MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

TUMESHUHUDIA MATOKEO DUNI YA MITIHANI YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2010 YALIYOTANGAZWA MWEZI ULIOPITA. NI 11.5% TU NDIO WANAWEZA JIUNGA NA VYUO NA KIDATO CHA TANO. WENGINE ITAKUWAJE? NI KOSA LA NANI?
JAMII IMEKUWA NA MASWALI MENGI KULIKO MAJIBU KUHUSU MSTAKABALI WA ELIMU YA WATOTO WETU NA HADHI YAKE.
KAMA VILE HAITOSHI NA VYUO VYETU VIKUU VIMEPATA PIGO HILO. WAALIMU WENGI WAMEKIMBILIA SIASA NA NYADHIFA MBALIMBALI NA KULEGALEGA KITAALUMA. CHUO KIKUU CHA DAR-ESALAAM KILIKUWA CHUO BORA AFRICA MASHARIKI NA CHUO NAMBA 10 KATIKA VYUO 200 BORA AFRICA. LAKINI KWA SASA(2011) CHUO KIKUU CHA DSM KIMESHUKA HADI NAFASI YA 12 NA KUPITWA NA NAIROBI UNIVERSITY. SUA IMESHUKA KUTOKA NAFASI YA 30 HADI YA 90.
WATANZANIA TUFANYE MAAMUZI MAGUMU SASA. TUTATAWALIWA KILA CORNER.

SOURCE: 2011 World University Ranking | Top 100 Universities in Africa
 
wizara ya elimu ina shule zake za O-level mpaka High Schoo. Shule za kata ziko chini ya Tamisemi ambayo haina High school. Baraza la mitihani ni la wizara ya elimu......???????????? ulitaka wale wa kata waonekane wamefaulu ili ionekane hata tamisemi na shule zake wanafanya vyema?

- jiulize dar kule o level school ngapi na high school ngapi. Wangefaulu wengi hizo high school zilizoko upanga (jangwani, tambaza, azania, zanaki) zingetosha?
 
Kushindwa vibaya kwa wanafunzi hasa wa shule za serikali si tu kwa sababu ya miundombinu mibovu kama uhaba wa walimu, ukosefu wa vitabu, maabara n.k bali hata baadhi ya walimu wanachangia watoto kufeli. Just imagine mtoto yatima anaishi na mama tu naye ni mlemavu anapata msaada wa kulipiwa school fees, anapewa sare ya shule, madafutari na kalamu vya kutosha. Lakini mwalimu anamfukuza wiki tatu sasa eti akafuate mchango wa dawati na mock wakati wenzake wanaendelea na masomo. Madawati yapo darasani hayana wanafunzi wa kuyakalia kwani wamefukuziwa michango. Je huyu anafaa kuitwa mwalimu?
 
Katika tamko la waislam walidai 50-50, kwa matokeo haya ya f4, katika 10 bora hakuna hata mwislamu mmoja, itawezekana?
 
Itawezekana. Mbona Uru Seminari wamekuwa wa kwanza kitaifa kama shule na hakuna mwanafunzi aliyekuwa wa kwanza? Wajipe moyo watafika.
 
50-50 itafikiwa tu pale mashekh watakapoa acha siasa na kufuata muongozo wa dini yao na kuhimiza watoto kwenda shule na kuzingatia elimu, sio kucheza kiduku na taarabu
 
Marks sio ishu mkubwa. Kama huamini 'unda' tume uchunguze vigezo vilivyotumika na TCU kuwapa wanafunzi chance za university mwaka huu...
 
Umenishutua tafadhali unaweza kufafanua maana ya sentensi yako? kwa sababu nimesikia mtu anasema hata waliochagualiwa darasa la saba kwenda sekondari mwaka huu kuna maeneo ambayo kigezo kimojawapo ilikuwa ni kuangalia majina na kugawa nusu kwa nusu

Marks sio ishu mkubwa. Kama huamini 'unda' tume uchunguze vigezo vilivyotumika na TCU kuwapa wanafunzi chance za university mwaka huu...
 
Nimeamua kupost thread hii kwa makusudi,kwanza ni kawaida kabisa na ni suala la wazi kwamba mbunge anapopata uwaziri,anafanya kila awezalo kunufaisha kwao jambo ambalo ni zuri na ni baya kwa upande mwingine.Mtu anapokuwa waziri anatakiwa kuwa a national leader na si vinginevyo.Mwandosya amejitahidi sana kupendelea kwao,na shule hiyo ina nafuu kwa majengo,walimu,vitabu na mengineyo kuliko shule nyingine za kata huko Rungwe Mashariki.NI MUHIMU SANA TUKATHAMINI MUUNDO WA ELIMU YETU KWA PAMOJA KAMA TAIFA

Ulitaka apendelee kwao hadi matokeo? Tuache unafiki waziri huyu hahusiki na matokeo hayo ila hao walimu na mfumo mzima wa elimu Tanzania. Mbona shule kibao tu zenye majina ya wakubwa huwa hazifanyi vizuri leo hii unamkomalia Mwandosya? Angeacha kuisapoti mngechooonga sa kasaidia bado tena mwamsarandia...acha hizo huo ni mfumo wa elimu na mitoto yenu ya siku hizi.
 
Madai hayana msingi. Wapeleke watoto shule na wawahimize kusoma kwa bidii. Hakuna njia ya mkato kwenye mafanikio.
 
Wakuu tuache kuleta hoja zisizokuwa na tija kwetu sote. Hili swala la mitihani ya form four has nothing to do with Islam or Christianity or paganism. Ni swala la vijana kuweka bidii. Sasa tunafika mahala haya maswali ya dini yanaanza kubore sasa..na anayeyaongelea anaonekana kichwa cha mwendawazimu.......Nani aliwaambia kwamba kuna affirmative actions kwenye mitihani? Swala ni kuweka bidii tuu. Wazazi na watoto washirikiane katika kuongeza ufanisi wa watoto mashuleni. Tuache hizi cheap politics za dini. Huwezi kuwa daktari kama hujafaulu mtihani wa udaktari..hata kama ungepewa nafasi ya bure kwenda Muhimbili. Utafeli tuu. Tusaidiane vijana wetu wasome.
 
Matokeo ya kidato cha nne 2010 yanatishia hatima ya nchi yetu,na tusipobadilika na kuona umuhimu wa elimu bora katika zama hizi za ubepari,basi kama taifa tumekwisha.
Hebu angalia matokeo ya Shule ya Sekondari Lufyilo ambayo ipo katika wilaya ya Rungwe,Lufilyo ndio nyumbani kabisa kwa Prof:Mark Mwandosya,waziri wa maji.

Summary ya matokeo ni kama ifuatavyo;

DIV-1=0
DIV-2=0
DIV-3=2
DIV-4-47
FLD- 73

Hizi ni symptoms of extremely serious problems, ambazo sidhani kama root causes zake tunazifahamu by the looks of it. Tunaishia kulalama tu,hii haitatusaidia sana,we need to take action now.
 
Kwa jinsi mambo yanavyoenda kuna uwezekano mkubwa kukatokea maandamano kwa waliofeli maana ndg zetu wa Pasu kwa pasu wameshaibuka na hoja za kuwa watu flani wanapendelewa, zaidi ya hapo mwanasiasa Mbatia wa NCCR-Mageuzi akadai usahihishaji urudiwe! sasa kuna hili la leo Tanzania Association of Managers nad Owners of Non -Government Schools and Colleges nao wanadai matokeo yafutwe na mtihani urudiwe (MICHUZI: chama cha shule na vyuo binafsi chataka matokeo ya mtihani wa fom foo yafutwe, usahihiswhe upya)! Hii kali...yaani hawa nao ni nani? wanatambulika kisheria? hawa si ndo wale wenye shule uchwara wanaziita academy aka international schools nyingine hata hazijasajiliwa? leo hii wana sauti kama nani? scholars au nani? Hii political mobilization ya watu kwenye mambo yasiyo na tija kwa ustawi wa taifa namna hii unatoka wapi? Hivi tunajua neno "standards"? Kwa jinsi ninavyoona kuna uwezekano wa matokeo ya mwaka kesho yakachakachuliwa ili kuridhisha umati maana siasa sasa inaingizwa kila mahali!

Hivi utaratibu wa kurudia mtihani ukifeli kama private candidate, umeondolewa nini?
Kweli tuna umbwe la uongozi! Tutaona mengi mpaka 2015!


 
Katika tamko la waislam walidai 50-50, kwa matokeo haya ya f4, katika 10 bora hakuna hata mwislamu mmoja, itawezekana?

Tz siyoyawakirist&waisiram kumbuka kuna dini zingine nakunawenine hawana dini unawaweka wap? tutowehoja zakujenga
 
N ile kusoma madrassa inapotezea sana muda watoto badala ya kwenda tuition wakitoka shule wao wanawapeleka madrassa! bora hata ingekuwa mara moja kwa week. yaani kila siku wapo madrass
 
Suala linaloongelewa hapo ni la Msingi sana. Hasitokee yeyote kukatisha mjadala huu! Matokeo ya mitihani ndo mchujo wa kuwapata viongozi wa baadae. Kama watu wa dini nyingine au wa kabila yoyote hile hawajalitambua hilo msistizo wao wa kuliongoza Taifa hili hautakuwa na msingi wowote. By the way if you have ten wives and twenty children how do give basic needs for your family including education! Some time the goverment opverlooks important issues like this alafu wanatuchonisha baadae. I hate our goverment plans and overlooking issues like family planning...
 
Back
Top Bottom