Jimbo la Bumbuli matokeo ya Ubunge yanaonesha kuwa waliopiga kura ni watu 20,512 ambapo January Makamba amepata kura 17,805. Lakini cha ajabu kwenye matokeo ya Urais jimbo hilohilo la Bumbuli waliopiga kura ni watu 44,011 ambapo Magufuli anadaiwa kupata kura 35,801.
Sasa jiulize imekuaje waliopiga kura za mbunge wawe watu 20,512 halafu kura za Rais wawe 44,011. Yani kuna watu 24,000 walienda vituoni kupiga kura za Rais tu lakini hawakupiga za Mbunge.
Haya ni maajabu ya dunia. Haihitaji degree kujua kwamba Tume imeongeza wapiga kura hewa 24,000 na kura zote hizo wakampa Magufuli.
Unyumbu ulipaswa uuache baada ya kampeni, sasa ni kazi tu!
Muombe Mbowe au Lowasa wakutumie scanned copy waliyopokea toka Bumbuli huiambatanishe na hiyo ya tume, kisha tuanze mjadala! Vinginevyo hizo ni fununu tu na hatuwezi kupoteza muda kuzungumzia hisia za watu!
Mlikuwa mnajitekenya na vijitafiti vyenu vya uzushi na mnakataa utafiti wenye tija wa TWAWEZA na synovate mlidhani huu ni wakati wa propaganda!