Matokeo ya Jimbo la Bumbuli yana Utata

Matokeo ya Jimbo la Bumbuli yana Utata

Status
Not open for further replies.
Hii haina ukweli wowote ni uzushi tu. Jimbo la Bumbuli katika Ubunge zimepigwa kura 44,011 na kati ya hizo kura 167 zimeharibika kwa hiyo kura halali ni 43,844. Kati ya hizo January Makamba amepata kura 36,887 na David Changeghea (CHADEMA) kapata kura 6,957.

Kura 20,512 ambazo unaziongelea ni kura zilizopigwa wakati wa Kura za Maoni za Chama cha Mapinduzi kuteua Mgombea wa Ubunge wa jimbo la Bumbuli.

Watanzania tuepushane na uzushi usio na msingi ambao unaweza leta machafuko. Naambatanisha matokeo hayo ya Urais, Ubunge na Kura za maoni BUMBULI. View attachment 303258View attachment 303259View attachment 303260

Hivi cyber crimes haiwahusu hawa wanaozusha bila vielelezo?
 
Kabisa mkuu. Historia duniani kote ipo wazi kuwa kuwaondoa watawala dhalimu ni lazima kinuke. Lakini kwa hizi keyboard, sidhani! Yaani kutokana na upole wetu, ccm sasa wala hawaiibi tena bali inapora ushindi kweupe huku tunaona, nasi tunasema, hewala baba ccm!?

Kabisa watu wanalalamika kwenye key board tu,
 
Ushahidi kama uo pelekeni kwenye vyombo vya habari, wachunguzi wa now na balozi sio JF peke yake haisaidii wakuu
 
Jimbo la Bumbuli matokeo ya Ubunge yanaonesha kuwa waliopiga kura ni watu 20,512 ambapo January Makamba amepata kura 17,805. Lakini cha ajabu kwenye matokeo ya Urais jimbo hilohilo la Bumbuli waliopiga kura ni watu 44,011 ambapo Magufuli anadaiwa kupata kura 35,801.

Sasa jiulize imekuaje waliopiga kura za mbunge wawe watu 20,512 halafu kura za Rais wawe 44,011. Yani kuna watu 24,000 walienda vituoni kupiga kura za Rais tu lakini hawakupiga za Mbunge.

Haya ni maajabu ya dunia. Haihitaji degree kujua kwamba Tume imeongeza wapiga kura hewa 24,000 na kura zote hizo wakampa Magufuli.

Mheshimiwa UKAWA ilianzishwa ili kutetea ile katiba ya Tume ya Warioba, ambayo ilikuwa na kipengele kinachoruhusu matokeo ya urais kuhojiwa mahakamani. EL kwa kudhani angepitishwa na CCM akafadhili hujuma dhidi ya katiba pendekezwa, ikadoda hadi leo. Leo yuleyule mamba aliyemfuga mwenyewe anamtafuna, wacha amtafune!
Kisa hiki (real story) kinatufundisha kuwa katiba ya wananchi ni ya wote. Kama uko chama tawala leo, kesho utakuwa upinzani. Mwenzetu huyo keshatafunwa na mamba, tuliobaki tujifunze kuwa jambo la maslahi ya taifa tunapaswa kulipigania sote, bila kujali tuko chama gani linapotokea suala hilo. Leo tunashindwa kuhoji haya mambo mahakamani kisheria kwa sababu katiba inakataza, ileile EL na wenzie waliyoitetea. Tumeona elimu ni ghali, tumejaribu ujinga tumeona matokeo yake, sasa tunahitaji matibabu.
 
Hadi hapo sie tunawaamini tume!!!!!! ndio tuliowapa dhamana.......huna ushaidi mzushi tu wewe

Hizo Namba huzioni wewe kalumekenge ? Namba hazidanganyi Na huhitaji kuamini NEC Kama Namba zinaonyesha TOFAUTI. Hata kuiba kwa akili limewashinda😡
 
hizo namba huzioni wewe kalumekenge ? Namba hazidanganyi na huhitaji kuamini nec kama namba zinaonyesha tofauti. Hata kuiba kwa akili limewashinda

jpm ndio keshakuwa rais wa jmt!!! Nuna basi??
 
Jimbo la Bumbuli matokeo ya Ubunge yanaonesha kuwa waliopiga kura ni watu 20,512 ambapo January Makamba amepata kura 17,805. Lakini cha ajabu kwenye matokeo ya Urais jimbo hilohilo la Bumbuli waliopiga kura ni watu 44,011 ambapo Magufuli anadaiwa kupata kura 35,801.

Sasa jiulize imekuaje waliopiga kura za mbunge wawe watu 20,512 halafu kura za Rais wawe 44,011. Yani kuna watu 24,000 walienda vituoni kupiga kura za Rais tu lakini hawakupiga za Mbunge.

Haya ni maajabu ya dunia. Haihitaji degree kujua kwamba Tume imeongeza wapiga kura hewa 24,000 na kura zote hizo wakampa Magufuli.

Unaeneza uongo kwa faida ya nani?
 
Am sick and tired,I hate my country!

I know it is difficult. But I urge you to try to check the veracity of most of the information which is floated in this forum. For example, the initiator of this thread is spreading a lie.
 
Hii haina ukweli wowote ni uzushi tu. Jimbo la Bumbuli katika Ubunge zimepigwa kura 44,011 na kati ya hizo kura 167 zimeharibika kwa hiyo kura halali ni 43,844. Kati ya hizo January Makamba amepata kura 36,887 na David Changeghea (CHADEMA) kapata kura 6,957.

Kura 20,512 ambazo unaziongelea ni kura zilizopigwa wakati wa Kura za Maoni za Chama cha Mapinduzi kuteua Mgombea wa Ubunge wa jimbo la Bumbuli.

Watanzania tuepushane na uzushi usio na msingi ambao unaweza leta machafuko. Naambatanisha matokeo hayo ya Urais, Ubunge na Kura za maoni BUMBULI. View attachment 303258View attachment 303259View attachment 303260

Sasa huyu anayejiita "Delegate" ni kwamba aliamua makusudi kupotosha ukweli au hakuelewa? Huu uzi alioanzisha unatosha kabisa kuwafanya watu wachukue silaha kuwaadhibu tume ya uchaguzi kwa kutoa matokeo ya kugushi. JF itamchukulia hatua gani mpotoshaji kama huyu bila kujali kafanya kwa makusudi au hakuelewa? Pili uzi kama huu unadhihirisha umakini wa Tume ya Uchaguzi yaani wakosoaji wamakosa lolote lililofanyika kimakosa inabidi makosa ya uongo yatungwe kuonye udhaifu ambao tume haina.
 
Poleni sana Bumbuli hampajui tu tuulizeni tunaotoka huko Bumbuli ni CCM miaka mia maendeleo yaliyopo huku ni shidaahhh...hadi imekuwa halmashauri
 
Mbona wameondoa kitufe cha LIKE? Pokea LIKE yangu Mkuu. Wanadhani wanadanganya watu, lakini mwisho wa siku serikali ya ccm itakosa uhalali wa kutawala kwa sababu hawakuingia madarakani kwa njia sahihi. Matokeo yangu ni serikali kudhoofika na mwisho wa siku kushindwa kuendelea kufanya kazi. Historia haidanganyi!

daah asee kweli mana nilikua nakitafta kumbe na wewe hukioni kitufe cha like

noma sana Fisiem
 
MATOKEO YA NEC YANA KASORO NYINGI.!

Jana nilisema nitatoa screnario tano kudhibitisha kuwa matokeo yanayoendelea kutangazwa na Tume si ya kweli na yanafaa kupuuzwa na kila mtu mwenye akili timamu. Licha ya Tume ya uchaguzi kutokua huru lakini imeamua kushirikiana na CCM kupuuza maoni ya watanzania na kuhujumu matokeo ya uchaguzi.

Scenario zifuatazo zinathibitisha hivyo;

1. Jimbo la Tunduma karatasi iliyobandikwa ktk ofisi ya Msimamizi wa uchaguzi ikiwa na muhuri wa Tume inaonesha Lowassa amepata kura 32,219. Lakini matokeo yaliyotangazwa na Tume yanaonesha Lowassa amepata kura 6,000 tu. This means NEC hawatangazi matokeo wanayopokea kutoka kwny majimbo bali wanatangaza matokeo yao kama wanavyoelekezwa na CCM.

2. Jimbo la Bumbuli matokeo ya Ubunge yanaonesha kuwa waliopiga kura ni watu 20,512 ambapo January Makamba amepata kura 17,805. Lakini cha ajabu kwenye matokeo ya Urais jimbo hilohilo la Bumbuli waliopiga kura ni watu 44,011 ambapo Magufuli anadaiwa kupata kura 35,801.

Sasa jiulize imekuaje waliopiga kura za mbunge wawe watu 20,512 halafu kura za Rais wawe 44,011. Yani kuna watu 24,000 walienda vituoni kupiga kura za Rais tu lakini hawakupiga za Mbunge. Haya ni maajabu ya dunia. Haihitaji degree kujua kwamba Tume imeongeza wapiga kura hewa 24,000 na kura zote hizo wakampa Magufuli.

Niliwahi kusema "CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu". Kiazi kama January ndo anapewa kazi ya kuiba kura za Lowassa unategemea nini? Haiwezekani watu 24,000 waende kituoni kumpigia kura Rais tu halafu wasipige za Mbunge. Utaratibu ulikua watu kupiga kura 3. Sasa iweje waliopiga kura za Urais Bumbuli wawe wengi kuliko waliopiga za Mbunge? Yani mtu alienda kituoni akapewa karatasi ya Rais tu, alipopiga akaondoka bila kupiga ya Mbunge?.

3. Majimbo mengi asilimia za kura zimeonekana kuzidi 100 jambo ambalo linadhihirisha wizi wa waziwazi. Jimbo la Monduli Arusha Lowassa anatajwa kupata kura 49,675 na Magufuli kura 11,335 lakini wote wametajwa kuwa na asilimia zinazolingana (18%).

Jimbo la Arusha Mjini Lowassa anatajwa kupata kura 150,107 na Mgombea wa Chauma amepata kura 551 lakini wote wametajwa kuwa na asilimia zinazolingana (69%). Yani Lowassa amelingana na Hashim Rungwe jimbo la Arusha mjini.

Jimbo la Ndanda ukijumlisha asilimia za wagombea zinakuja 108%. Jimbo la Arusha mjini zinakuja asilimia 182% na majimbo mengine hivyo hivyo. This means waliopewa kazi ya kuiba kura walikosa umakini. CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu.

4. Baadhi ya majimbo idadi ya kura zilizopigwa imezidi idadi ya wapiga kura. Kwa mfano ukijumlisha matokeo ya Jimbo la Makunduchi Zanzibar kwa wagombea wote utapata kura 10,382. Lakini idadi ya kura halali ni 10,352. Yani kura zilikua nyingi kuliko idadi ya wapiga kura. Sasa sijui kama kuna watu walipiga kura mara mbili au vp. CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu.

Hali hiyo pia imejitokeza katika jimbo la Kilindi, jimbo la Bumbuli na majimbo mengine. Hii inapaswa kuingia kwenye kitabu cha records za dunia (Guiness) maana ni maajabu kupata kura nyingi kuzidi idadi ya wapiga kura.

Mwaka 1927 aliyekua Rais wa Liberia Charless King aliingia kwny kitabu cha Guiness baada ya Tume ya uchaguzi nchini humo kumtangaza kuwa ameshinda kwa kura 234,000 wakati idadi ya wapiga kura nchini kwake ilikua 15,000 tu. NEC nao wamefuata nyayo za Charless King. Wanapenda namba lakini hawajui hesabu.

5. Kwa mujibu wa NEC jimbo la Bumbuli na Bukoba mjini ndio majimbo yenye watu smart kuliko majimbo yote Tanzania maana ndio majimbo pekee ambalo hakuna hata kura moja iliyoharibika.

Kwa mfano Bumbuli Idadi ya wapiga kura ni watu 44,011 na idadi ya kura halali ni 44,011. Haya ni maajabu mengine ya dunia. Yani ktk watu 40,000 hakuna hata mmoja aliyekosea. These people are very smart.

Ni ajabu jimbo la Makunduchi Zbar lenye wapiga kura 10,000 walioharibu kura ni watu zaidi ya 100 lakini jimbo la Bumbuli lenye wapiga kura zaidi ya 40,000 hakuna hata mmoja aliyeharibu kura. Kama unaelewa Probability utajua huu ni uongo wa kiwango cha PhD. Watu 44,000 are more likely kuharibu kura nyingi kuliko watu 10,000. KaJanuary hakajui hii formular coz kanapenda namba tu lakini hakajui hesabu. Itz shame.

NINI CHANZO CHA YOTE HAYA?

Sababu inayopelekea fraud hii ya kijinga ktk kutangazwa matokeo inasababishwa na Tume kuacha kutangaza matokeo halisi na kuamua kutangaza matokeo wanayopewa na CCM.

Kuna kikosi kazi cha vijana wa CCM wanaofanya tallying na kuwatumia Tume ya Uchaguzi. Kwa hiyo matokeo yanayotoka majimboni hayaendi moja kwa moja Tume, yanapita kwanza kwa vijana wa CCM wanayachezea ndipo yanaenda Tume. Katika kufanya kazi hiyo wanakosa umakini na kukosea hata vitu vidogo kama niliorodhesha hapo.

Licha ya kubadilisha matokeo ya Urais, mbinu nyingine wanaofanya ni kupunguza kura za Lowassa kwa kuongeza kwenye idadi ya kura zilizoharibika. Katika majimbo mengi Lowassa aliyoongoza hata idadi ya kura zilizoharibika ni nyingi.

Hebu jiulize imekuaje jimbo la Arusha mjini watu zaidi ya 5000 waharibu kura? Watu 5000 ni sawa na wakazi wote wa jimbo la Wawi Zanzibar. So ni sawa na kusema jimbo lote la Wawi wameharibu kura. Impossible.!

Mbinu nyingine ni kupunguza kura za Lowassa na kuwaongezea wagombea wa vyama vidogo. Kwa mfano jimbo la Moshi mjini mgombea wa ADC alipata kuta 11 jimbo zima. Na fomu ya matokeo iliyobandikwa ofisi ya Mkurugenzi inaonesha hivyo. Lakini kwenye matokeo yaliyotangazwa na Tume inaonekana amepata kura 186. Ongezeko la kura 175. Ujinga huu wameufanya ktk majimbo mengi.

WAY FOWARD.

Sisi tumefanya tallying ya majimbo yote ya nchi nzima na tunayo matokeo halisi kama yalivyosainiwa na mawakala wa vyama vyote. Matokeo hayo yanaonesha maoni halisi ya watanzania.

Viongozi wa chama wanakutana leo na muda si mrefu watatoa tamko. Rais wa Tanzania anachaguliwa na Watanzana, ni vizuri kuheshimu maamuzi yao.!

Ningekuwa Invisible , hii comment ningeipandisha hapo juu kwenye uzi huu.
 
Last edited by a moderator:
Jimbo la Bumbuli matokeo ya Ubunge yanaonesha kuwa waliopiga kura ni watu 20,512 ambapo January Makamba amepata kura 17,805. Lakini cha ajabu kwenye matokeo ya Urais jimbo hilohilo la Bumbuli waliopiga kura ni watu 44,011 ambapo Magufuli anadaiwa kupata kura 35,801.

Sasa jiulize imekuaje waliopiga kura za mbunge wawe watu 20,512 halafu kura za Rais wawe 44,011. Yani kuna watu 24,000 walienda vituoni kupiga kura za Rais tu lakini hawakupiga za Mbunge.

Haya ni maajabu ya dunia. Haihitaji degree kujua kwamba Tume imeongeza wapiga kura hewa 24,000 na kura zote hizo wakampa Magufuli.
Weka na ya ubunge tukuamini unachokiongea
 
Duh......haya sasa ngoja wafia chama waje hapa na mapovu mdomoni kutetea matatizo.

Nimekupenda bure...Watoto wao hawana ada wamefukuzwa shule, eti FISIEMU oyeee...are serious?:angry::angry::angry:
 
Mheshimiwa UKAWA ilianzishwa ili kutetea ile katiba ya Tume ya Warioba, ambayo ilikuwa na kipengele kinachoruhusu matokeo ya urais kuhojiwa mahakamani. EL kwa kudhani angepitishwa na CCM akafadhili hujuma dhidi ya katiba pendekezwa, ikadoda hadi leo. Leo yuleyule mamba aliyemfuga mwenyewe anamtafuna, wacha amtafune!
Kisa hiki (real story) kinatufundisha kuwa katiba ya wananchi ni ya wote. Kama uko chama tawala leo, kesho utakuwa upinzani. Mwenzetu huyo keshatafunwa na mamba, tuliobaki tujifunze kuwa jambo la maslahi ya taifa tunapaswa kulipigania sote, bila kujali tuko chama gani linapotokea suala hilo. Leo tunashindwa kuhoji haya mambo mahakamani kisheria kwa sababu katiba inakataza, ileile EL na wenzie waliyoitetea. Tumeona elimu ni ghali, tumejaribu ujinga tumeona matokeo yake, sasa tunahitaji matibabu.

Labda umalizie vile vile kuwa wananchi siyo wapumbafu na malofa kama watu wengine wanavyofikiria. Wengi hawasemi lakini wanajua kinachoendelea na wanaweza kuadhibu muda ukifika. Hayo ndiyo yaliyotokea Dar es Salaam katika uchaguzi huu.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom