Ieleweke kwamba ndani ya Zanzibar vyama vyenye nguvu ni viwili tu; CCM na CUF. Na katika vyama hivi kila Chama kina Anga yake za mashumbuli ambazo hua zinazitegemea, na kwa hakika Anga ya Uzini ni miongoni mwa moja kati ya Anga ambayo CCM inaitegemea ikijumuishwa na Donge na maeneo mengine kama ilivyo kwa CUF na maeneo yake. Na ushahidi wa haya angalia hata matokeo Uchaguzi wa Raisi 2010 na miaka mengine iliyopita. Kusema kwamba CUF imepata nafasi ya tatu kwa sababu ya CHADEMA kuivamia Zanzibar ni zaidi ya kusema uongo! Hata hivyo chama cha CUF chaguzi kama hizi za Wawakilishi, Wabunge na Madiwani hua hawazipanii sana na wengi wa wanachama wao hua hawaendi kupiga kura siku ya uchaguzi (Uchaguzi wa Uzini kuna watu zaidi ya 4000 hawakupiga kura) tofauti na CCM wapenda ngoma, ubwabwa, kofia za bure, wanawake wa 'kuserebuka' nao nk na hili ni kosa kubwa panapohusika siasa. By the way kwa sasa Wazanzibari kwa asilimia kubwa hawaelekezi nguvu zao katika vyama tena (wameondoa ushabiki wa kishamba) bali wanataka Zanzibar iliyo huru kwanza, na mambo mengine yatafata baadae!