Matokeo ya Jimbo la Bumbuli yana Utata

Matokeo ya Jimbo la Bumbuli yana Utata

Status
Not open for further replies.
Hii haina ukweli wowote ni uzushi tu. Jimbo la Bumbuli katika Ubunge zimepigwa kura 44,011 na kati ya hizo kura 167 zimeharibika kwa hiyo kura halali ni 43,844. Kati ya hizo January Makamba amepata kura 36,887 na David Changeghea (CHADEMA) kapata kura 6,957.

Kura 20,512 ambazo unaziongelea ni kura zilizopigwa wakati wa Kura za Maoni za Chama cha Mapinduzi kuteua Mgombea wa Ubunge wa jimbo la Bumbuli.

Watanzania tuepushane na uzushi usio na msingi ambao unaweza leta machafuko. Naambatanisha matokeo hayo ya Urais, Ubunge na Kura za maoni BUMBULI.
attachment.php
attachment.php
attachment.php
 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1446026868.531595.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1446026868.531595.jpg
    31.8 KB · Views: 275
  • ImageUploadedByJamiiForums1446026911.407177.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1446026911.407177.jpg
    38.8 KB · Views: 241
  • ImageUploadedByJamiiForums1446026936.743361.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1446026936.743361.jpg
    23.3 KB · Views: 270
Am sick and tired,I hate my country!

Inauma sana nifah binafsi namuomba Mungu nisije nikamkufuru maana sometime mawazo yananijia kama Mungu ni Mungu wa haki na anapenda viumbe wake why anaacha haki za watu zinalawitiwa kiasi hiki yaani mafisiem wanafanya chochote watakacho. Mimi hupenda haki daima even if Magufuli angekuwa anaongoza kwa haki wala nisingemaind at all
 
Weka ushahidi wa copy za NEC una nyuzi humu zimebandikwa zote.

Kwanini unaandikia mate na wino upo?
 
Hivi lowassa ana msaada gani mpaka sasa kupambana na ccm kwenye wizi wa kura? Amekuja cdm anajua fika ccm wanahuo mchezo, sasa yeye analalamika na sisi tulalamike kwa nani?
 
mimi naomba ulete nyaraka za uthibitisho zote zilizotangazwa za ubunge na urais.......tusiwe tunaongea tu bila uthibitisho halisi wakati upo
 
ivi kama unataka kupata viza inakuwaje jamani kwani huu ndo ulofa wenyewe unaibiwa unachekacheka afu mtu anakwambia tumewaamini tume sio nchi ya kuishi hii kila kibaya kinapatikana humu ebu ona uchawi tz makanisa mengi feki tz, wasio na ajila wengi tz,kwenye michezo atupo kabisa, ujinga ndo usiseme wajinga wengi sana cha mwisho watanzania wengi tunaandamana kwenye mitandao ya kijamii sio live na uku nako walisha kuja na sheria kukuziba mdomu kinacho baki nini hapo
 
MATOKEO YA NEC YANA KASORO NYINGI.!

Jana nilisema nitatoa screnario tano kudhibitisha kuwa matokeo yanayoendelea kutangazwa na Tume si ya kweli na yanafaa kupuuzwa na kila mtu mwenye akili timamu. Licha ya Tume ya uchaguzi kutokua huru lakini imeamua kushirikiana na CCM kupuuza maoni ya watanzania na kuhujumu matokeo ya uchaguzi.

Scenario zifuatazo zinathibitisha hivyo;

1. Jimbo la Tunduma karatasi iliyobandikwa ktk ofisi ya Msimamizi wa uchaguzi ikiwa na muhuri wa Tume inaonesha Lowassa amepata kura 32,219. Lakini matokeo yaliyotangazwa na Tume yanaonesha Lowassa amepata kura 6,000 tu. This means NEC hawatangazi matokeo wanayopokea kutoka kwny majimbo bali wanatangaza matokeo yao kama wanavyoelekezwa na CCM.

2. Jimbo la Bumbuli matokeo ya Ubunge yanaonesha kuwa waliopiga kura ni watu 20,512 ambapo January Makamba amepata kura 17,805. Lakini cha ajabu kwenye matokeo ya Urais jimbo hilohilo la Bumbuli waliopiga kura ni watu 44,011 ambapo Magufuli anadaiwa kupata kura 35,801.

Sasa jiulize imekuaje waliopiga kura za mbunge wawe watu 20,512 halafu kura za Rais wawe 44,011. Yani kuna watu 24,000 walienda vituoni kupiga kura za Rais tu lakini hawakupiga za Mbunge. Haya ni maajabu ya dunia. Haihitaji degree kujua kwamba Tume imeongeza wapiga kura hewa 24,000 na kura zote hizo wakampa Magufuli.

Niliwahi kusema "CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu". Kiazi kama January ndo anapewa kazi ya kuiba kura za Lowassa unategemea nini? Haiwezekani watu 24,000 waende kituoni kumpigia kura Rais tu halafu wasipige za Mbunge. Utaratibu ulikua watu kupiga kura 3. Sasa iweje waliopiga kura za Urais Bumbuli wawe wengi kuliko waliopiga za Mbunge? Yani mtu alienda kituoni akapewa karatasi ya Rais tu, alipopiga akaondoka bila kupiga ya Mbunge?.

3. Majimbo mengi asilimia za kura zimeonekana kuzidi 100 jambo ambalo linadhihirisha wizi wa waziwazi. Jimbo la Monduli Arusha Lowassa anatajwa kupata kura 49,675 na Magufuli kura 11,335 lakini wote wametajwa kuwa na asilimia zinazolingana (18%).

Jimbo la Arusha Mjini Lowassa anatajwa kupata kura 150,107 na Mgombea wa Chauma amepata kura 551 lakini wote wametajwa kuwa na asilimia zinazolingana (69%). Yani Lowassa amelingana na Hashim Rungwe jimbo la Arusha mjini.

Jimbo la Ndanda ukijumlisha asilimia za wagombea zinakuja 108%. Jimbo la Arusha mjini zinakuja asilimia 182% na majimbo mengine hivyo hivyo. This means waliopewa kazi ya kuiba kura walikosa umakini. CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu.

4. Baadhi ya majimbo idadi ya kura zilizopigwa imezidi idadi ya wapiga kura. Kwa mfano ukijumlisha matokeo ya Jimbo la Makunduchi Zanzibar kwa wagombea wote utapata kura 10,382. Lakini idadi ya kura halali ni 10,352. Yani kura zilikua nyingi kuliko idadi ya wapiga kura. Sasa sijui kama kuna watu walipiga kura mara mbili au vp. CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu.

Hali hiyo pia imejitokeza katika jimbo la Kilindi, jimbo la Bumbuli na majimbo mengine. Hii inapaswa kuingia kwenye kitabu cha records za dunia (Guiness) maana ni maajabu kupata kura nyingi kuzidi idadi ya wapiga kura.

Mwaka 1927 aliyekua Rais wa Liberia Charless King aliingia kwny kitabu cha Guiness baada ya Tume ya uchaguzi nchini humo kumtangaza kuwa ameshinda kwa kura 234,000 wakati idadi ya wapiga kura nchini kwake ilikua 15,000 tu. NEC nao wamefuata nyayo za Charless King. Wanapenda namba lakini hawajui hesabu.

5. Kwa mujibu wa NEC jimbo la Bumbuli na Bukoba mjini ndio majimbo yenye watu smart kuliko majimbo yote Tanzania maana ndio majimbo pekee ambalo hakuna hata kura moja iliyoharibika.

Kwa mfano Bumbuli Idadi ya wapiga kura ni watu 44,011 na idadi ya kura halali ni 44,011. Haya ni maajabu mengine ya dunia. Yani ktk watu 40,000 hakuna hata mmoja aliyekosea. These people are very smart.

Ni ajabu jimbo la Makunduchi Zbar lenye wapiga kura 10,000 walioharibu kura ni watu zaidi ya 100 lakini jimbo la Bumbuli lenye wapiga kura zaidi ya 40,000 hakuna hata mmoja aliyeharibu kura. Kama unaelewa Probability utajua huu ni uongo wa kiwango cha PhD. Watu 44,000 are more likely kuharibu kura nyingi kuliko watu 10,000. KaJanuary hakajui hii formular coz kanapenda namba tu lakini hakajui hesabu. Itz shame.

NINI CHANZO CHA YOTE HAYA?

Sababu inayopelekea fraud hii ya kijinga ktk kutangazwa matokeo inasababishwa na Tume kuacha kutangaza matokeo halisi na kuamua kutangaza matokeo wanayopewa na CCM.

Kuna kikosi kazi cha vijana wa CCM wanaofanya tallying na kuwatumia Tume ya Uchaguzi. Kwa hiyo matokeo yanayotoka majimboni hayaendi moja kwa moja Tume, yanapita kwanza kwa vijana wa CCM wanayachezea ndipo yanaenda Tume. Katika kufanya kazi hiyo wanakosa umakini na kukosea hata vitu vidogo kama niliorodhesha hapo.

Licha ya kubadilisha matokeo ya Urais, mbinu nyingine wanaofanya ni kupunguza kura za Lowassa kwa kuongeza kwenye idadi ya kura zilizoharibika. Katika majimbo mengi Lowassa aliyoongoza hata idadi ya kura zilizoharibika ni nyingi.

Hebu jiulize imekuaje jimbo la Arusha mjini watu zaidi ya 5000 waharibu kura? Watu 5000 ni sawa na wakazi wote wa jimbo la Wawi Zanzibar. So ni sawa na kusema jimbo lote la Wawi wameharibu kura. Impossible.!

Mbinu nyingine ni kupunguza kura za Lowassa na kuwaongezea wagombea wa vyama vidogo. Kwa mfano jimbo la Moshi mjini mgombea wa ADC alipata kuta 11 jimbo zima. Na fomu ya matokeo iliyobandikwa ofisi ya Mkurugenzi inaonesha hivyo. Lakini kwenye matokeo yaliyotangazwa na Tume inaonekana amepata kura 186. Ongezeko la kura 175. Ujinga huu wameufanya ktk majimbo mengi.

WAY FOWARD.

Sisi tumefanya tallying ya majimbo yote ya nchi nzima na tunayo matokeo halisi kama yalivyosainiwa na mawakala wa vyama vyote. Matokeo hayo yanaonesha maoni halisi ya watanzania.

Viongozi wa chama wanakutana leo na muda si mrefu watatoa tamko. Rais wa Tanzania anachaguliwa na Watanzana, ni vizuri kuheshimu maamuzi yao.!
 
Hadi hapo sie tunawaamini tume!!!!!! ndio tuliowapa dhamana.......huna ushaidi mzushi tu wewe

Unataka ushahidi gani zaidi ya huo? Yaani nyie ccm mmh ni virusi kabisa asee
 
Inauma sana nifah binafsi namuomba Mungu nisije nikamkufuru maana sometime mawazo yananijia kama Mungu ni Mungu wa haki na anapenda viumbe wake why anaacha haki za watu zinalawitiwa kiasi hiki yaani mafisiem wanafanya chochote watakacho. Mimi hupenda haki daima even if Magufuli angekuwa anaongoza kwa haki wala nisingemaind at all

Acheni kumtaja Mungu kwenye huu upuuzi wenu.

Yaani mnalalamikia vitu ambavyo havipo.

Msipende kubeba uzushi bila kufuatilia.
 
Nilishasema huko nyuma na narudia tena CCM haiwezi kuondoka kwa sanduku la kura, ni lazima watoke kwa nguvu, watanzania tuache ujinga na kujidanganya, kama kweli tunataka ukombozi wa kweli kwa nchi hii ni lazima tupigane na damu imwagike. Hakuna haki inayopatikana hivi hivi tu. Huu ndio ukweli na utabakia kuwa hivyo kama hilo hatuliwezi tukae kimya tu CCM itawale milele na umasikini utumalize mpaka kizazi cha tatu kutoka sasa.
 
Hivi lowassa ana msaada gani mpaka sasa kupambana na ccm kwenye wizi wa kura? Amekuja cdm anajua fika ccm wanahuo mchezo, sasa yeye analalamika na sisi tulalamike kwa nani?
Sikuzote wanachakachua safari hii kwakuwa wale waliokuwa jikoni wamekihama chama na wametoa siri za uchakachuaji ndiyo maana mambo yamekuwa wazi.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom