Matokeo ya Law school of Tanzania, kati ya wanafunzi 500+ walio-clear masomo yote ni 22 tuu!

Ila mkuu kilicho kirahisi kwako kwa mwingine kigumu....

Huo mjadala ni wa enzi zile za secondary wanasema ooh PCM ngumu kushinda HKL lakini huyo mtu wa PCM ukimpa mtihani wa Kiswahili anataga....

Hakuna kitu kirahisi duniani kwa kila mmoja wetu...kila mtu ni kilaza kwenye kitu fulani ndo mana unavosema law ni course nyepesi hiyo ni kwako sio kwa wote hakunaga course nyepesi..
Uko too general..

Ndo mana katika law... kwenye evidence....expert evidence...kuna rule moja inasema kua
"An expert in field one is a layman in another field"...
 
Uko sawa, kuna philosphy katika education tulijifunza, kuwa :beauty is not a concept, but a beautiful thing is appreciated by many! Nakubali ugumu ni relative, but there are some concepts more difficult to understand compared to others! Albert Einstein alipokuwa anjaribu kuelezea how gravity comes about , ali introduce concept ya Warping of space and time (warping spacetime), ilikuwa shughuli kwa wanasayansi wenzake mabingwa kumwelewa.... it was a difficult concept to grasp compared to other concepts Einstein had proposed in the past!
 
Nimekupata asante sana kwa ushauri mzuri, ubarikiwe.
 
Lakini eventually walikuja kumuelewa...mtu akisema law ni course ngumu au nyepesi namkatalia...ila ni course ambayo inasomeka kama ukidhamiria ila kusema ni ngumu au nyepesi ni ishu ya mtu binafsi na ubongo wake..

Hao makondakta wa daladala wanajua kuhesabu hela vizuri na kurudisha kwa wakati tena under presssure na haraka unaweza kuzani wanajua hesabu sana...ila mulize 5×3 ni ngapi uone jibu lake...

Halafu wale waliosomea hesabu na uhasibu wao kazi muda wote kutumia calculator tu ukimpa ile kazi ya konda kurudisha chenji kwa wakati bila kutumia calculator unafikir wataweza??

Ugumu wa kitu au rahisi ni inategemea mtu na mtu
 
Nimekupata asante sana kwa ushauri mzuri, ubarikiwe.
Kwenye account namshauri...afanye kila awezalo ikifika siku ya pepa...ajue kuandaa income statement na balance sheet plus ajue zile accounting principles/concepts mana piga ua lazima yatoke hayo maswali...
Yani kwa ufupi kwenye accounting kama akiweza kupitia zile past papers zote mi nauhakika lile somo lazima achomoe..

Sema lile somo sasa kumbe nimeskia ili ufaulu lazima kila part usipate chini ya marks 25...yani part ya accounting usipate chini ya 25 kati ya 50 halafu ile.part ya leadershp HRM records managemnt nayo afanye asishuke chini ya 25 ila jumla iwe 50..

Mfano part moja akapata 35 nyingine tuseme 15 si inakua hamsini hapo?
Ujue hapo lazima supp tu hawezi kufaulu japo kapata 50....

Yale kiufupi pale yapo masomo mawili yanayojitegemea ndani ya kivuli cha somo moja so asije kusema kua mimi accounting siitaki nakomaa na part ya leadership pekee mradi nipate 50 hapo hataweza kuchomoa..
Lile somo watu wanafeli sana kwa kutokujua iyo trick kua yapo masomo mawili pale yanayojitegemea sasa mtu anakomaa na part moja anajua lazima apate 50 mwishowe anakua hajabalance anasupp....

Mkuu kususu conveyancing akomae na manual za sisti zipo steshenari lazima atatoka tu..
 
asante nimemweleza na kumtumia this advice
 
asante nimemweleza na kumtumia this advice

Poa mkuu pia ajaribu kuuliza wale walioko darasani kwa sasa hivi wamefundishwa nini na nn mana wao ndo wenye mtihani....
Mtihani unatungwa kulingana na walivofundishwa wao ...
So akipata tips kutoka kwao inasaidia mana anaweza kukomaa na madesa aliyesoma yeye wakati yupo class kumbe kuna vitu vimepunguzwa au kuongezwa...

So asione haya kuwauliza mana ukiuliza unapata Knowledge na Knowledge is always Power...
 
Law School Tanzania wapo vizuri tatizo ni aina ya wanafunzi wenyewe....Imagine muda ni mfupi sana lakin Wanafunzi eti wako busy nakula Bata Mara waandae Tour Bagamoyo Mara sijui welcome nini yani mambo ya kitoto kabisa ambayo tulipaswa kuyafanya first year vyuon na sio LST....kingine LST inajenga watu wawe na uelewa mpana na sio kuungaunga km vyuon yan watu wana GPA nzuri lakin after graduating wanashukuru Google kwa degree zao maana wengi wao degree ni zamagumashi....Laiti vyuo vikuu wangekua na mitazamo ya LST na CPA basi pale watu wangesoma na sio kuharibika maana statistics show vijana wengi wanaharibikia vyuon....By the way hao 22 wanatosha sana maana they know exactly what was LST is.....Ukifatila ata matokeo yao ya nyuma wengi wao wana F ya Mathematic japo haisiani na Sheria.....polen 23rd cohort kwa kuendekeza picnic za Bwagamoyo
 
nakataa, HKL ni rahisi kuliko PCM, ukimchukua mtu wa PCM ukimuhamishia HKL, akafundishwa kidogo tu, ataelewa fasta kutokana na uwezo wake kichwani ulivyo, ila ukimchukua wa HKL, ukamuhamishia PCM ata afundishwe vipi kutoboa ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu. Ndio maana unaona PCM inaweza beba choice zote mpaka za HKL ukiingia chuo, ila HKL haiwezi. sisi tulikua tunaiita HKL comb ya dada zetu Alevel
 
Inategemea umemchukua mtu wa aina gani...
Kama umemchukua mtu hana interest na PCM inakua ngumu so ishu sio ugumu ishu ni interest ya mtu....

Nakupa mfano wangu binafsi toka nasoma shule ya msingi mpaka naanza vidato my performance kwenye masomo ya sayansi hasa Chemistry na Physics was very impressive...sikuwahi kupata chini ya B ya Phy na Chem...

Ila binafsi hakuna masomo niliyokua siyapendi kusoma kama hayo....but nilikua nafaulu vizuri tena nakuambuka kua form 1 na 2 somo la kiswahili lilikua gumu kwangu mm kushinda Phy na Chem nilivoingia 3 ..somo la kiswahili likawa my co-favorite nikawa nachezea A ...too sad sikuja kulisoma nilivofika form 5

Ndo mana nakataa kua eti HKL ni ngumu kushinda PCM....
Mimi sikuona ugumu wowote wa Phy au Chem sema sipendi mambo ya sayansi mpaka leo.
Nafanya mambo kuridhisha nafsi yangu mana hatuishi milele nisipofurahi leo naweza nisipate nafasi ya kufurahi kesho..

So it's all about interest na kichwa cha mtu sio kila aliyesoma Arts alikimbia sayansi.
 
Kweli mkuu vijana siku izi ukiskiliza stori zao ni 'bata na instagram na mpira'

Kama juzi kati nilishangaa sana kuskia eti wanafunzi wa LST wanalalamika Rais aliyechaguliwa ni wa CCM sijui...
Nilishangaa sana nikasema hao wanakaa miezi 4 tu LST baada ya hapo umemaliza sasa huo muda wa kwenda instagram kusema sijui Rais wa CHadema sijui CCM wanaupata wapi....

Sisi cohort yetu nakumbuka walitaka kufanya uchaguzi wa viongozi mpaka wakachoka kusubiri mana hakuna aliyejitokeza kugombea hamna aliyekua interested, ikabidi baadhi ya wale viherehere wa darasa (always darasa linakuaga na viherehere) wajitolee kuokoa jahazi kulikua hakuna mambo ya siasa wala kampeni....

Ama kweli zama zimebadilika sio kila homa ni malaria!
 
Elimu ya Tanzania imejengewe fikra kwamba wanapofaulu wachache ndio ubora wa elimu.

Hii ni dhana ya kizamani ya kishamba na ulimbukeni wa elimu.
Elimu itolewe kwa kiwango sahihi na watu wafaulu kwa kiwango sahihi bila ubabaishaji na vikwazo.

Nimependa sana comment hizi
, ni lazima tuwe na fikra chanya kuhusu elimu ya nchi yetu, tuache ulimbukeni na ushamba wa kijinga kwamba wanaofeli hawasomi. Ulishayasikia madudu haya huko kwenye Law Bars za wenzetu? Google hapo Ontario bar, Harvard bar, Northwestern law bar, Toronto n.k. . . .
 
Nimeenda na nimefaulu first sitting lakini kazi ilikuwa ya mapambano makali sio lelemama, viwango vya law school ni vya juu sana mtu mwepesimwepesi kuviweza ni ngumu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…