Elections 2015 Matukio na Matokeo toka maeneo mbalimbali ya Tanzania - Uchaguzi Mkuu 2015

Ukawa kwisha habari yao! ni kama kafulila anavyopotosha umma kuwa anaongoza kwa kura huku akitambua fika. kapigwa kipigo cha nguvu na Iron Lady Hasna S.K.
 
Ukawa kabla hata ya uchaguzi tulijua mtalalamika ka vile mtaonewa huruma na kuambiwa haya chukueni hiki au kile.

Watu tunataka - hapa kazi tu

Wavivu wote wawajibike na wapenda rushwa aaaggghhh

Na Jembe kukaa muhula ujao atainyoosha tu hii nchi aaagghhh


Vigelegele
 
Ni kweli mkuu mwanzo mzuri mabadiliko hayaji kama kumuua sisimizi ni hatua,SASA NI KUFANYA KAZI NZURI KTK HALMASHAURI NA MIJI NA MAJIJI MULIYOYACHUKUA ILI MUWAONYESHE WALE WALIOWAACHA NI JINSI GANI MUNAWEZA.
 
Kusoma mpaka chuo kikuu siyo kigezo cha kuwa mwadilifu (walisema lowasa hana maadili ni fisadi ila hao hao akina professor Baregu wanasema siyo fisadi)

Kuwa mchungaji siyo kigezo cha kuwa mwadilifu (wachungaji wengi mfano kakobe, gwajima, mwingira walilalamikia mno serikali ya ccm kusema ina ufisadi na ilikuwa huwezi kutaja ubadhirifu serikalini bila lowasa au sumaye, ila kipindi cha uchaguzi eti sumaye, lowasa, ni watu safi na walitenda mema wanahimiza tuwape nchi).

Uadilifu ni zawadi toka kwa Mungu
 
1390616702918272.jpg
 
Hivi Jamani tuseme ukweli kasoro zipo kama segerea. Kama yule dada wa segerea alijitoa utamlaumu vipi??

CUF WAMEPATA MAJIMBO 23 mpaka sasa huoni kama ni faida sana kuwa ukawa

CHADEMA 35 na isingekuwa kanda ya ziwa kuitosa CDM cdm wangekuwa hata na wabunge hata 60

UKAWA IMESAIDIA MNO TUSIBEZE KIRAHISI

Faida zipo na hasara zipo ila faida inaonekana jamani.

Uwepo wa LOWASA umesaidia pia tusibeze...kabisa

Watz wamejitahd sema magoli ya maradona.

Lengo la UKAWA haikuwa kupata wala kuongeza majimbo ilikuwa kupata Raisi
USIMPANDISHE PRESHA LOWASA NA VIONGOZI WA UKAWA.Mbowe alikuwa kajiandaa kuwa waziri mkuu dili limetibuka
 
Majimbo mengi yaliyochukuliwa na CUF au Chadema yangebaki ccm kama si uwepo wa maridhiano...
Pia tuna mtaji mkubwa wa kura hata majimbo tuliyoshindwa ambayo itaongeza nafasi za viti maalum.

Tuwapongeze maana ni rahisi kuwazodoa lakini kupambana na chama dola sio jambo jepesi.
 
Wadau, poleni sana kwa wale wenzetu wa UKAWA. Najua wapo wengi humu waliotubeza na kututukana kwa sababu tu eti tunakitetea chama tawala, chama pendwa. Tulivumilia matusi hayo na kejeli tulizopewa. Tena wengine walienda mbali na kutuambia kuwa tutafute pa kujificha pindi Lowasa atakapotangazwa mshindi.


Namshukuru Mwenyezi Mungu. Chaguo langu na la Watanzania wote, John Pombe Magufuli anazidi kuchanja Mbuga. Natoa wito kwa wapinzani wote nchini. Kubalini matokeo. Hapa hata mfanyeje hamuwezi kupindua matokeo. Mikakati mnayopanga ya kutaka kugomea matokeo hayatawasaidia kitu. Kila kitu kipo wazi na Watanzania tunajionea wenyewe.


Jipangeni kwa ajili ya uchaguzi wa 2025
 
Mie nimejifunza kutoamini vyombo vya habari na kutowaamini wanasiasa hasa akina banili....eti "Hakuna uadui wa kudumu kwenye siasa na tumebadili gia angani"mmmmmmm
 
Cha Msingi jamaa wamesha tuzidi Ujanja hakuna jinsi Wamuapishe tu Magufuli

dont loose hope my brother still you have a chance......but next time msiweke effort yote mijini tuliwaaambia mkajitutumua kuwa hadi vijijini mnakimbiza kiko wapi leo?????
 
Watanzania wameshatimiza wajibu wao kwa kupiga kura kuchagua viongozi wao oktoba 25.

Kazi iliyobaki sasa ni kwa tume kuyatangaza matokeo na washindi.

Kauli zozote za kuhamasisha uvunjifu wa amani zisipewe nafasi.

Tume zisiingiliwe katika kutimiza wajibu wake kikatiba.

Tujifunze kusubiri na kuyapokea matokeo kwa maslahi mapana ya Taifa.
 
Japo malengo yalikuwa makubwa zaidi ila sip mbaya, na bado majimbo mengine tutashindia mahakamani.........ila niseme tu hapa kuwa baada ya haya mambo kupita UKAWA wahakikishe wanafanya kitu tofauti ili vijana wazidi kuhamasika kuwa nao bega kwa bega, vijana wamefanya kazi kubwa nikichukulia mfano wa ukonga kwa Jerry, Kawe kwa mdee, kibamba kwa Mnyika.....vijana walijitolea mpk usiku mkubwa kuhakikisha uhuni haufanyiki na matokeo tumeyaona.
 
Back
Top Bottom