Mateso yangu

Mateso yangu

Mmmmmh kumbewanamke mzuri lazma awe na macho legev 😂😂😂😂😂
 
MATESO YANGU

SEHEMU YA 003

Yalikua Maneno Yalioupumbaza Moyo Wangu. Nikashikwa na Mzubao na Fadhaa juu yake.. Sauti Yake tamu ikahamaniza katika masikio na Kugota ndani kabisa Ya Moyo Wangu. Nilikuwa nimesikia lakini sikuwa na Uhakika kuwa Alikuwa Akiniambia Miye. Mawazo Yakasafiri Umbali mrefu nikajikuta nikiivuta picha kuwa nipo na Atoto katika Ulimwengu wa Mapenzi na Mahaba, Ulimwingu ambao haukua na BughUdha wala Shida. Mzubao Ulionishika Siwezi kuuleza mkauelewa... Ni kweli Atoto Alikuwa Mzuri, tena Mzuri Kupindukia: Ni kweli kwa mwanaume Yoyote Lijali Angebahatika kukutana na Atoto Hakika Angebaki kinywa Wazi hasa Kutokana na Jinsi Mungu Alivyotulia Katika Kumuumba.

Wakati bado nikiwa kwenye tafakuli Juu ya kauli Ya Atoto, Nikashtuliwa na Sauti yake tamu ikirudia Ile kauli hasa Lile neno la Mwisho.. Ibrah nikatoka kwenye Bumbuwazi Huku nikikubali kuwa ni kweli lile neno Nilikuwa nikiambiwa mimi lakini nitawezaje Kumtafuna Atoto Wakati nimejitolea Kumsaidia? Kusema kweli maswali Yote niliokuwa nikijiuliza Sikua napata Majibu Yake Lakini Mwisho Wake nikaamua Kutulia na Kuyaondoa Mawazo Ambayo Yalikuwa Yakipishana kichwani Mwangu, Nikaamua Kumshika mkono Atoto nakuanza Kuongozana nae kuelekea nilipoiacha Gari:..

Tulipofika nikamfungulia mlango kisha namimi nikapanda ndani ya Gari na Safari Ya Kuelekea Kigamboni Ikaanza. Niliendesha Gari Kwa Umakini Mkubwa Huku kila mmoja akionekana kuwa kimya akiwaza mambo yake. Ukimya Uliendelea Kutawala ndani Ya Gari Huku kuna Wakati Nikishindwa Kujizuia kumtazama Atoto kupitia kwenye kioo Cha Gari Huku Moyoni ni kikili kuwa ni Kweli Mungu Amejua kuumba na Huyu ni Mmoja kati Ya Watu Walioumbwa na Kuthibitisha kuwa Mungu huwa Hakoseagi.

Niliendesha gari Huku ukimya Ukiendelea ndani ya Gari lakini Kuna Wakati nilipokuwa naangalia kando niligundua Kuwa Atoto Alikuwa Akinitizama kwa kiwiziwizi... Katika Akili Yangu na Ufahamu nilionao nikajua kabisa kuwa Atoto Alikuwa Akiniogopa Na Hakuwa Ananiamini... Nikaona Huu ndio muda Muafaka Wa Kumtoa Hofu.. Nikamtupia Jicho la Kiwaziwazi nikakutana na tukio lililoushtua Moyo Wangu, Lilikuwa tukio lililobadili Mapigo Ya Moyo Wangu na Kuanza kuyapeleka Kasi.. Nilijitahidi kuyakwepesha Macho Yangu Lakini Kulikuwa na Ugumu na Ugumu wenyewe Ulinatokana na kile Ambacho Nilikutana nacho Nilipokuwa Namtazama Atoto.

Nikayaacha Macho Yangu Yaangalie Kwa Uhuru Zaidi, Atoto alikuwa Amesinzia Eti Huku Kisiketi Chake Kifupi Cha Shule Kikiwa kimepanda Juu na Kuyaacha Mapaja Yake mazuri yakiwa Wazi kabisa. Kilikuwa Kipindi Kigumu Sana kutokea kwangu hasa katika siku Ile, Ilikuwa ni ngumu Kuvumilia Kile Kilichokuwa Kikifanywa na Atoto, Kila nilipokuwa nikiangalia Ndivyo nae Alipozidi Kuiachia Miguu Yake, Aliiachia Miguu katika Hali Ambayo Ibrah Nikaanza Kupatwa na Hali tofauti, Nikatamani Kuingia Ocean Rd lakini Nilijua Muda Ule ningepambana na Watu Wa Usalama wa Taifa Kwani Mwisho Wa kupita barabara ile Ilikuwa ni Saa kumi na mbili Jioni Hivyo Adhma Yangu Yakumtafuna Atoto Isingetimia. Niliendelea kuutazama Ule Mkao Huku Wakati Mwingine Nikishuhudia Mlinzi Wa Ikulu Akionekana na Kusababisha Mtafaruku Akilini Mwangu... Nikawa naendesha Gari Huku Nikiangalia sehemu Nzuri Ya Kupaki Gari Ili niweze Kupiga Hata Kimoja Cha Ugenini.... Wakati Macho Yangu Yakiwa nje Kuangalia Sehemu Husika Macho Yangu Yakavutiwa na Kitu, Kitu Ambacho Nilikuwa Nikikiona Kupitia Kioo Cha mbele.. Kumbe Atoto Hakuwa Amelala na Hata Kile Ambacho Alikuwa Akikifanya Ilikuwa ni Makusudi ili Kunipima Imani ili kujua kama ni Kweli na Msaidia Au kuna Kingine nakihitaji.

Ingawa Nilikuwa nimegundua Kuwa hakuwa Amelala Lakini Alifanikiwa Kuniingiza Mtegoni Kwa 60%. Na hata Akili Yangu Haikuwa Sawa tena... Nilichokifanya Nikuendesha Gari Mpaka Kigamboni..

Tulivuka Salama na Safari Ya Kuelekea Nyumbani Kwetu Ikaanza.. Kumbuka Muda Wote kila Mmoja Alikuwa Kimya Kabisaa na Hakuna Aliyemuangalia Wala Kumsemesha Mwenzake Wote Tulikuwa Kimya....

JE NINI KITATOKEA BAADA YA KUFIKA NYUMBANI?

TUKUTANE KESHO
 
Kwa style hii bila shaka itakuwa ISIDINGO ya JF...haiwezekani muda wooote huo eti mmeongea neno moja tu,kazi kulia kutazama,kwikwi,macho yake sijui ameumbika,lete story acha mbwembwe nyingi hadi unapoteza utamu wa story.
 
MATESO YANGU


SEHEMU YA 004

ILIPOISHIA.......

Hakuna hata mmoja Aliyefungua Kinywa chake kuongea na mwenzake.

Sasa Endelea,

Nilisimamisha gari mbele ya Geti la Nyumba Yetu nikapiga honi kama mara tatu nikaona Geti likifunguliwa na mdogo wangu. Nikaendesha gari taratibu na kuingiza gari ndani na Baada ya Kuipaki nikashuka nikazunguka Upande wa Kushoto alipokaa Atoto nikamfungulia Mlango Kisha Nikamuomba Ashuke... Ni kweli Alishuka Huku akipandisha vizuri Kisketi chake ambacho kilikuwa kimepanda juu nikaongozana nae kuelekea mlango mkubwa wa kuingilia ndani Huku nikiwa nimemuacha umbali kama wa hatua tatu akitembea kwa kujivuta.. Wakati Nikikaribia Kuufikia mlango Nikashtukia kuuona Mlango unafunguliWa Kisha nikamuona Mama Yangu Mzazi Akitokea.... Mshtuko nilioupata Ilibaki kidogo nipige mweleka.. Sikutegemea mama Kuwa Macho mpaka muda ule, Nilitarajia kumkuta Akiwa Amelala. Mshtuko nilioupata Mimi Ukamshtua hata na Atoto ambaye alibaki amejikunyata Huku akionekana ni Mwenye Aibu Nyingi Sana... Mama Alipotoka Hakuongea kitu bali Alitukaribisha Ndani Huku akionekana Kutokuwa na furaha Kabisa. Lakini hilo Halikunishangaza kwa Kuwa namjua Mama Yangu Tangia Zamani Sana Hakua Anapenda niingie kwenye Uhusiano na Wanafunzi Hivyo Kuniona pale nyumbani tena nikiwa na Mwanafunzi Kulionyesha Kumkera Mama.

Tuliingia ndani Huku Atoto Akionekana ni Mwenye aibu Sana nikamkaribisha Sebuleni lakini kabla Hajakaa Kwenye kiti, Mama Yangu Akamuita Chumbani kwanza.. Kitendo Cha Mama kumuita Atoto ndani Kuliniacha Katika maswali Mengi sana. Nilikuwa nikijiuliza ni Kipi ambacho mama anataka Kumuuliza Atoto? Kwanini Asingesubiri nimuelezee Ilivyokuwa Kuwa... Kwa kweli ibrah nikapoteza furaha, Nikawa mwenye wasiwasi muda Wote Huku nikijua lazima Mama Atakinukisha tu, Lakini Kumbe Haikuwa Hivyo. Muda Ule ule nikamuona Atoto Akitoka Kule Chumbani kwa Mama Akiwa Amebadili Mavazi Yake na Kujitanda Khanga mbili juu na Chini Huku Tabasamu Nadhifu Likichanua Katika Uso Wake. Nikabaki kumtizama Huku nikishangazwa na Lile tabasamu, Tabasamu Ambalo Halikuwepo kule njiani... Moyoni Nikajisemea Huyu Anafurahia kumkuta mama Hapa Nyumbani anajua Ameepukana na Kugegedwa.

Alisogea mpaka nilipokaa Mimi nae Akakaa kwa Pembeni Yangu. Mara nikamuona mama Akitokea Akiwa na Chupa Ambayo tulikuwa tukitumia Kuwekea maziwa... Alikuja na Kutumiminia Maziwa Kisha yeye Akavuta Kitu na Kukaa Karibu Yatu Huku akitutazama Wote kwa Zamu....

Hatukuona Shida ya Kumficha Mama na Wala Sikutaka Kujizungusha.. Kwa vile nilamua Kumsaidia Atoto basi Sikuona Sababu ya Kumficha Mama.. Nikamueleza Mwanzo Mpaka Mwisho kuhusu kukutana kwetu, Kisha nikamueleza ni Ipi ilikuwa Nia Yangu katika Kumsaidia Huko.. Mama Aliniangalia Kwa muda Kisha nikamuona kama Akifikiria kitu baada ya Hapo akamgeukia Atoto na Kumuuliza kama ni Kweli.

Atoto Hakusita kukubali, Alikubali Kuwa ni Kweli... Mama akataka Kujua kitu Gani ambacho Kilisababisha Yeye Kufukuzwa Kwao, na Je kumsaidia kwetu hakutakuwa na Hatari Upande Wetu?

Yalikuwa Maswali Ambayo Sikuwaza hapo mwanzo kama ningemuuliza kutokana na Kujawa na Hamu ya kugegeda kutokana na Vibwanga Alivyonifanyia Atoto tulipokua Njiani.

Atoto Aliangalia Mimi kisha Akamuangalia mama harafu kwa Sauti Yake Ile ile Yenye Utamu Wa Kinanda Akamjibu Mama..

'''''Ukweli wangu ni kwamba ni kweli nilimkosea baba, nasema baba kwasababu Mama Yangu Hayupo hapa Duniani, Mama Yangu Ameshakufa Zamani Sana. Nilikuwa nikimpenda Sana Mama Yangu lakini nadhani Mwenyezi Mungu Alimpenda Zaidi, akamchukua mama Angu na Kuniacha na Baba.... Alipofikia hapo machozi Yalikuwa Yakionekana Machoni Mwake...

''''Aliniacha na Baba ambaye Alinipenda sana tena sana, Alinipenda na kunilea kama Yai, Alinidekekeza na Kunipa kila nilichohitaji. Lakini Licha Ya Kunipenda Huko lakini hakuniruhusu Kuwa Nje Ya Nyumbani Kuanzia Saa Moja Jioni. Ki Ukweli Nilikuwa nikifuata Kila Alichokuwa Akiniambia.. Lakini Hali Hiyo Ilikoma Pale Nilipokutana Na Kijana Aitwaye KABOOM.... ki ukweli Huyo ndiyo aliyenibadilisha na Kunifanya Nisitulie Nyumbani na ndiye Aliyesababisha Mimi kuwa Hapa Mpaka Muda Huu....

JE UNADHANI NINI KILITOKEA?

KWANINI KABOOM ALIMUACHA ATOTO BILA MSAADA? JE KUSAIDIWA KWA ATOTO NDIO MWISHO WA PENZI LAKE NA KABOOM?

Tukutane kesho
 
Kwa style hii bila shaka itakuwa ISIDINGO ya JF...haiwezekani muda wooote huo eti mmeongea neno moja tu,kazi kulia kutazama,kwikwi,macho yake sijui ameumbika,lete story acha mbwembwe nyingi hadi unapoteza utamu wa story.

Mkuu kitu kipo hewani
 
Back
Top Bottom