Matokeo ya Uchaguzi Uzini - Raza (CCM) aibuka kidedea!

Matokeo ya Uchaguzi Uzini - Raza (CCM) aibuka kidedea!

Mkuu, tupe updates!

Ni kweli Raza kasinda kwa zaidi ya kura elf tano na mia saba na msindi wa pili ni Mgombea wa CDM ana kura 281, na watatu ni 200 na kidogo, na NRA 14, SOURCE radio one breacking news sahizi.
 
ritz!
Sina data zakunifanya kuona chadema kama ingeshinda uko ila ilinifanya nijiulize kwanini umjilipua hivyo kwa ahadi ngumu kiasi kile?

Ungekuwa unazifahamu siasa za Zanzibar wala usingenishangaa, ndio maana chaguzi za bara siwezi kujilipua hivyo.
 
Mleta mada kimsingi sikupingi unachokiripoti,ila najiuliza kwa nini hujaweka source ya habari zako,pili ushindi huo umekaaje?kwa maana ya idadi ya kura.Rudi hapa tena ukiwa na updates

Source Radio one breaking news
 
TBC taarifa ya habari saa 2:
CCM 5377
CDM 281
CUF 23
tadea 14
AFP 8
 
Hii ni mbaya sana kwa team nzima ya chadema takwimu zilizotolewa hapo hata msijipe matumaini ila mjiulize mlienda kufanya nini uko? unapoingia field au kwenye trade test at list score should be 30-45% ila kwa hii inakua kama mtoto wa mkulu pale magogoni.
Sasa mnatoka na majibu mepesi or tumejitaidi hw? kutoka Igunga, Uzini na sasa mnaenda Arumeru mnatuambia nini nyie campaigner wa CDM include top leaders? ambarrassed at all.
 
Leo umedhihiri ule ukweli kuwa cdm ndo chama kikuu cha upinzani tz.Ni uhakika kuwa chama kikuu cha upinzani tz-chadema kumbe kina uwezo mkubwa wa ku-penetrate even the isles of Zbar very soon.Hv punde matokeo ya uchaguz jimbo la uzini yametangazwa na ccm-5377, CDM-281, na mnyonge maskini cuf jamani,cuf jamani nasema tena si yu efu wamepata kura 223.Mm niseme 2 ile fursa ya cdm kuingia hku kwetu zbar imefika,kilichobaki hapa ni mikakati ya kuwaondoa hawa ma-cuf hapa zbar ya ku-hold upinzani pasipo mwlkeo

Kwa kweli nionavyo mimi sio mwanzo mbaya kwa siasa za huko visiwani, hongera CDM na hongera RAZA kwa ushindi. Lakini kwa kweli watanzania bado hawajifunzi kutokana na makosa yao. Lakini watanzania bado hawajajifunza kutokana na makosa yao! Mimi siwezi tena kuilamu serikali kwa mambo yanayotokea bali wananchi walioiweka hiyo serikali madarakani.Jay Z aliwahi kusema "men lie, women lie, numbers dont". Kwa uwiano huo, utagundua Watanzania wengi bado wana walakini katika ufanyaji wa maamuzi sahihi.

Jay Z aliwahi kusema "men lie, women lie, numbers dont". Kwa uwiano wa huo ushindi, utagundua Watanzania wengi bado wana walakini katika ufanyaji wa maamuzi sahihi. Binafsi sikutegemea CDM ishinde kirahisi huko Uzini but nilitegemea wanauzini wangetuma ujumbe mzito sana kwenye Ballot Box jumapili hii. Sasa kwa matokeo haya tegemeeni mkiwaona CCM na Serikali yake wakizidi kubweteka na kusherekea ushindi, wakati wananchi wanazidi kutaabika.


 
Ni kweli Raza kasinda kwa zaidi ya kura elf tano na mia saba na msindi wa pili ni Mgombea wa CDM ana kura 281, na watatu ni 200 na kidogo, na NRA 14, SOURCE radio one breacking news sahizi.
watatu cuf amepata kura 20 TBC1 habari
 
Ndg wana JF, tar11/02/2012 siku ya jumamosi nilifanikiwa kuhudhuria hafla fupi pale Kibo Palace Hotel Arusha, wakati Kijana Machachari wa Chadema Arumeru Mashariki Kamanda na mpambanaji Joshua Nassary alipotangaza nia yake ya kuomba kuteuliwa na Chama chake cha Chadema aweze kupeperusha bendera ya chama hicho ktk kinyang`anyiro cha uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni hapo.
Mwitikio niliouona umenifanya nishawishike kushiriki nanyi kilichojiri,
1. Idadi ya watu waliojitokeza kumuunga mkono ilikuwa ni nyingi mno tofauti na matarajio ya wengi, kinababa kinamama bila kujali itikadi zao za chama,vijana wa kiume na kike walijitokeza kwa wingi kumuunga mkono, watumishi mbalimbali wa serikali walijitoa kwa hali na mali na kuahidi kuwa naye bega kwa bega hadi wahakikishe wanaupata ukombozi kamili,
2. Michango ya papo kwa hapo ilifanyika na ndani ya dakika chache zikapatikana kianzio cha zaidi ya Tsh 11,000,000/= Milioni kumi na moja ikiwa ni cash na ahadi, Magari nane yenye uwezo wa kwenda sehemu korofi pamoja na mafuta yake kwa wakati wote wa kampeni yalipatikana kama kianzio , Vyombo vya Kupazia sauti vya uhakika kwa muda wote wa kampeni, watu mbalimbali walijitolea nyumba na vyakula sehemu tofauti tofauti, pia walijitolea vijana wa kike na kiume, wababa na wamama kwenda kuweka kambi vijijini kwa muda wote wa kampeni hadi wakati wa kumalizika uchaguzi na kutangazwa matokeo. hii imeonyesha ni jinsi gani watu wanamkubali huyu kujana na ni wazi watu wameichoka CCM hata vijijini.
 
CDM si haba. Kura 200 nafasi ya pili inatosha kwa jaribio la kwanza. Imeonyesha kwamba CDM inaweza kujipenyeza huko zanzibar na kubadili hali ya kisiasa hasa baada ya kutawaliwa na vyama vya CCM na CUF pekee. Kuishinda CUF huko zanzibar kuna ujumbe mpana sana.
 
kwa mujibu wa itv taarifa ya habari saa mbili ni kwamba bw. Raza ameshinda kwa kura zaidi ya 5,000 akifuatiwa na Chadema na cuf ya tatu.
 
Kwa mujibu wa Zec Ccm ya kwanza kwa kura 5568 ikifuatiwa na Chadema kura 286 na ya tatu ni Cuf kura 21.
Source Tbc 1
 
Back
Top Bottom