Matokeo kuhusu JK kule ThisDay mpaka sasa leo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matokeo kuhusu JK kule ThisDay mpaka sasa leo!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwanamayu, Oct 8, 2010.

 1. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Do you approve or disapprove of President Jakaya Kikwete's overall job performance (2005-2010)?

  Approve (5%, 4 votes)
  Disapprove (94%, 83 votes)
  Undecided (1%, 1 votes)

  Total Votes: 88

  ThisDay http://www.thisday.co.tz
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Poa wale jamaa wa redet ni wachakachuaji tu!
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Sauti ya watu hii!
  Sasa wale jamaa zangu waliokaa mahali kusikojulikana na kutoa 72% wanamtumikia nani?
   
 4. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Asante mkuu, na kumbe bado poll inaendelea, so tafadhali pigeni kura huko ambako hakuna uchakachuaji kama wa REDET, aibuuu.. wasomi wazima kuchakachua mchana kweupe!
   
 5. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  jAMANI HAWA CCM WANAITAKIA MEMA NCHI HII KWELI?? HATA YA UHURU ILIONYESHA UONGOZI WA JK HAUKUBALIKI!
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  na sauti ya watu nisauti ya Mungu, anaeipinga atakwenda na Maji. kama mzee wa majini.
   
 7. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]TUIGE WELEDI NA UZALENDO TOKA JWTZ[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot](Source: RAIA MWEMA NEWSPAPER)
  [/FONT]

  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]ONYO la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na vyombo vingine vya usalama limeibua mjadala mpana na mzito nchini. Ni mjadala unaohusu weledi wa mijeledi. Wengine katika vyombo vya habari wanapigia kelele wakisema si weledi kumbe wanaogopa mijeledi!

  Baada ya Luteni Jenerali Abdulraham Shimbo kutoa onyo, wapo waliostuka na wakidhani JWTZ imetangaza hali ya hatari, wengine wakidiriki kusema imedhamiria kuinusuru CCM huku wengine wakisema ilikuwa ni kazi ya jeshi la polisi.

  Niliposikia hayo wakati nikiwa katika ndege, niliogopa nikidhani wajomba wamechukua hatamu sasa. Hawataki upuuzi na wanataka Jakaya Kikwete aongoze nchi vyema hadi matokeo ya uchaguzi mkuu yatakapotangazwa.

  Lakini baada ya kukaa na kutulia, nilitafuta kauli sahihi iliyorekodiwa na kisha nilipata taarifa sahihi kwamba kumbe JWTZ haijatoka kambini kama ilivyokuwa imeripotiwa na wanasiasa na wadau wengine!

  Kumbe ilichokuwa imekifanya JWTZ ni kujaribu kuonya vyama (ikiwemo CCM) kwamba hakuna damu itakayomwagika; kwani uchaguzi utafanyika katika mazingira ya amani na utulivu.

  Ila, kilichonistua na kuonyesha watu hawajaelewa mantiki ya onyo la JWTZ ambalo ni jeshi lenye historia ya utiifu, ni pale wanasiasa wa Upinzani walipoibuka na nadharia kwamba jeshi limelenga kuinusuru CCM.

  Nilipaswa kurejea onyo la Luteni Jenerali Shimbo, lakini bado nilipata ukakasi kuoanisha na kile kilichozungumzwa na Upinzani asubuhi yake. Wapinzani ambao baadhi tunafikiri ni wanasiasa wasomi, wakajikuta katika lindi la ujinga.

  JWTZ ilisema, kwa niaba ya vyombo vya ulinzi na usalama: "Hakuna umwagaji damu utakaofanyika. Uchaguzi utafanyika kwa amani na kwamba vyombo hivyo viko tayari kupambana na yeyote atakayejaribu kuvuruga amani."

  Hapa ukifanya uchambuzi wa kimaduhui, huoni hata sehemu moja ambayo JWTZ inasema imepanga kuibebea mbereko CCM kama ilivyodaiwa na vyama vingine vya Upinzani.

  Jambo la ajabu kabisa ni kwamba, hata mwanangu wa chekechea alimwelewa Shimbo. Alichokisema ni kwamba, wao wa vyombo vya ulinzi na usalama watakabiliana na yeyote atakayejaribu kuvuruga amani ya nchi.

  Lakini, nilistuka kusikia eti JWTZ imepanga kuinusuru CCM! JWTZ haikusema kwamba vyama vya Upinzani vikubali matokeo yoyote ambayo yatatangazwa kwamba CCM imeshinda. Ilichosema ni kwamba vyama vya siasa, ikiwemo CCM, vikubali matokeo yoyote.

  Sasa unaweza kuona jinsi uwezo wa kufikiri wa baadhi ya wanasiasa wetu ulivyo mdogo au kuchanganyikiwa na mambo mengi ya maisha. Ni wanasiasa wenye migogoro ya kinafsia.

  Wanasiasa wenye migogoro ya kinafsia, kifamilia na jamii, ndiyo ambao huweza kutamka na kurupoka kile walichoota jana usiku kwamba, kuna njama za kutaka kumuua. Inawezekana jana usiku mwanasiasa aliota kakabwa na jinamizi la usingizini, basi, anaamka asubuhi na kuambia umma yuko tayari kuuawa!

  Huu ndiyo ujumbe tuliopata baada ya JWTZ kutoa onyo. Jeshi lina dhima ya kulinda nchi kutoka maadui wa ndani na nje, Jeshi lina intelejensi yake (Military Intelligence), kwa mantiki hiyo, linapozungumza kuna njama za watu kuvuruga amani, huwa halikurupuki.

  Nilitegemea wananchi walipongeze jeshi kwa kuonyesha msimamo mapema na kutoa onyo kwa watu wanaotaka kuivuruga nchi. Unashangaa unaona wanasiasa wenye kuangalia madaraka badala ya Tanzania wanakurupuka na kulihusisha jeshi na mbeleko kwa CCM.

  Wapo wanaosema JWTZ imeenda mbali zaidi kwani hilo lilikuwa jukumu la jeshi la polisi, lakini wamesahau kwamba hatua ya jeshi kuchelewa kuchukua hatua ndiko kunakofanya nchi kuvurugika na damu kumwagika.

  Leo hii, watu wanalalamika uzembe katika kudhibiti mauaji ya halaiki ya Rwanda, kwa sababu Dk. Kofi Annan akiwa mkuu wa Ulinzi na Usalama wa UN, alishindwa kushauri umoja huo haraka kuzuia mauaji nchini humo.

  Kwa mantiki hiyo, JWTZ iko sahihi kuhakikisha amani ya nchi haivurugwi na maadui wa ndani au nje. Jeshi limekuwa sahihi kutoa onyo mapema kwa sababu hatuwezi kuruhusu umwagaji damu wa kutisha ndipo tuombe nguvu za jeshi.

  Amani na usalama wa nchi haufanyiwi majaribio. Amani, uhuru na umoja wa kitaifa unalindwa kwa nguvu. JWTZ imekaa katika nafasi yake husika.

  Nimestushwa kusikia kauli ya JWTZ ikihusishwa na mbereko dhidi ya CCM. Hili ni jambo la kipumbavu. Kwa nini CCM ikae kando wakati nacho ni chama cha siasa kinachopaswa kutii matokeo kama kikishindwa?

  Uropokaji huu wa wapinzani umezidi kuifanya CCM ionekane kama ni chama makini, kilichobobea katika siasa na kisichokurupuka. Ndiyo maana, ingawa chenyewe ni chama cha siasa, hakikutaka kukurupuka na kuirukia JWTZ.

  Kwani kinajua jeshi letu lina nidhamu ya hali ya juu, halijihusishi na mambo ya siasa za majitaka, lina nidhamu, utiifu na uzalendo.

  Hivyo, kudhani kauli ya JWTZ ni mbereko kwa CCM ni mawazo yasiyosadikika, na ni dhana tu isiyo na mashiko. Ni vema vyama vikaiga ukimya wa CCM. [/FONT]
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Tatizo la wenzetu wa REDET watadai hayo ni mawazo ya watu wa mijini wenye uelewa wa kompyuta lakini nderemo za mikutano ya Dr. Slaa huko vijijini hawaioni?

  Jamani hata kama JK amewaahidi vyeo serikalini lakini uzalendo na heshima ya taaluma yenu nyie REDET kweli yote mpo tayari kuitupia kaburini kweli?

  Sasa baada ya NEC kumtangaza Dr. Slaa ni mshindi hayo matope mtajifuta vipi ambayo tayari mmekwisha kujipaka?
   
Loading...