Shine
JF-Expert Member
- Feb 5, 2011
- 11,481
- 1,372
Eeh ndo yanaelekea ila ccm wameula..CCM oyee.!!
Uliza matokeo sasa usikie walivyoning'inizwa mpaka hamu ya kurusha tena bomu imewajia
Eeh ndo yanaelekea ila ccm wameula..CCM oyee.!!
chadema ni chalenger tu si champion bado hawajakubalika na watanzania bali ni wanywa viroba na waendesha bodaboda tu
Mkuu pole kwa maumivu lakini wapiga kura ndiyo wenye maamuzi ya mwisho kazi bado inaendelea.
Mkuu nadhani ukipata matokeo ya 16/6/2013 ukaangalia kwa ujumla CCM ilipata kura ngapi na Chadema ilipata kura ngapi (Jumla ya kura zote katika kata zote) unaweza kupata mwanga ni kwa jinsi gani Watanzania wanaikataa CCM na fedha zao chafu
Kwa hiyo waendesha bodaboda siyo watanzania? Na wanywa viroba pia? Nadhani hapo ulipo unatwanga kiroba ili kupunguza maumivu ya kushindwa a town kwa vile wewe ni mchina.
This is an important observation!
Sijafurahi kuona ccm ikipata zaid ya kura 100 kwenye kata za jiji la Arusha. CDM inapaswa kujipanga zaidi, ccm haitaancha kucheza michezo michafu zaidi ya bomu nakutisha raia. CDM ielekeze nguvu kwenye elimu ya uraia umuhimu wa vijana kujiandikisha na kupiga kura.
Nikiwa kama mmoja wa wapenda mabadiliko nashangazwa sana na matokeo ya Arusha muda huu'tulitegemea ccm kupata chini ya asilimia 10 ya kura zote'nikienda kwenye point moja kwa moja ni kwamba kama Arusha yenye watu walioamka kiasi hiki wameweza kupigia ccm kura nyingi kiasi hiki je mikoa ambayo bado imelala itakuwaje?
Sijui kama unaweza kutafakari na kuelewa ninachojaribu kuweka hapa'nafikiri kazi ni kubwa mno iliyo mbele yetu kwani kama Arusha ccm wameweza kupata kura nyingi hivi je 2015?itakuwaje'natoa wito kwa wapenda mabadiliko wote tuungane kwa hali na mali kuhakikisha tunaweka mambo sawa kwa mikoa yote'kwa kweli 2015 kuongozwa tena na ccm ni kuleta maangamizi zaidi kwa taifa letu
chadema ni chalenger tu si champion bado hawajakubalika na watanzania bali ni wanywa viroba na waendesha bodaboda tu
...yaa hata mimi nilitazama kwa mtazamo huo lakini nikajaribu pia kuangalia facts kwamba daftari lililotumika ni la 2010,pia hawa ccm walikuwa na special interest hapo arusho so naamini wamecheza kila aina ya rafu ili waharibu jina la cdm. So ukichukulia eneo ni dogo na wanaweza kupita nyumba kwa nyumba na kugawa buku ten hasa kwa watu wasio na msimamo...This is an important observation!
rosemarie kwanza ni muhimu utambue kwamba ccm ni chama dola, kina financial resources za serikali, kinatumia vyombo vya dola kufanya chochote wanachotaka, na ukizingatia mazingira ya Arusha ambapo watu wameuwawa katika mkutano wa Chadema na kisha siku mbili baadae wakapigwa tena katika uwanja huo huo wakiomboleza vifo vya wenzao na kama haitoshi ccm kwa kutumia mkuu wa mkoa na waziri ole medeye wakatumia nguvu ya ukabila mkoani Arusha, ni wazi kuwa lengo lao lilikaribia kutimia ni bahati nzuri kwamba wananchi wa Arusha walikuwa tayari kuifia demokrasia ndio maana tumefika hapo.
Pili ufahamu kuwa ccm haijafa kabisa Arusha isipokuwa kikiwa chama tawala na chama dola lakini kimezidiwa nguvu na Chadema. Pia kuna watu ambao bado wako ccm kutokana na maslahi yao binafsi kwahiyo wataendelea kuipigia kura.
Lakini kwa ujumla vitisho vya vyombo vya dola vimechangia kwa sehemu kubwa wananchi wengi kushindwa kujitokeza kupiga kura na hilo ndio lilikuwa lengo la ccm ili watumie fursa hiyo kuchakachua bahati mbaya kwao makamanda wa Chadema walikuwa wamejipanga vizuri mno na kudhibiti mianya yote ya kuchakachua. Hata hivyo ninaungana na wewe kwamba wapenda mageuzi wite tuungane pamoja kama kweli tunataka kuing'oia ccm madarakani mwaka 2015 kwakuwa wao wana nguvu ya pesa na vyombo vya dola.