UZZIMMA
JF-Expert Member
- Nov 20, 2014
- 406
- 456
Habari yenu katika ujenzi wa maisha yenu. Nimehitimu chuo 2020 stashahada ya uhandisi majengo katika chuo fulani cha serikali hapa nchini.
Tatizo kubwa matokeo yangu yamekosewa katika mfumo wa NACTE na hii imekuwa ni kikwazo nisiweze kuendelea na masomo.
JITIHADA NILIZOZIFANYA KWA SUALA HILO
Baada ya kuthibitisha matokeo yangu yamekosewa NACTE mimi nikafwata uongozo wa chuo upande wa academic. Nikaambiwa niandike barua ya maombi yangu.
Baada ya kuandika barua nikakaa kama mwezi mmoja nikaenda chuo kusikilizia ombi langu. Nikaambiwa chuo kimeandika barua NACTE kuhusu swala langu. Nikasubiri kama miezi mitatu huku nikiulizia chuoni kama barua ilioandikwa kwenda NACTE imejibiwa.
Kiukweli siku zote nilizowasiliana na chuo changu nikaambiwa barua haijajibiwa.
Nikaamua kwenda kwenye ofisi za NACTE kusikilizia swala langu. Baada ya kwenda nilienda na matokeo yaliomo kwenye ststem halisi ya chuo.
Majibu nikaambiwa NACTE hawajapokea barua yoyote inayohusu madai yangu kutoka chuoni.
Na ili nisaidiwe ni lazima CHUO HUSIKA ndio watume barua.
Baada ya kurudi chuo tena kueleza yaliojiri NACTE chuo kinadai kimetuma barua NACTE, ila kwa kuwa haijashughulikiwa watatuma barua nyengine.
Imepita takeiban miezi minne tangu niende chuoni kufwatilia madai yangu kwa mara ya mwisho, leo hii nimeongea nao wakanimbia barua ya pili wameshaituma NACTE ila majibu hawajapata.
Jamani naombeni msaada tafadhali niipate haki yangu. Bado sijakata tamaa kutafuta haki yangu.
Ni mimi binadamu mwenye uchungu wa elimu.