Nimecheka kinoma tena kwa sauti .Umesahau kuwa ili uwe dereva ulifanyiwa usahili na Traffic hao hao,Umesahau ukipata ajali wanakuhudumia ili upate kulipwa bima ni hao hao,Umesahau kuwa hao hao ndiyo wanaoongoza misafara yote viongozi wa nchi,Umesahau kuwa hao Traffick ndiyo wanaoongoza hili jiji LA Dar es salaam katika junction .Umesahau kuwa magari yote ya hili jiji asubuhi yanakwenda posta na kariakoo na jioni ndiyo yanarudi ,He Umesahau wanaomiliki magari wengi wao wanatokea kuanzia mwenge kueleke boko?.Kumbuka tena kuna barabara nyingine kutoka salender bridge kuja mwenge zina magari mengi sana na zinajaza magari bagamoyo road. Mwisho nakokotoa kwa kusema taifa hili linawhandisi majinga kuliko waandisi wote duniani wameshindwa kubuni mbinu mbadala ya kutatua foleni za hii nchi wameachia Traffic wafanye hiyo kazi. Mwisho wewe unayetokea Ubungo huu muda huna umuhimu sana kama anayetokea Posta maana ofisi zote za serikali zipo Posta ofisi za mashirika na makampuniy makubwa zipo posta,mabenki yote yapo posta na wanaotokea airport wanapita nyerere road wanaingia Ally hassan mwinyi kisha Bagamoyo road .Sasa wewe umetoka wapi?.Bila shaka wewe ni mpiga debe wa pale Ubungo stendi unatusumbua wasafiri tunaotaka kwenda mikoani. Kumbuka tena huwezi kupata elimu ya Usalama barabarani kokote kule bila kuwa afisa wa polisi maana wewe utafundishwa kanuni,sheria na alama za barabarani,Ila hutofundishwa barabarani gani ipendelewe zaidi kuliko nyingine,Hutofundishwa kujua misafara ya siri yaviongozi inakuaje,Hutofundishwa majambazi wablokiwa vipi barabarani,Hutofundishwa kupeleleza ajali inapimwa vipi ,Hivyo hata use na PHD yako ya nyuki au kujenga maghorofa bila kwenda chuo cha polisi wewe ni mbumbumbu sana kuliko yule form failure unayemsema ambaye amefundishwa kufanya kazi kama mwanajeshi inapobidi kutumia medani hizo rejea kumbukumbu ujambazi Ubungo ,kufanya kazi kama daktari anapokuokoa unapopata ajali au kuzoa mzoga wako unapkuwa umesagwa na lorry, anapofanya kazi kama mwanasheria anapokupeleka mahakamani upate haki yako ulipwe bima au ufungwe kwa madhara uliyesababisha ,Kumbuka Huyo ndiye anayskuokoa kwa kukumbusha funga mkanda ukipata ajali utachomoka. Tuulizane swali rahisi tu hivi MTU Aliyepata form Four failure ndiye anayeajiriwa na serikali? Hivi wewe kwenye hicho chuo kikuu ulichosoma hakuna wahitimu wanaofanya kazi polisi? Je hao unaowajua unafikiri wakati wanaajiriwa walianzia na cheo kikubwa?.Je unafikiri huyo Traffic anayekupimia ajali uliyesababisha,unayekujazia taarifa zako vizuri mpaka unapata lesseni, anayekutolea ushaidi mahakamani mpaka unafungwa ? Bado unaamini hana elimu.Je wahitimi wa vyuo vikuu huwa wanafanya usahili wa ajira katika polisi ili iweje .au ukishajiliwa na polisi tu hata kama unaphd unakuwa form four failure. Acha hasira kwa vitu usivyovijua umaskini wa nchi hii ni mkubwa sana na aibu kubwa inaficha na hawa Mapolisi maana bila kufanya hayo wayafanyao mambo huwa hovyohovyo .