Matokeo rasmi ya Uchaguzi mdogo wa mitaa Magu: CHADEMA yaigalagaza CCM

Mbusule

Member
Aug 2, 2011
87
83
Kulikuwa na uchaguzi mdogo wa mitaa miwili, vijiji 6 na vitongoji 37... Pia nafasi 120 za wajumbe wa serikali za vijiji.

CHADEMA kimeendelea kuitesa CCM ambapo kimezoa mitaa yote miwili (Bank & Ihimbili), vijiji vinne kikiwemo cha Nyahanga kata ya Sukuma ambapo Mbunge wa sasa wa Magu anatokea (viwili wamegawana CCM+UDP), wajumbe wa serikali za mitaa 80, vitongoji 16 kati ya 20 walivyosimamisha wagombea (2 CCM, 1UDP & 1CUF).

CCM imeanza kuaga pole pole!
Ndiyo Wakuu, Heshima kwenu!

Hatimaye ile kauli ya Mjinga akijitambua mwelevu yupo matatani ime endelea kujidhihirisha jana baada ya cdm kuigalagaza vibaya ccm katika uchaguzi wa serikali za vijiji na vitongoji wilayani Magu .

Kwa mujibu wa matokeo ni kuwa vijiji vilivyo kuwa vinagombaniwa jumla yake ni 5 ambapo CHADEMA imeshinda vijiji 3 vya Kahangara, Kabila na Ihayabuyaga.

CCM imeambulia kijiji 1 cha Langi na UDP nacho pia kime ambulia kijiji 1.

Katika upande wa vitongoji, jumla kulikuwa na vitongoji 37 ambapo vitongoji 17 CCM imepita bila kupingwa kwasababu ya jiografia na maandalizi. Hivyo kwenye vitongoji 20 vilivyo gombaniwa cdm imepata vitongoji 14 na ccm imeambulia vitongoji 6.

Vilevile ndani ya vitongoji 14 vilivyochukuliwa na CHADEMA kuna kitongoji cha Bugando kijiji cha Lemeji kata ya Sukuma anakotoka Mbunge Dkt Festus Limbu.

Pia kuna kitongoji cha Mtaa wa bank -NMB Magu mjini kilichopo kwenye makao makuu ya CCM Magu mjini kimebebwa na CHADEMA kwa kura nyingi.

Mwl Nyerere ktk Kitabu cha "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania" -1973 alipata kusema

"WATU WANAWEZA WAKACHOKA NA KUSEMA POTELEA MBALI WAKACHAGUA CHAMA CHOCHOTE ILI MRADI TU WAONDOKANE NA KANSA YA UONGOZI WA CCM. HAINIFURAHISHI KUYASEMA HAYA ,LAKINI UHAI WA NCHI YETU UNATAKA YASEMWE ."
 
Hongera Chadema,ccm wanajisahau kuna chaguzi ndogo ambazo ni muhimu kwa uchaguzi mkuu 2015,Mungu amewapiga upofu wapo busy kuchafua Chadema na hawajui wanapoteza muda
 
Haya mapigo ni kama yale ya Bruce Li kwenye ile movie ya Enter the Dragon,,, watu wa enzi zetu tunayakumbuka yale mapigo...

CCM amefuatwa kwenye ngome yake na kupigwa huko huko. We Nape endelea kuhubiri Elimu ya Mnyika huku wenzio wanachukua nchi taratibu, siku unashtuka nchi yote iko mikononi wa CDM. Hongereni makamanda kwa kazi nzuri sisi wananchi tuko nyuma yenu
 
Bado Wakina Nape hapa wanapambana na watu, Jamaa kwa sasa kazi yao ni kusimam majukwaani na Kuitamka CHADEAMA mara 100 wakati CCM inatamkwa mara 8,

Ninacho Furahi kwa sasa kama ilivyo kuwa zamani kwamba ukisha pitishwa na CCM basi wewe jihesabu kwamba umeshinda kwa sasa ni tofauti kabisa, kwa sasa ukisha pitishwa na CHADEMA basi umeshinda
 
Haya mapigo ni kama yale ya Bruce Li kwenye ile movie ya Enter the Dragon,,, watu wa enzi zetu tunayakumbuka yale mapigo...

CCM amefuatwa kwenye ngome yake na kupigwa huko huko. We Nape endelea kuhubiri Elimu ya Mnyika huku wenzio wanachukua nchi taratibu, siku unashtuka nchi yote iko mikononi wa CDM. Hongereni makamanda kwa kazi nzuri sisi wananchi tuko nyuma yenu

Kazi nzuri sana ya Kamanda Mawazo, Huyu jamaa ni Balaa kabisa, ni sawa na secretariet yote ya Magamba, na ni kweli jamaa wako bise kuthibitisha vyeti vya Mnyika kana kwamba ndo vimesababisha hii nchi iwe masikini,
 
Hongera kwa wananchi wa magu.................... wameujua ukweli.
Kuichagua ccm ni kuchagua utumwa.
Kuichagua chadema ni kuchagua ukombozi wa kweli
 
Kulikuwa na uchaguzi mdogo wa mitaa miwili,vijiji 6 na vitongoji 37... Pia nafasi 120 za wajumbe wa serikali za vijiji..CHADEMA kimeendelea kuitesa CCM ambapo kimezoa mitaa yote miwili(Bank& ihimbili), vijiji vinne kikiwemo cha Nyahanga kata ya Sukuma ambapo Mbunge wa sasa wa Magu anatokea( viwili wamegawana CCM+UDP),wajumbe wa serikali za mitaa 80, vitongoji 16 kati ya 20 walivyosimamisha wagombea(2CCM, 1UDP&1CUF).CCM imeanza kuaga pole pole!

Hongereni sana Chadema na wote wenye nia njema na taifa letu ingawa hapo kwenye red kidogo inanipa shida; kwamba jumla ya vitongoji vilikuwa 37 na katika hivyo Chadema wakasimamisha wagombea katika vitongoji 20 tu! Na katika hivyo 20 wakanyakua vitongoji 16 (80%).

Hii maana yake hawakugombea vitongoji 37 - 20 = 17; yaani karibu nusu ya vitongoji! Tatizo liko wapi? Yaleyele ya 2010 kati ya majimbo 270 waligombea majimbo 80 tu! (only about 30%)! Frankly speaking, Chadema inapaswa, pamoja na mambo mengine kuhakikisha wanaanza kufanya recruitment ya uhakika kila eneo. Hopefully, mgawanyo wao wa kiutawala waliouzindua hivi karibuni (Provinces/Zones) utafanikisha hili. Hatutaki tena kusikia eti kuna sehemu Chama hakikusimamisha mgombea - nafasi zote kuanzia ya chini kabisa hadi ya mwisho.
 
Mwenye Ile song ya Sarafina FREEDOM IS COMING TOMOROW pls aiweke ile iwe Dedcation kwa Makamanda wote Tanzania Nzima
 
Kulikuwa na uchaguzi mdogo wa mitaa miwili,vijiji 6 na vitongoji 37... Pia nafasi 120 za wajumbe wa serikali za vijiji..CHADEMA kimeendelea kuitesa CCM ambapo kimezoa mitaa yote miwili(Bank& ihimbili), vijiji vinne kikiwemo cha Nyahanga kata ya Sukuma ambapo Mbunge wa sasa wa Magu anatokea( viwili wamegawana CCM+UDP),wajumbe wa serikali za mitaa 80, vitongoji 16 kati ya 20 walivyosimamisha wagombea(2CCM, 1UDP&1CUF).CCM imeanza kuaga pole pole!

Kama napaa angani vile! Unajua ccm ilishatufanya mtaji sisi maskini halafu wao wanaficha mabilioni nje huku wakituhonga sabuni, chumvi, dagaa, vitenge/khanga na pombe kabla ya ubwabwa wanapokuwa wameshinda. Tuwakataeni. Maji ya ziwa victoria yanaweza kutoka mwanza kwenda kahama kwenye miradi yao hadi shinyanga kwenye sekondari ya savannah halafu yasifike vijiji vilivyo karibu na shule hiyo inayosemekana kuwa ya first lady. Hii ni dharau kubwa kwa mtu maskini!
 
Nashindwa kuelezea furaha niliyonayo,Mungu ibariki CDM,wabariki na uwape afya njema makamanda wote,tuseme amen
 
Back
Top Bottom