Matokeo rasmi ya Urais kwa mujibu wa NEC (Official Results) - Uchaguzi Mkuu 2015

Dalili za urais kwa lowassa zilionekana tangu yuko ccm na baada ya kujikomboa sasa ni wazi kuwa atapata urais kwa haki..
Huu ni wakati ambao NEC-CCM wanajishauri kutangaza matokeo yaliyobaki baada ya kuona lowassa kampita magufuli katika kura zilizobaki wapo wanashauriana wakatangaze au wachakachue kabisa ila wanashindwa kuchakachua kwa sasa kelele za wanamabadiliko zimekuwa nyingi hawana jinsi itabidi waje watangaze tu..
Walisema watatangaza saa tatu asubuhi hadi wakati huu saa 5 hii bado hawajatangaza nini maana yao baada ya kuona lowassa atashangaza watu kwa kura nyingi alizopata katika majimbo yaliyosalia..
Tunaomba matokeo ili lowassa atangazwe kwa kishindo ushindi wa kusawazisha na kuongeza amin nawaambia lowassa asipotangazwa rais wa tanzania kuna hujuma nyingi sana zimefanyika ila leo hadi kieleweke tunataka lowasa atangazwe rais wetu
Mi nikajua labda kuna njia nyingine kama kuingia msituni? Kwa upande wa kura, sahau, kwanza ndo dozi kali inafuata! Mpaka sasa Magufuli kamuacha lowassa 1.6, kilimanjaro na Arusha tayari, Mbeya nimegundua ni porojo tu za ukawa, sio ngome ya chadema! Ukitoa mbeya mjini.
 
Thubutu nani atangaze unakumbuka hadithi ya nani atamfunga paka kengele halafu panya mabaka kajitia kimbelembele unajua kilichompata
 
Dogo unachekesha kweli, Lowassa mwenyewe ameshaingiza upepo tayari na ameshasema eti ameibiwa kura. Magufuli ni rais tayari anasubiria tu kuapishwa. Lakini sio vibaya ukiendelea kuota ndoto za mchana. Una haki ya kuota dogo. mpaka sasa hivi CCM wana viti vya ubunge 130 na CHADEMA wana viti 30 tu. Yamebakia majimbo 69 tu. Hata kama CHADEMA watashinda viti vyote hivi vilivyobakia bado hawatakuwa na uwezo wa kuunda serikali. Na sio rahisi wakapata viti vyote hivyo 69 vilivyobakia. Hauhitaji kuwa na PHD kutambua mahesabu haya rahisi kabisa. Lakini sio vibaya kuota, wewe endelea kuota. #HapaKaziTu
 
Mkuu...

Hadi sasa Magufuli ana KURA 6.1 MILIONI...

Lowassa ana kura 4.3 milioni...!!!

Pamoja na kuchakachua kote.. ila sasa majimbo yaliobakia wamekwama kutangaza, sbb Lowassa ataziba hilo gap...!!! Trust me...!!

kweli kabisa mkuu mimi hainiingii akilini sehemu walizopiga goli la mkono wametangaza mapema sehemu walizoshindwa wanasuasua kutangaza hadi sasa tangu saa 3 tume hawaonekani ukumbini
 
Ndugu zangu wa ukawa ni kweli tumepigwa goli LA mkono na ni ujinga wetu tumeshidwa kulizuia kwahiyo tukubali tu au itafutwe alternative nyingine ila kwa kura thubutu hatutoki ingawa roho inaniuma ila ndo ukweli
 
Nina imani na Lowasa na cjawai kata tamaa hata siku moja hata likibak jimbo moja na maguful anaongoza kwa kura milioni 10 bado Nina I

Wewe ndo uliyeenda kupiga magoti kwa ostadh Juma na Musoma??
 
Dalili za urais kwa lowassa zilionekana tangu yuko ccm na baada ya kujikomboa sasa ni wazi kuwa atapata urais kwa haki..
Huu ni wakati ambao NEC-CCM wanajishauri kutangaza matokeo yaliyobaki baada ya kuona lowassa kampita magufuli katika kura zilizobaki wapo wanashauriana wakatangaze au wachakachue kabisa ila wanashindwa kuchakachua kwa sasa kelele za wanamabadiliko zimekuwa nyingi hawana jinsi itabidi waje watangaze tu..
Walisema watatangaza saa tatu asubuhi hadi wakati huu saa 5 hii bado hawajatangaza nini maana yao baada ya kuona lowassa atashangaza watu kwa kura nyingi alizopata katika majimbo yaliyosalia..
Tunaomba matokeo ili lowassa atangazwe kwa kishindo ushindi wa kusawazisha na kuongeza amin nawaambia lowassa asipotangazwa rais wa tanzania kuna hujuma nyingi sana zimefanyika ila leo hadi kieleweke tunataka lowasa atangazwe rais wetu
Dogo unachekesha kweli, Lowassa mwenyewe ameshaingiza upepo tayari na ameshasema eti ameibiwa kura. Magufuli ni rais tayari anasubiria tu kuapishwa. Lakini sio vibaya ukiendelea kuota ndoto za mchana. Una haki ya kuota dogo. mpaka sasa hivi CCM wana viti vya ubunge 130 na CHADEMA wana viti 30 tu. Yamebakia majimbo 69 tu. Hata kama CHADEMA watashinda viti vyote hivi vilivyobakia bado hawatakuwa na uwezo wa kuunda serikali. Na sio rahisi wakapata viti vyote hivyo 69 vilivyobakia. Hauhitaji kuwa na PHD kutambua mahesabu haya rahisi kabisa. Lakini sio vibaya kuota, wewe endelea kuota. #HapaKaziTu
 
Tena Uchaguzi ukirudiwa mtaumia zaid maana maharamia wa Mtandao wamesamabaratishwa tayari. Mlisema mtachukua nchi kabla ya kwisha misa ya kwanza October 25 mbona misa yenyewe ni ndefu sana mpaka leo Alhamis haijaisha
 
Mkuu kahtaan umenena.
Viongozi nao wana mioyo ya nyama kama sisi na kimsingi wote tunategemeana lakini wananchi ndio force kubwa zaidi. Tatizo kubwa investment kubwa iliyofanyika Tanzania ni katika ujinga na itatutesa kweli. Mtu mwenye uelewa (elimu) wa kweli anaweza kuwa na maono kuwa nitashinda njaa siku tatu lakini matokeo ya hiyo njaa yanaweza kunipa shibe ya miaka mitatu.
Nimeona juzi tu Afrika kusini (sawa wametutangulia) wanafunzi wamezuia kuongezwa karo na wakafanikiwa kwa asilimia 100.
Huwezi kupata msaada wa kupambana na magari ya washawasha na mabomu endapo utaishia tu kutii ile amri ya "ukidai chako utakiona", ukiamua kuandamana kwa mfano ndipo utagundua kuwa aliyekutishia 'utakiona' sio yeye anayerusha mabomu bali kawaweka mbele vijana ambao ni watoto wa masikini na wana njaa kama mimi na wewe! Na hapo mtaungana kudai hizo haki pamoja. Ukikaa tu chini hakuwezi kuwa na matokeo, kinyume cha hapo tuendelee kukaa na kuishia kusema 'wamechakachua' wakati tukijua (sina uhakika kama tunajua hili) kura yako ndio haki pekee na kuu katika maamuzi ya nchi.

Tatizo letu ni pale wananchi wanaposhindwa kukubaliana na sisi badala ya kutunga mbinu mpya na kujipanga upya tunafikiria kuwa tumehujumiwa au wananchi ni wajinga. Hivi hawa mnaoleta haya madai, mmefanya kweli utafiti usio na Chembe ya unafiki mkaona kuwa mlikuwa na "case" ya uhakika??

Watanzania wanahitaji watu wenye "case" ya uhakika. Ukiwa "case" yako imeshindwa badala ya kukata tamaa ni afadhali utafute mbinu mbadala badala ya kuanza kuwaona wale ambao hawajakubaliana na wewe kuwa ni wajinga. Fanyeni utafiti makini. Angalieni majimbo walikoshinda wapinzani; utajua walikuwa na "case" yenye nguvu. Majimbo mengi ambayo wapinzani waliokoteza wagombea wameshindwa! Sasa una wagombea wa kuokoteza; wakishndwa unajaa upepo na kulalama kuwa watu ni wajinga sababu hawajachagua mgombea wako!! kweli??

Siku wananchi wakikubaliana na "case" ya wapinzani, mambo yatakuwa automatica. As for now bado. Case ya Lowasa ilikuwa weak, kwa sababu ni case ambayo imeshindwa CCM. Kama hilo mlikuwa hamulioni, wapo walioliona. Nguvu mlizokuwa mkizitumia ku argue, haziifanyi case yenu iuzike zaidi. Finally we have to agree with one thing, people choose leaders they trust. If they don't choose you, they are not stupid, they simply don't trust you!
 
hawatendi haki kabisa hawa jamaa kila kitu wanafanya kwa maslahi yao tu hawamwogopi hata Mungu

Pole Alphaking, kwani ccm wanamjua Mungu? CCM wakati wakifunga kampeni zao Mwanza walisema wamestopisha mvua kwa nguvu za waganga wao! Nashangaa nchi inaongozwa kwa uganga! Mungu kwao ni historia kakangu! Polen wanamabadliko, pole Tanzania na kizazi kitakachokuwa ktk utawala wa kijani bila ridhaa yao!! Kama kweli Mungu UPO, utafanya jambo, haijalishi kwa wingi wao wanatubeza kwa kiasi gani baada ya kutuibia! Njia za Mungu ni nyingi na za ccm ni mbili tu, yaani kuiba na mabavu!:angry:
 
Dogo unachekesha kweli, Lowassa mwenyewe ameshaingiza upepo tayari na ameshasema eti ameibiwa kura. Magufuli ni rais tayari anasubiria tu kuapishwa. Lakini sio vibaya ukiendelea kuota ndoto za mchana. Una haki ya kuota dogo. mpaka sasa hivi CCM wana viti vya ubunge 130 na CHADEMA wana viti 30 tu. Yamebakia majimbo 69 tu. Hata kama CHADEMA watashinda viti vyote hivi vilivyobakia bado hawatakuwa na uwezo wa kuunda serikali. Na sio rahisi wakapata viti vyote hivyo 69 vilivyobakia. Hauhitaji kuwa na PHD kutambua mahesabu haya rahisi kabisa. Lakini sio vibaya kuota, wewe endelea kuota. #HapaKaziTu

magamba utawajua tu lakini nakwambia wananchi tumechoka na ndio tunaoamua kuwatoa madarakani
 
Back
Top Bottom