NasDaz,Kama ndivyo ilivyotokea bado naendelea kushikiria msimamo wangu kwamba kuna ulazima viwango vya zamani vitumike......it's wasn't fair at all! Mitihani imefanyika somewhere around October - November huku wahusika wakuu (wanafunzi wakiwa wanafahamu wazi kwamba grading ipo hivi!! Mitihani wameshafanya, wametulia nyumbani wanasubiria matokeo; huku nyuma wapuuzi wachache wanakaa na kuweka viwango vipya....NO, UNACCEPTABLE! Narudia, wengi wetu tunatamani kila wakati tupate sababu ya kuilaumu serikali; hapa wasilaumiwe kwa kurudisha viwango vipya bali walaumiwe kwa kutumia viwango vipya kinyemela (bila wahusika waathirika wakuu) kufahamu! Tuache ubinfasi wa kujiona tumeshavuka mto! Hapa JF nafahamu kuna wanafunzi wengi wa vyuo vikuu! Assume, tangu unaingia First Year unafahamu (say) C inaanzii 50-64; na umefanya paper unafahamu hivyo ndivyo viwango! Hatimae unarudishiwa paper yako, unakuta umepata 52; unapumua kidogo coz' unafahamu umepata C. Matokeo yanawekwa notice board, unakuta somo husika umewekewa D; unakuja kuhoji unaambiwa mara baada ya mitihani kwisha; board ilikaa na kuweka viwango vipya ambavyo C inaanzia 55-69! Let's be honest here...hivi kweli huko vyuoni kungekalika?! Yaani from nowhere, muambiwe viwango vibadilishwa tena kimya kimya! HAPANA, HILI HALIKUBALIKI! Hao wote waliokaa na kupitisha maamuzi sio waathirika wa moja kwa moja, waathirika wa moja kwa moja ni wanafunzi waliohusika na wazazi/walezi wao!
cc JokaKuu
..lakini NECTA ni chombo cha serikali pia.
..umesahau kwamba mtendaji mkuu wa necta anateuliwa na raisi??
..binafsi nadhani students were not supposed to fail that much hata kama grading scheme[madaraja]imebadilishwa.
..naamini wanafunzi wameathirika kiasi kile kwasababu wengi wao wanafaulu at borderline.
cc: Kichuguu, Kitila Mkumbo, @Kubwajinga, Nyani Ngabu