Matokeo ya Uchaguzi Uzini - Raza (CCM) aibuka kidedea!

Matokeo ya Uchaguzi Uzini - Raza (CCM) aibuka kidedea!

Tegemea kupata vichwa vya habari hivi katika magazeti ya kesho: 1-CHADEMA YAANGUKIA PUA UZINI. 2-JOPO LA UONGOZI WA CHADEMA LAONDOKA UZINI KIMYA KIMYA NA KUSAHAU MAHEMA YAO- ni baada ya kugaragazwa vibaya sana na CCM, 3-CHADEMA WASAFIRISHWA KWA KUTUMIA MAJAHAZI KUELEKEA BONGO -ni baada ya kutumia pesa zote katika kampeni jimbo la Uzini na kusahau kujiwekea nauli, 4-CUF YAAMBULIA NAMBA MBILI UCHAGUZI WA UZINI NA KUWAACHA CHADEMA WAKIPIGWA NA BUTWAA!
Ndiyo mnavyodanganyana kule mzalendo.co
 
Daudi Ismail Isma Jamani kura zimenza kuhesabiwa hapa
uzini katika kituo cha miwani
wamepata kura 14 kwenye kura miane
raza oyee ushindi unakuja.
 
Ni kweli kwamba ccm watashinda, lakini matokeo uliyoyaweka hayana ukweli.
Sisi hapa Zenji tunasubiri matokeo bado hayajatangazwa
unyanyungu A
CCM 78
CUF 21
CDM 3

UNYANYUNGU B
CCM 77
CUF 18
CDM 6
 
this is a ****,nimewaambia chadema kule
hamshindi ila mna jitangaza zenji vizuri sasa.

Tatizo ni wewe na sio CDM kushinda au la! Kama ni kweli inaongoza, ni kuwa hoja yako ya 'CDM haitashinda' ni ishara ya ugonjwa wa wanaCCM wengi kudhani bado wamesimama au wako makini kumbe ni marehemu mtarajiwa, ndio maana wanachakachua ili kumaintain status quo, hadi waambiwa chama kilichakufa. Hata CDM isiposhinda, ikipata idadi nzuri ya kura kama inavyoelekea, ni picha ya kupotea kwa CCM na mchumba-ke Cuf. Tusubirie majibu yatatuthibitishia.
 
Daudi Ismail Isma kada wa CCM on facebook say "Jamani kura zimenza kuhesabiwa hapa
uzini katika kituo cha miwani
wamepata kura 14 kwenye kura miane
raza oyee ushindi unakuja." Naamini yupo Uzini muda huu na ni Wakala wa CCM.
 
Waliopo kwenye scene of incident watupe taarifa jamani lah! choka kusubiri
 
Wakuu maeneo mengi upigaji kura umekwisha. Sasa shughuli ya kuhesabu kura imeanza. Lakini kuna rabsha na faulo nyingi zinaonekana kufanywa kwa makusudi kwa nia ya kuvuruga uchaguzi na hatimaye kupata matokeo yatakayoendeleza 'status quo'.

Mawakala hodari na makini wa CHADEMA wameweza kubaini uwepo wa wapiga kura kutoka majimbo mengine, kama vile kutoka Kitope, Mjimkongwe na majimbo mengine, tena wakiwa na vitambulisho vya kutoka majimbo hayo. Mathalani katika vituo vya Ghana mawakala wa CHADEMA wamewabaini intruders wapatao 40, kituo cha Mitakawani wamebaini intruders wapatao 50, hali ilikuwa hivyo takribani katika vituo vingi.

Inavyoonekana hawakuletwa tu kupiga kura, lakini pia wameletwa kwa ajili ya kukaa vituoni. Karibu kila kituo cha kupigia kura kuna watu takriban mia. Imebainika kuwa lengo lao ni kutaka kuzuia vyama vya upinzani, hususan CHADEMA ambayo imetoa upinzani mkiubwa kwa status quo kwa Uzini, visiweze kutoka na nakala za fomu za matokeo.

Katika kila kituo, kuna watu, wakiongozwa na masheha, wanaandika majina ya watu wanaotoka ndani kupiga kura. Wanawatisha kuwa wakipigia kura upinzani, hususan chama mbadala CHADEMA, watabainika na watachukuliwa hatua!

Kuna kijana wetu mmoja alikuwa anapiga picha katika eneo la Umbuji. Polisi wakamkata na kumnyang'anya vifaa vyake, ikiwemo kamera aliyokuwa akitumia. Baada ya consultations za hapa na pale, ikaonekana kuwa tatizo ni kutokuwa na kitambulisho cha kumruhusu kufanya hivyo. Hivyo ikashauriwa kama tatizo ni kitambulisho, basi asiruhusiwe lakini vifaa vyake arudishiwe na yeye aachiwe. Wakati polisi wakiwa katika kuhakikisha hilo linafanyika, akawasili Seif Khatib, akaamuru kijana asipewe vifaa hivyo, asiachiwe na atiwe ndani kwa mwezi mmoja.

Lakini haki imeshinda baadae. Kijana ameachiwa. Kura zinaendelea kuhesabiwa. Tutajuzana, hata kama ni usiku wa manane. Kila linalojitajika kujadiliwa, litawekwa hapa, bila upendeleo. Asanteni wakuu. Nawasilisha.

Updates;

Ngoma sasa iko kwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Uzini. Matokeo yanaendelea kukusanywa na kufanyiwa majumuisho kwenye kompyuta. Mechanism yetu pia inaendelea kukusanya matokeo yote ya kura zote. Uchaguzi umetawaliwa na vitisho na ubabe mwingi. Mpaka sasa zipo taarifa juu ya CCM kuweka ofisi ndogo katika kila kituo cha kupigia kura. Wakiwakamata wapiga kura na kuwashikisha vitambulisho vya kupigia kura. Wakitoka kupiga kura anakuwepo mtu maalum anawapatia pesa.
 
Tatizo ni wewe na sio CDM kushinda au la! Kama ni kweli inaongoza, ni kuwa hoja yako ya 'CDM haitashinda' ni ishara ya ugonjwa wa wanaCCM wengi kudhani bado wamesimama au wako makini kumbe ni marehemu mtarajiwa, ndio maana wanachakachua ili kumaintain status quo, hadi waambiwa chama kilichakufa. Hata CDM isiposhinda, ikipata idadi nzuri ya kura kama inavyoelekea, ni picha ya kupotea kwa CCM na mchumba-ke Cuf. Tusubirie majibu yatatuthibitishia.

Hiyo red inaonesha unge fupisha kuongea kwako na ukasema kwa ufupi tu kwamba
"Naunga mkono hoja yako".......
 
Daudi Ismail Isma Uzini kituo cha kiboje school chadema
kura 15 ,cuf kura kumi na mbili ,ccm
kura 194.shangilia ushindi unakuja
shangalia shangilia unakuja.
 
Asante kwa taarifa, kuna uzi mmoja huko nyuma umetupa matokeo yasiyo ya kweli,tumeishia kulumbana tu. Tunasubiri matokeo halisi mkuu.
 
safi sana kwa uchambuzi wako mzuri. hebu tupe dondoo za awali haraka kama utakavyoweza
 
Daudi Ismail Isma Uzini kituo cha kiboje school chadema
kura 15 ,cuf kura kumi na mbili ,ccm
kura 194.shangilia ushindi unakuja
shangalia shangilia unakuja.
 
Daudi Ismail Isma Jamani kura zimenza kuhesabiwa hapa
uzini katika kituo cha miwani
wamepata kura 14 kwenye kura miane
raza oyee ushindi unakuja.

Hiyo ni namba ngapi vile?
Kumbe wapemba wote mna fanana na MS eh.
 
DSC_1315.jpg

DSC_1319.jpg

DSC_1311.jpg
 
Back
Top Bottom