Mathayo atoboa siri ya kushindwa Ubunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mathayo atoboa siri ya kushindwa Ubunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Technician, Jun 17, 2011.

 1. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  na Sitta Tumma, Musoma


  MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Musoma Mjini mkoani Mara na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Vedastus Mathayo, ametoa siri ya
  kushindwa kwake nafasi hiyo, huku akilia na propoganda zilizoenezwa dhidi yake.
  Amesema, kuangushwa kwake na mbunge wa sasa, Vincent Nyerere (CHADEMA), katika uchaguzi mkuu uliopita 2010 kumetokana na kile alichokiita kupakaziwa maneno na kuundiwa fitina zisizokuwa na ukweli ndani yake.
  Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Mukendo, Mathayo ambaye alikuwa akizungumza huku akikatizwa kwa kuzomewa mkutanoni hapo, alisema miongoni mwa tuhuma alizokuwa akitupiwa wakati wa kampeni ni kuhusu madai ya kujimilikisha viwanja katika maeneo mbali mbali ya miradi mjini hapa.
  "Nilipakaziwa na kuundiwa zengwe zisizokuwa na ukweli," alisema kisha kuzomewa. Baada ya kuzomewa akasema tena: "Ninyi pigeni kelele tu, Chroloquine ni chungu lakini inaponya," akazomewa tena.
  Katika mkutano huo uliomalizika saa 12:15 jioni, chini ya ulinzi mkali wa askari wa Kutuliza Ghasia (FFU), mjumbe huyo wa NEC, Mathayo, alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuachana na kile alichokiita 'ushabiki' wa kisiasa.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Muraaah wangemgema aache upuuzi wake
   
 3. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Ulinzi mkali wa nini sasa kama wewe unakubalika?
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hahaaa CCM bwana...
   
 5. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kwanini hawa FFU hawakumkamata?
   
 6. Raimundo

  Raimundo JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 13,552
  Likes Received: 10,940
  Trophy Points: 280
  Izi dakika 15 zilizozidi vip? Mbona hakukamatwa kwa kuzidisha muda wa 12:00 kwa sababu nakumbuka Zitto alikamatwa kwa kuzidisha dkk 20. Sheria si msumeno eeh?
   
 7. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  NEC!? Siyo kuwa alikuwa mjimbe kwa nafasi ya Ubunge, hivyo hapaswi kuwa NEC tena au Katiba ya CCM ilibadilishwa?
   
 8. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Polisi ni CCM mpaka katiba mpya itakapo patikana na ku-overhaul hilo jeshi la kikoloni
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Pole sana Muraa!!!

  subiri Next time
   
 10. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  yeye ni nani by the way? wameshindwa kina mramba sembuse yeye?
   
 11. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Teh! Eti CHROLOQUINE NI CHUNGU ILA CHUNGU TEH!
   
 12. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Huyu si ndiye aliyedai madawati yake baada ya kushindwa?
  Gamba lililovuliwa... Hongera sana wananchi wa Musoma
   
 13. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2011
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Hivi kesi ya Mramba na Yona niaje au ulikua mtaji wa magamba, I am SORRY OFF THREAD
   
 14. emmanuel1976

  emmanuel1976 JF-Expert Member

  #14
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 301
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Mathayo anadhani Musoma ni mali yake? Wana Musoma angewashukuru sana kwa kumchagua mwaka 2005, kutokuchaguliwa kwake si kwamba yeye ni mbaya bali hatoshi katika viatu vya siasa za sasa. Wengi tu walipigwa chini ajue, nia ya wananchi ni kuipiga chini au kujivua gamba hili CCM lililo wang'ang'ania watanzania. Mie nadhani gamba ni CCM yenyewe na halijavuliwa bado, wananchi ndio wenye hatma ya kulivua gamba hili CCM.
   
 15. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Huyu Mathayo ni mpuuzi na uelewa wake mdogo anasaha kirahisi sana . Je anakumbuka alivyo mfanyia yule jamaa wa pride akala pesa zake na baadaye akagombea na kutaka kimfanya jamaa masikini hadi leo beef ni kubwa ? Alitumia pesa za jamaa kujenga maeneo ya musoma hadi polisi posts na kupang rangi majengo na kumzunguka ? Laana ile bado iko .Je anakubuka alicho mfanyia Ibrahim Marwa mshikaji wa JK leo ni Mkuu wa Wilaya ? Ngoma bado .Kila muosha maiti ataoshwa tu .
   
 16. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #16
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Nimecheka sana, yaani wananchi wamekuja kwa hiari yao kusikiliza natumai hapakuwa na motisha ya malori kuwasafirisha; badala ya kusikiliza hoja wanaamua kumzomea. Na hao hao ndo alitegemea wampe kura, hapo alilamba garasha/hadanganywi mtu.
   
 17. emmanuel1976

  emmanuel1976 JF-Expert Member

  #17
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 301
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekumbuka kitu, alihutubia hadi saa 12:15 jioni, na ule msemo wa hakuna aliye juu ya sheria kumbe ni kwa ajili ya wapinzani wa kweli. Mbona tena analindwa na polisi katika kuvunja sheria wakati Mbowe wametumia milioni 50 kumkamata eti hayuko juu ya sheria. Watarudi kwetu 2015 kutuomba kura na watakoma hapo hakuna kuiba wala usanii..si tumeanza kukomaa na kujifunza mambo ya ki-musoma musoma. CCM wana tuvituko bwana.
   
 18. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #18
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,460
  Likes Received: 3,715
  Trophy Points: 280
  alipoona umati wa watu akajua wanashangilia pole Mathayo
   
 19. mtanzaniahai

  mtanzaniahai Member

  #19
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa kinachomtatiza ni shule; hana shule na anataka kutumia vijisenti vyake vya magendo ya mafuta na nyama kuwarubuni wananchi... Wamekushtukia.. hapo ndipo ninapowapendea Wanamusoma.... Ukiwa na malaria sio lazima utumie Chloroquine chungu siku hizi kuna dawa chungu tele... Wacha vijimisemo vyako vya ngumbalo... Halafu huyu jamaa ni msanii as anakaa na hao polisi wanaopenda rushwa kumlinda akiwapa vijembe wananchi??? Nadhani mawe hayakuwa karibu siku hio... lol
   
 20. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #20
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hapo umenena, sijui FaizaFoxy yuko wapi atwambie sheria za Tanzania ni msumeno au ni panga butu
   
Loading...