Matokeo ya uchaguzi CCM Mwanza yaingia Dosari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matokeo ya uchaguzi CCM Mwanza yaingia Dosari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by WABHEJASANA, Oct 17, 2012.

 1. WABHEJASANA

  WABHEJASANA JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 4,225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Matokeo ya uchaguzi wa viongozi wa ccm Mkoani Mwanza yameingia dosari baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa huo Clement Mabina kukataa matokeo ya uchaguzi huo katika nafasi ya uenyekiti na kuahidi kukata rufaa kamati kuu.

  Mabina alitoa kauli hiyo jana majira ya saa 2 usiku muda mfupi baada ya matokeo hayo kutanagazwa wakati alipopewa nafsi ya kushukuru,ambapo Dk.Anthony Diallo alishinda kwa kupata kura 611 huku Mabina akipata 328.

  Miongoni mwa madai yake ya kupinga matokeo hayo ni matumizi mabaya ya fedha(Rushwa) ambapo amewatuhumu wagombea wenzake na hasa mshindi kwamba alitoa rushwa ndio maana amemshinda kwenye uchaguzi huo,dai lingine ni ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi ambapo anadai mshindi alizunguka na kufanya mikutano na wapigakura wakati kanuni za uchaguzi haziruhu.

  Hata hivyo Mabina alikumbana na kasheshe la kuzomewa na wapiga kura wakati akitoa madai hayo huku wengine wakimjibu kwa sauti kubwa zilizosikika,kwani wewe hukutoa mbona ulitoa,kafie mbali sisi kazi tumeshamaliza na viongozi wamepatikana.

  Mabina alijikuta akikosa uvumilivu na kuanza kushambuliana kwa maneno ya wapiga kura waliokuwa wakimzomea,lakini yeye akasisitiza kwamba rufaa ni haki yake na lazima afanye hivyo hata kama hatagombea.

  Habari kutoka kwa badhi ya wapambe wake wa karibu zimedai kuwa lengo lake anataka akate rufaa ili uchaguzi ufutwe na wote (yeye na mshindi) waondolewe kugombea nafasi hiyo wakose nafasi.
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ni lini rushwa haijatumika kwenye chaguzi za Magamba?
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,184
  Likes Received: 565
  Trophy Points: 280
  Kweli kazi imeisha washapokea chao na wameshaweka mfukoni sasa kelele za nini
  Halafu Taasisi ya kuendeleza na kurutuubisha rushwa wapo tuu wamekaa kimya mpaka watu wanaongea maneno haya
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  CCm bana ...rushwa hawawezi kuikwepa maana hata yule wa magogoni ndo balaaa yeye aliiba kura kabisa
   
 5. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Hiyo ndiyo CCM inayodai imamuenzi Julius Kambarage Nyerere Muasisi wa chama hicho. Ama kweli atukanaye hachagui tusi!
   
 6. WABHEJASANA

  WABHEJASANA JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 4,225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Haaaaaa!!!!!kamanda hebu nieleze vizuri unasema aliiba niniiii!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 7. WABHEJASANA

  WABHEJASANA JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 4,225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kamanda Zaleo,unadhani kwenye hili la kumuenzi Mwl.Nyerere kuna ambaye ataliweza,hata wale NCCR,CDM,C.U.F,SIJUI CCK hakuna hata mmoja ambaye analiweza,twende tu kuna siku inakuja ambayo tutafanya mapinduzi sisi wenyewe,hakuna kumtegemea mtu kila mmoja anatengenezea tumbo lake na familia yake.
   
 8. k

  kinai Senior Member

  #8
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 159
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na bado
   
 9. K

  KP ONE ONE New Member

  #9
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hatuna uchama umeshindwa kubali tukiwambia mhamie cdm mnakataa! Tukusaidieje sasa???????
   
 10. WABHEJASANA

  WABHEJASANA JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 4,225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wewe KP moja moja,mi bana sijakuelewa,unasema tuhamie wapi?,kwa ajili ya kazi gani?,kwani sisi hatuna makao yetu?,hebu fafanua bana Moja moja!!!
   
 11. M

  MTK JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  Mabina atulie tuli, kanyolewa bila maji, Hiyo ndio CCM yake, akubali yaishe hana ubavu wa kupambana na Diallo katika zama hizi za CCM ya wenyenacho, atulie amlilie Muasisi wa taifa maana zama zile za CCM kikiwa chama cha wakulima na wafanyakazi hata mnyonge alikuwa na nafasi angalau kidogo.
  Mabina fuata nyayo za Sumaye (Hanang) na Kusilla (Dodoma)
   
Loading...