BAK,Wapinzani hawatapata mafanikio yoyote katika chaguzi za Tanzania bila ya kuungana. Watanzania tumewapigia kelele juu ya umuhimu wa kuungana ili kuunda chama kimoja chenye nguvu. Hata Waziri Mkuu wa Kenya Odinga alipitembelea Tanzania ili wapate mafanikio ya kuing'oa CCM madarakani inabidi waungane, lakini wapi.
Kama wameshindwa huku Mbeya vijijini hakuna wa kulaumiwa bali ni wao wenyewe wapinzani. Hii danganya toto ya vyama vya upinzani 'vina ushirikiano' haitawafikisha kokote bila kuvunja vyama vilivyopo na kuunda chama kimoja chenye nguvu.
2010 inakaribia na dalili si nzuri maana bado kuna mgawanyiko mkubwa miongoni mwa Wapinzani. CCM haistahili kuendelea kuwa madarakani kutokana na matatizo mbali mbali yakiwemo ya mafisadi, lakini Wapinzani kwa kutotaka kuungana wanaisadia sana CCM kuendelea kubaki mdarakani kwa kuyaweka mbele maslahi yao badala ya yale ya Taifa. Enyi wapinzani sikilizeni vilio na ushauri wa Watanzania ili muungane kabla ya uchaguzi wa 2010 kwani bado kuna muda wa kutosha kabisa kuweza kufanya hivyo.
Lakini wafu hawapigi kura. Hata kama majina yao yamo kwenye orodha ya wapiga kura.
Wapinzani hawatapata mafanikio yoyote katika chaguzi za Tanzania bila ya kuungana. Watanzania tumewapigia kelele juu ya umuhimu wa kuungana ili kuunda chama kimoja chenye nguvu. Hata Waziri Mkuu wa Kenya Odinga alipitembelea Tanzania ili wapate mafanikio ya kuing'oa CCM madarakani inabidi waungane, lakini wapi.
Kama wameshindwa huku Mbeya vijijini hakuna wa kulaumiwa bali ni wao wenyewe wapinzani. Hii danganya toto ya vyama vya upinzani 'vina ushirikiano' haitawafikisha kokote bila kuvunja vyama vilivyopo na kuunda chama kimoja chenye nguvu.
2010 inakaribia na dalili si nzuri maana bado kuna mgawanyiko mkubwa miongoni mwa Wapinzani. CCM haistahili kuendelea kuwa madarakani kutokana na matatizo mbali mbali yakiwemo ya mafisadi, lakini Wapinzani kwa kutotaka kuungana wanaisadia sana CCM kuendelea kubaki mdarakani kwa kuyaweka mbele maslahi yao badala ya yale ya Taifa. Enyi wapinzani sikilizeni vilio na ushauri wa Watanzania ili muungane kabla ya uchaguzi wa 2010 kwani bado kuna muda wa kutosha kabisa kuweza kufanya hivyo.
Kuungana hapa sio kwamba CHADEMA, NCCR, CUF, CHAUSTA, SAU, UDP nk waungane wawe na chama kimoja, hapo itakuwa ngumu, japo kama ingewezekana ingekuwa bora. Lakini muungano uwe kama Kenya wakati wa "Rainbow Coalition" ama juzujuzi "Pentagon", vyama vinakuwa chini ya mwamvuli mmoja wa makubaliano. Ina maana vyama vibaki kama vyama, lakini vikubaliane kuweka mgombea mmoja wa uRais na wabunge, madiwani nk. Ila kwa Tanzania ni wakati kuweka nguvu ya kuachiana majimbo ya ubunge na udiwani, wakiweza kupata madiwani na wabunge wengi haitakuja kushindikana kuachiana hata nafasi ya Rais.
Umoja ni muhimu, kama vyama vyote vikiamua kudai tume huru, hata kususia chaguzi, nina imani hiyo pressure na pia itakayopatikana toka kwa nchi wahisani tutapata tume huru. Wakati wa mjadala wa Zanziba (muafaka), vyama vingine viliomba kushiriki, kusema ukweli pale ndio ilikuwa wakati muafaka vyama vyote vingeshiriki na kuweka nguvu pamoja, kama ingepatikana tume huru Zanziba na mengineyo, basi ingebidi na Bara ifanyike hayo hayo kama ya Zanziba.
Mbona vyama vinaungana tu lakini haviiwezi CCM. Kwani hapa Mbeya Vijijini si vyama vya upinzani vya TLP, NCCR na PPT vyote viliungana kuisaidia CUF lakini vimeshindwa. Imagine vyama vinne vya upinzani vimeungana dhidi ya chama kimoja CCM na bado wameshindwa. Kwani ili muungano wa vyama uwepo ni mpaka CHADEMA nayo iwepo? CHADEMA haikuwepo kwenye muungano huo wa Mbeya Vijijini lakini muungano ulikuwepo na umeshindwa vibaya. CHADEMA ingefanya vizuri zaidi kuliko huo muungano, nakumbuka vyombo vya habari viliandika kuwa kule Tarime palikuwa na muungano wa TLP, CUF na NCCR dhidi ya CCM ambao ulielezwa kwamba ungetoa upinzani mkali. Lakini matokeo yake CHADEMA ndio ikashinda kwa uzembe wa kina Makamba. Huo muungano wa NCCR na wenzake na kile chama cha DP si walipata chini ya asilimia 5 za kura?
CCM imeushinda muungano wa vyama mbeya vijijini, tena hata kinara wa ushirikiano Mrema naye alikuwepo kumnadi mgombea wa CUF lakini bado wakashindwa.
........ndiyohiyo
CCM imeshinda uchaguzi wa Mbeya Vijijini. Kutokana na matokeo ambayo nimeyaona hapa kwenye kata mbalimbali mpaka sasa CCM inaongoza. Hata hivyo, idadi ya wapiga kura imekuwa ndogo sana. Katika kata za mjini kama utengule usongwe ambayo ina mji wa Mbalizi, wapiga kura waliojitokeza katika vituo vingi hawafiki hata asilimia 10. Wakati kwenye kata ya Ilembo waliojitokeza ni asilimia 15 tu ya wapiga kura wote. Kwenye kata nyingi zilizobaki wapiga kura waliojitokeza ni wastani wa asilimia 25, kati kata za Santilya, Iwiji, Iyunga Mapinduzi, Iwindi, Ikukwa nk. Mpaka ilipofika mchana hapakuwa na foleni za wapiga kura, watu wengi walikuwa makanisani, wengine majumbani na baadhi mashambani. Watu wengi walieleza dhamira ya kutokupiga kura kutokana na kampeni kupoteza mvuto baada ya mgombea wa CHADEMA kuenguliwa. Wananchi hao walikuwa wakielezea kwamba wanasubiri kupiga kura mwaka 2010 kukiwa na ushindani kati ya Shitambala na mgombea wa CCM. Nawapongeza timu yetu, hususani Mzee Malecela, kwani mbinu iliyotumika mchana ya kutuma mabalozi kwenye kila kaya kuhimiza watu kwenda kupiga kura ilifanya jioni ya kati ya saa 9 na 11 wapiga kura kujitokeza kiasi ambao kwa kweli wamechangia ushindi wa CCM. Nitawaletea matokeo kamili lakini katika vituo vingi CCM imeshinda kati ya asilimia 70 na 80 ya kura zilizopigwa. Nasubiri ya kata chache zilizobaki ili kupata matokeo kamili. Bado naendelea kujiuliza sababu ya watu kujitokeza chini ya asilimia 20 kupiga kura kama ni hiyo inayosemwa tu ya watu kususa baada ya CHADEMA kuondolewa au kuna sababu nyingine ya siri. CUF imeanza kulalamika kwamba imeshindwa kwa sababu ya hujuma za CCM na CHADEMA. Kwamba CCM imechukua kadi za kura kwa kubadilishana na mbolea na kwamba CHADEMA imechochea wananchi wasione umuhimu wa kupiga kura kwa kuwa wagombea wa CCM na CUF wameshirikiana kumwondoa mgombea aliyekuwa chaguo la wananchi wengi. Mrema naye ametoa lawama kwa CHADEMA kwamba ndio chanzo cha kuvurugika kwa uchaguzi huo.
.ndiyohiyo
TANU wakati ule wa kupata uhuru ilishinda bila KUUNGANA na chama kingine chochote. Naamini ule ndio ulikuwa uchaguzi HURU na wa HAKI wa MWISHO nchi hii. Chaguzi zilizofuata baada ya hapo ni MAIGIZO na VICHEKESHO vitupu hadi leo! Tatizo sio kuungana, tatizo ni jinsi tunavyoziendesha chaguzi hizi, wapiga kura wetu wengi vijijini ni MASIKINI sana, elimu ndogo sana ya URAIA, hatujapata bado KIONGOZI mwenye MVUTO na HAIBA, mwenye kipaji cha UONGOZI upande wa upinzani.
Kenya unadhani yalikuwa makundi mawili tu ya PNU na ODM kwenye uchaguzi wa urais, ubunge na udiwani? Yalishiriki mavyama kibao tu mengine kivyao vyao. Suala sio kuungana tu au kushirikiana. Mfano wa Kenya ni mfano mbovu sana kwa kuwa Kenya hakuna vyama kamali vya siasa, ni vikundi tu vinavyoongozwa na personalities za watu. ODM ilikuwa ni muunganiko wa personalities za watu hao unawaoita Pentagon. Ni kama leo CHADEMA iamue, kule Kigoma kuwe na Zitto, Kagera Baregu, Kilimanjaro Ndesambaro halafu imchukue Prof Lipumba Tabora ndio itengeneze pentagon ili kupata kura katika maeneo yao. Tanzania ni tofauti kidogo.
Kuhusu vyama kushirikiana mjadala wa muafaka hapa Zanzibar, haina maana yoyote kwa kuwa mjadala ulikuwa kati ya vyama vya CUF na CCM. Ingekuwa na maana kama mjadala ungekuwa kati ya CUF na Serikali iliyoiba kura na ambayo ndio iko madarakani.
Soma tena post yangu hapo juu, muungano au ushirikiano wa vyama ni kitu kinachoweza kuongeza nguvu ya kushinda lakini si njia pekee ya kushinda, na si lazima kwamba mkiungana tu mnashinda.
Nataka watu waondokane na huu utumwa wa kufikiri kwamba bila muungano wa vyama hakuna mabadiliko Tanzania
CCM imeshajua kuwa wananchi wanahuu utumwa ndio maana inapenyeza mamluki katika muungano wa vyama. Lakini pia kwa kujua hili, mtakumbuka pia CCM iliunda muungano wake wa vyama vidogo vya upinzani ulikokuwa na vyama vingi zaidi kuliko huu muungano wa vyama vinne, ulikuwa chini ya DP na SAU nao waliuzindua kwa kishindo ukawa unakabiliana na muungano wa vyama vya CHADEMA, TLP, CUF na NCCR. Kwa hiyo tukitegemea muungano tu, tutakatishwa tamaa na kujikatisha tamaa.
Asha
Utakufa nacho kijiba cha roho
Je, ni ukweli kama uamuzi wa Tume kumwondoa Shitambala baada ya kuwasilisha hii rufaa yake Mbeya vijijini: Kampeni, uchaguzi na yatokanayo - Page 40 - JamiiForums.com
umechangia kufanya watu wasusie kwenda kupiga kura?
.CHADEMA yashindwa vibaya
--------------------------------------------------------------------------------
Chama cha demokrasia na maendeleo kimeshindwa vibaya katika uchaguzi wa udiwani kati ya kati mjini Arusha.
Katika uchaguzi huo CCm ilipata ushindi mkubwa wa zaidi ya 68% uku CHADEMA ikiambulia 22%.CHADEMA ilitumia nguvu kubwa katika uchaguzi huo,mwenyekiti wa CHADEMA F Mbowe alitumia siku tatu za mwisho kumpigia debe mgombea wake Bwana Simba kitu ambacho kiliwashangaza wakazi wa jiji la Arusha hasa ikizingatiwa uchaguzi ulikuwa ni kata tu
Mama Asha,
Operesheni Sangara ifuatiwe na kuipanga upya safu ya VIONGOZI wenu WAKUU. Kuna watu mle wanaweza kuleta mabadiliko ya Uongozi wa Nchi hii.
Mama Asha,
Operesheni Sangara ifuatiwe na kuipanga upya safu ya VIONGOZI wenu WAKUU. Kuna watu mle wanaweza kuleta mabadiliko ya Uongozi wa Nchi hii.