengine kupewa maonyo makali.Kubwa zaidi ni mengine kusababisha watu kujadili uwezo wa Rais na watendaji wake katika kuongoza Taifa hili . Yapo matukio mengi lakini makubwa ni nane kama ifuatavyo;

1.
Kusaini kwa mbwembwe Sheria ya Gharama za Uchaguzi 2010 yenye vipengele tata vilivyochomekwa kinyemela.

Hivi karibuni Rais alisaini kwa mbwembwe sheria ya gharama za uchaguzi iliyopitishwa na Bunge mwanzoni mwa mwaka huu.Itakumbukwa kuwa sheria hii kabla na baada ya kuwa sheria ilipigiwa kelele sana na wanaharakati pamoja na vyama vya upinzani kuwa ni mbovu haifai.Rais bila kujua kilichomo aliisani kwa mbwembwe zote kwa kuwakaribisha watu toka kada mbalimbali wakiwemo mabalozi.

Muda mfupi baadaye ikagundulika kuwa Sheria iliyosainiwa na Rais ilikuwa na vipengele ambavyo havikujadiliwa Bungeni. Wote tumeshuhudia sheria hii ikarudishwa tena bungeni ili kujadiliwa pamoja na kwamba ilishajadiliwa, hili tukio sio la kawaida wala la kupuuzia hasa ikizingatiwa kuwa sheria hii ni sheria nyeti sana. Tukio hili la kituko lilifanyika katika Viwanja vya Ikulu

2.
Kujiuzulu kwa Waziri Mkuu-Edward Lowassa

Kwa kuwa Waziri Mkuu anateuliwa na Rais tena wakati mwingine bila kushauriana na mtu kitendo cha Lowassa kulazimika kujiuzulu baada ya kashfa ya Richmond ilikuwa ni pigo jingine kwa Rais. Hii inamaanisha kuwa Rais wetu hayuko makini katika teuzi zake ndio maana anateua watu ambao sio viongozi wasafi wasio na dhamira ya dhati ya kuongoza taifa hili. Hii ni aibu nyingine kwa Rais kwani mtendaji wake mkuu aliyempenda kuliko Mawaziri wote kumuangusha kwa utendaji wake mbovu hivyo kulazimisha kuvunjwa kwa baraza la Mawaziri na kumteua mtu mwigine ambaye hakuwahi kumfikiria kuwa Waziri Mkuu.

3.
Mradi wa Malaria
Mtakumbuka kuwa Rais alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Mradi wa Malaria haikubaliki uliofanyika Leaders Club. Baada ya uzinduzi huu uliowashirikisha wanamuziki mbalimbali wa Bongo Fleva wa hapa nchini,mwanamuziki Joseph Mbilinyi(Sugu) aliwatuhumu baadhi ya wasaidizi wa Rais kumtumia Rais kutimiza maslahi binafsi za kibiashara amabpo wasaidizi hao walimpora mradi huu wenye thamani kubwa.

Tukio hili lilikanushwa vikali na Ikulu lakini pamoja na hayo limeidhalilisha ikulu na hivyo kumdhalilisha Rais.

4.
Gari la Kubeba Wagonjwa
Itakumbukwa kuwa mwanzoni mwa mwaka huu Rais aligoma kukabidhi gari la la msaada la kubeba wagonjwa baada ya kutokea utata kuhusu halmashauri inayopaswa kukabidhiwa gari hilo. Gari hilo lililotolewa msaada na Kampuni ya CMC Automobiles Limited lilipaswa kutolewa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Longido lakini cha ajabu alifika mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.Tukio hili lilitokea ndani ya Ikulu.

5.
Kupokea Hundi yenye Utata

Rais alijikuta kwenye tukio jingine la aibu baada ya picha yake kuchapishwa katika vyombo mbalimbali vya habari ikimuonyesha akiwa anapokea hundi kutoka kwa maofisa wa juu wa benki ya Dunia. Kama mtakumbuka tulionyeshwa Rais akikabidhiwa hundi hiyo ambacho kiasi cha fedha kilichoandikwa kwa maneno,dola za Kimarekani laki mbili kilkuwa tofauti na kile kilichoandikwa kwa tarakimu dola 300,000. Hili lilikuwa ni tukio jingine la aibu kwa Ikulu na Rais wetu kwa ujumla.

6.
Daraja la Lugoba
Itakumbukwa kuwa mwaka 2006, daraja la Lugoba ambalo linaunganisha mikoa ya Dares salaam,Tanga, Kilimanjaro na Arusha liliharibiwa na mvua na hivyo kuwa katika matengenezo. Rais alifanya ziara ya kutembelea daraja hilo lakini alipofika alishangazwa na kutokuwepo kwa Waziri mwenye dhamana kwa kipindi hicho ambapo alikuwa ni Basil Mramba ambaye alipaswa kuwemo kwenye ziara hivyo. Inasemekana kuwa Mramba alikuwa hana taarifa kuhusu ziara hivyo.

7.
Uzinduzi wa Hotel ya Snow Crest -Arusha
Hivi karibuni Rais alipozindua hotel ya kimataifa ya Snow Crest Arusha iliyojengwa ka gharama ya shilingi bilioni 10 lakini baadaye hotel hiyo ilivunjwa na wakala wa Barabara Tanzania(Tanroads) kwa kuwa ilikuwa imejengwa ndani ya eneo la barabara..Hii pia ni aibu kwa Rais.

8.
Sakata la Mahujaji
Mwaka 2007 Mahujaji walikwama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kukosa ndege ya kuwapeleka Makka.Rais aliwahoji wasaidizi wake na kujibiwa kuwa tayari ndege imeshaandliwa kwaajili ya kuwasafirisha.

Rais alishuhudia baadhi ya Mahujaji hao wakipandishwa kwenye ndege lakini baada ya yeye kuondoka Mahujaji hao walishushwa kwa madai kuwa ndege hiyo ilikuwa na hitilafu. Ilikuwa ni changa la macho kwa Rais.

9.
Kuzidiwa Jukwaani/kwenye Mkutano Muhimu
Mwishoni mwa mwaka jana afya ya Rais ilitetereka mpaka kupelekea kushindwa kuhutubia mamia ya waumini wa Kanisa la AICT na wanachi wengine katika uwanja wa CCM Kirumba.Rais alibebwa na watu wa usalama wa Taifa na kupelekwa kwenye chumba cha kumpumzika.

Rais pia alizidiwa na kupelekwa kwenye chumba cha mapumziko alipokuwa kwenye mkutano wa Sulivan uliofanyika jijini Arusha. Kwa nchi yeyote ile iliyoendelea Rais hapaswi kuzidiwa anapokuwa jukwaani au kwenye mkutano wowote.Rais ana dakatari anyelipwa vizuri hivyo anapaswa kujua afya ya Rais wakati wote.

Haya ni baadhi tu ya matukio ambayo kwa mtazamo wangu naona yalimdhalilisha Rais na hivyo kutufanya watu tuhoji utendaji wa Rais na Serikali yake kwa ujumla. Na mengine yanakuja kabla hatujaingia Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.



 
hoja nzuri, mtazamo mzuri, mpangilio mzuri............... nimecheka mahujaji waliopandishwa kwenye ndege na alipoondoka wakashushwa!!.... hahah... kweli only in tz..... huyu mheshimiwa anapaswa kuwa mkali kidogo, wamemfanya babu yao................
 
hoja nzuri, mtazamo mzuri, mpangilio mzuri............... nimecheka mahujaji waliopandishwa kwenye ndege na alipoondoka wakashushwa!!.... hahah... kweli only in tz..... huyu mheshimiwa anapaswa kuwa mkali kidogo, wamemfanya babu yao................

Hii nimeipenda..Thanks..Habari ndio hiyo jamaa alidanganywa laivu,ni kweli wanamfanya babu yao..Si ni rafikia zake walijua kuwa hawezi kuwafanya kitu.
 


9. [/SIZE][/FONT] Kuzidiwa Jukwaani/kwenye Mkutano Muhimu
Mwishoni mwa mwaka jana afya ya Rais ilitetereka mpaka kupelekea kushindwa kuhutubia mamia ya waumini wa Kanisa la AICT na wanachi wengine katika uwanja wa CCM Kirumba.Rais alibebwa na watu wa usalama wa Taifa na kupelekwa kwenye chumba cha kumpumzika. Rais pia alizidiwa na kupelekwa kwenye chumba cha mapumziko alipokuwa kwenye mkutano wa Sulivan uliofanyika jijini Arusha. Kwa nchi yeyote ile iliyoendelea Rais hapaswi kuzidiwa anapokuwa jukwaani au kwenye mkutano wowote.Rais ana dakatari anyelipwa vizuri hivyo anapaswa kujua afya ya Rais wakati wote.

Hili mkuu naona ni lakuokoteza. Sio aibu wala kudhalilika mtu anapougua ghafla na wala hakuna kiumbe (dokta) anayeweza kumkagua kiumbe mwenzake na kumhakikishia kwamba hawezi kupatwa na ugonjwa wa ghafla.
 
Hili mkuu naona ni lakuokoteza. Sio aibu wala kudhalilika mtu anapougua ghafla na wala hakuna kiumbe (dokta) anayeweza kumkagua kiumbe mwenzake na kumhakikishia kwamba hawezi kupatwa na ugonjwa wa ghafla.

Rais wa nchi anapaswa kuchekiwa afya yake mara kwa mara..Hivyo kuzidiwa na kushindwa kuhutubia jukwaani ni tatizo na ni aibu.Kwa nchi zilizoendelea hali kama hii ingejitokeza ama daktari wake au wasaidizi wake wangekuwa responsible kwa hili..Huu ni mtazamo wangu...
 
Rais wa nchi anapaswa kuchekiwa afya yake mara kwa mara..Hivyo kuzidiwa na kushindwa kuhutubia jukwaani ni tatizo na ni aibu.Kwa nchi zilizoendelea hali kama hii ingejitokeza ama daktari wake au wasaidizi wake wangekuwa responsible kwa hili..Huu ni mtazamo wangu...

Hapana, mtazamo wako haumtendei haki JK hata kidogo. Kuchekiwa afya mara kwa mara kamwe hakumaanishi kwamba anayechekiwa hawezi kuugua ghafla. Kwa hiyo mimi nikiugua ghafla ni nani anapata aibu; mimi ninyeugua, dokta wangu, au watu wanaoniona nikikimbizwa kwenda hospitali?

Mkuu sio kweli kwamba ingekuwa katika nchi zilizoendelea dokta au msaidizi wake angeachichwa kazi. Kama ndio hivyo madktari wa watu binafsi USA, UK na Canada wangekuwa wanafukuzwa kazi kila kukicha mana kila siku watu wenye madaktari wao wanapata shinikizo la damu na strokes, wengine wanadondoka, wengine wanapata mshituko wa moyo wakiwa wanaendesha n.k. Sasa hapa sijui aibu anapata nani? JK kadhalilika kwa mengi yakiwemo hayo 8 uliyoyataja, ila hili la kuugua ghafla kwa kweli nimefaulu kushawishika bila mafanikio.
 
2. Kujiuzulu kwa Waziri Mkuu-Edward Lowassa

Kwa kuwa Waziri Mkuu anateuliwa na Rais tena wakati mwingine bila kushauriana na mtu kitendo cha Lowassa kulazimika kujiuzulu baada ya kashfa ya Richmond ilikuwa ni pigo jingine kwa Rais. Hii inamaanisha kuwa Rais wetu hayuko makini katika teuzi zake ndio maana anateua watu ambao sio viongozi wasafi wasio na dhamira ya dhati ya kuongoza taifa hili. Hii ni aibu nyingine kwa Rais kwani mtendaji wake mkuu aliyempenda kuliko Mawaziri wote kumuangusha kwa utendaji wake mbovu hivyo kulazimisha kuvunjwa kwa baraza la Mawaziri na kumteua mtu mwigine ambaye hakuwahi kumfikiria kuwa Waziri Mkuu


HII MBONA iko vice versa? siyo kuwa JK alipata heshima sana nje ya nchi kuwa na waziri mkuu anayekubali kuwajibika?

Pili je Kudhalilika huko huko utawapa kila rais dunia hii? watu wanabadilika sana, na Rais kamwe hayuko kuwa kama Mola wa kuweza kujua yajayo.

Then Nyerere alidhalilika Mwinyi alipojiuzulu? No sitaki kuikubali sana hii point labda ungeandika kivingine
 


. Rais pia alizidiwa na kupelekwa kwenye chumba cha mapumziko alipokuwa kwenye mkutano wa Sulivan uliofanyika jijini Arusha. Kwa nchi yeyote ile iliyoendelea Rais hapaswi kuzidiwa anapokuwa jukwaani au kwenye mkutano wowote.Rais ana dakatari anyelipwa vizuri hivyo anapaswa kujua afya ya Rais wakati wote.


...du hii ya arusha ..wengine tulikuwa hatujaipata na mkutanoni tulikuwepo full time....tumtendee haki muungwana kwa kumpa tuhuma za kweli....ie...kushambuliwa mwanza,kuanguka jangwani,kuzidiwa mwanza ...etc....hii ya arusha inaweza kuwa kweli lakini haina ushahidi....kama inavyosadikika pia kuwa huzidiwa mara kwa mara ....inakuwa haina ushahidi....
 
...bila kusahau kwamba alipokea jezi ya mchezaji wa Real Madrid Ikulu..."what a shame"
 
Mkuu nadhani umeanzisha chachu maana naona hii thread itakuwa na matukio mengi kuliko ulivyodhani, wewe umekumbuka Tisa lakini nina uhakika yatakuwa 100 na hayo baada ya kuchuja na kuyaondoa yale ambayo tutaona sio ya aibu, kama la kupanda bembea sioni kama ni Aibu I was in Jamaica kwa likizo ya dec 2008 hilo ni utalii wa kawaida Jamaica kwa kila mtalii anayeingia kwao.

lakini matukio ambayo mimi ningempa ni mawili (ingawa hapa nataja zaidi).
1. Msafara wake kupigwa mawe kule Mbeya.
2. Msafara wake kuzuiwa barabarani Mbeya ili wananchi watoe kero ya kujengewa soko na pia kero ya matuta bara barani
3. Kuruhusu binti yake kuchezwa ngoma
4. Kurusu mama wa kwanza kwenda Swaziland kushiriki Ngoma ya Reed Dance
5. Kuzuiwa kumpa mama wa Kwanza ashike Kombe la dunia la FIFA uwanja wa Taifa
6. Kudanganywa ujenzi wa Daraja mto Ruvuma (Tanzania - Msumbiji) kuwa limekamilika wakati bado, na kujaribu kumpandisha kwenye ki-boat.
 
...bila kusahau kwamba alipokea jezi ya mchezaji wa Real Madrid Ikulu..."what a shame"

Binafsi nisingeona shida kupokea Jezi, hilo limekaa kishabiki zaidi lakini lakupokea msaada wa Yebo Yebo kutoka China lile lilinishtua kiasi.
 
Alishawahi kwenda kichwakichwa kugawa pikipiki Arusha bila kujua ni za nani, ikabidi achomoe.
 
Alishawahi kwenda kichwakichwa kugawa pikipiki Arusha bila kujua ni za nani, ikabidi achomoe.
Thanks Tindikali umeniwahi na mimi nilitaka kuchangia hilo. Inakuwaje mtu wa EPA anaendelea kuwepo kwenye kwenye protokali za chama na usalama wa taifa wanamwangalia hadi rais mwenyewe aje kushtukia?
 
nina neno moja tu kwa wasaidizi wake (ambao wengi amewateua yeye wamlifrect)
INCOMPETENT
 
Waoh this is great Presidaaa we have here,

HE KNOWS EVERYWHERE AND EVERYONE OUTSIDE TANZANIA and HAS COMPLETELY FORGOTTEN POOR ALIBINO'S KILLED EVERY DAY (WHAT HAPPENS TO THOSE KILLERS) CANT THE PRESIDENT SAY, DO, COMMENT,ACT POSITIVELY ON THIS. ( TO FAVOUR OUR BROTHERS AND SISTERS)
 
kuoa mke wa nne mtoto wa zakia meghji hivyo kuzihirisha wazi ule msemo wa serikali ya kishikaji kwa kuwa huyo mama aliwahi kuwa waziri kwenye serikali yake so mama mkwe wa mkulu,
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom