Technician
JF-Expert Member
- Mar 30, 2010
- 841
- 224
na Sitta Tumma, Musoma
MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Musoma Mjini mkoani Mara na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Vedastus Mathayo, ametoa siri ya
kushindwa kwake nafasi hiyo, huku akilia na propoganda zilizoenezwa dhidi yake.
Amesema, kuangushwa kwake na mbunge wa sasa, Vincent Nyerere (CHADEMA), katika uchaguzi mkuu uliopita 2010 kumetokana na kile alichokiita kupakaziwa maneno na kuundiwa fitina zisizokuwa na ukweli ndani yake.
Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Mukendo, Mathayo ambaye alikuwa akizungumza huku akikatizwa kwa kuzomewa mkutanoni hapo, alisema miongoni mwa tuhuma alizokuwa akitupiwa wakati wa kampeni ni kuhusu madai ya kujimilikisha viwanja katika maeneo mbali mbali ya miradi mjini hapa.
"Nilipakaziwa na kuundiwa zengwe zisizokuwa na ukweli," alisema kisha kuzomewa. Baada ya kuzomewa akasema tena: "Ninyi pigeni kelele tu, Chroloquine ni chungu lakini inaponya," akazomewa tena.
Katika mkutano huo uliomalizika saa 12:15 jioni, chini ya ulinzi mkali wa askari wa Kutuliza Ghasia (FFU), mjumbe huyo wa NEC, Mathayo, alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuachana na kile alichokiita 'ushabiki' wa kisiasa.