Mateso yangu

Mateso yangu

ibra87

R I P
Joined
Jul 22, 2015
Posts
5,614
Reaction score
5,379
******MATESO YANGU*******

********SEHEMU YA 001********

Ilikuwa Yapata Majira ya Saa tano na Nusu usiku nikiwa kwenye gari nikitokea maeneo ya Tegeta nikielekea Nyumbani Kigamboni. Ulikuwa ni Usiku wenye mvua kubwa na Upepo mkali sana. Nilikuwa nikiendesha gari kwa uangalifu kutokana na Hali ya hewa kuwa mbaya sana na nilipofikia Maeneo Ya Ubalozi Wa Ufaransa Macho Yangu Yalivutiwa na Kitu ambacho Nilikiona Nje.. Ni kitu ambacho Kilinipumbaza na Kunifanya nisiamini Macho Yangu.. Hakikuwa Kitu kibaya Bali Alikuwa ni Binti Mdogo Mwenye Umri wa Miaka Isiyopungua kumi na minane akiwa Amevalia Sare Za Shule huku amejikunyata na mvua Kubwa ikiwa inaendelea kumnyeshea. Maswali Lukuki Yakajipitisha katika kichwa Changu, Sikuwa Tayari Kukiamini Kile nilichokuwa nakiona.. Kwanini Huyu Mtoto Yuko Hapa? Anafanya Nini hapa Mpaka Muda Huu? Au nichangudoa yupo kazini? Yalikuwa ni Baadhi Ya maswali ambayo Yalipita kichwani mwangu Bila kupata Majibu Sahihi... Niliendelea Kumtizama Yule binti kwa Muda mrefu bila kupata jibu sahihi ya kile ambacho anakifanya pale.

Hakuonekana kama ni Changudoa na Hakuonekana kama ni dada poa, alikuwa ni Binti mzuri na Mwenye uzuri wa Asili... Roho Ya Ubinadamu Ikanivaa, Nikaendesha Gari mpaka Kituoni kabisa Nikaipaki Pembeni Kisha nikashuka nikaelekea Pale Alipokuwa Amejikunyata Yule Msichana. Sikujali Mvua Wala Sikujali kulowa nilichoangalia ni Kujua nini ambacho kinamsumbua Yule Binti... Nilimsogelea Kwa nidhamu na Upole wa hali ya Juu Lakini Kila Nilipokuwa Nikizidi Kusogea ndipo nilipozidi Kushangazwa na Muonekano Wa Yule Binti... Alikuwa ni Mrembo haswa tena mrembo kupindukia, Sura Yake Ndefu ndefu Iliobeba macho Mazuri Ya Kusinzia Iliongeza nakshi nakshi za Uzuri Kwake.... Nilipiga moyo konde nikasogea mpaka pale alipo lakini Uzuri wake Ukanifanya nishindwe kumuuliza chochote nikabaki kuduwaa Huku mvua ikiendelea Kuninyeshea... Niliendelea Kumwangalia Yule Binti bila kumuuliza Chochote Lakini Nikiwa Katika Ule Ukimya Nikashuhudia Machozi Yakimbubujika na Kilichofuatia ni yule binti Kulia Kilio Kikubwa Cha Kwikwi... Kilikuwa Kilio kilichoushtua Moyo Wangu na Kunifanya nipigwe Butwaa.. Roho Ya Huruma Ikaniingia, Nikashindwa Kuvumilia nikainama na Kumshika mabega, alikuwa katika hali ambayo kwa kila mtu mwenye Huruma lazima Angemhurumia Binti Yule. Nikajaribu Kumsemesha lakini Binti Hakuwa anaongea na mimi.. Nikajaribu tena na tena lakini bado haikusaidia kitu binti bado alikuwa Akilia tena kilio kikubwa kabisa. Kufikia Hapo Hata mimi nikahisi Machozi Yakinilengalenga, Nilikuwa nimeguswa na Kilio cha Binti Yule... Muda Mfupi Baadae Ibrah Nilikuwa nikilia, nilikuwa nikilia Pamoja na Yule Binti... Sikujua Kilichokua kikiniliza Lakini Thamani Ya Chozi lile la Binti Yule Lilinifanya na Mimi Nilie.. Nilikuwa nikithamini Sana Machozi Ya Wanawake na Nilikuwa Sipendi Kumuona Mwanamke Akilia Wala Kutoa Chozi.. Nililithamini Chozi La Mwanamke kwa Kuwa kila nilipokua nikimuona Mwanamke Akilia Basi Nilikuwa Nikijihisi Vibaya Sana...

Kitu chenye Ncha Kali kikauchoma Moyo Wangu, nikahisi Fundo likinikaba Kooni..... Macho Yalikuwa Yakiendelea Kunitoka Huku Mvua ikiendelea Kutunyeshea..... Angali nikiwa Nimemuinamia Yule Binti nikamuona Binti Yule Akinyanyua Uso Wake na Kuniangalia, Aliniangalia Kwa Macho yake mazuri ya kulegea, yalikuwa Macho Ambayo kila Mwanaume Lijali Ayaangaliapo, Nilazima Ahisi Utofauti Mkubwa sana ndani Boxer na Ndani Ya Nafsi Yake.

Macho Yake Mazuri Yakanitazama Kwa Muda huku Yakinisanifu na Kuniangalia kwa Aina mbali mbali Za Kutazama, Ibrah Nikahisi Nikikosa Nguvu na Kushindwa kumwangalia Usoni.. Ingawa Ulikuwa ni Usiku lakini Nilishindwa Kutazamana na Binti Yule Kutokana na Uzuri Wa Macho Yake. Binti Aliniangalia kwa muda mrefu sana Kisha Akainama tena Chini na Kuanza Kulia. Nilijikuta Ibrah Nikiwa Kwenye Wakati Mgumu sana. Nikamshika tena, lakini safari Hii nilimshika mkono na Kumuomba Asimame.... Binti Kweli Akasimama; Hapo ndipo niliposhuhudia Uambaji Uliotukuka kutoka Kwa Muumba.

Binti Alikuwa ameumbwa na Kuimbika Mpaka Kupitiliza. Kwa Jinsi Alivyoumbwa Ibrah Nikabaki kutetemeka... Nimewaona Wengi lakini Kwa HuyU Ilikuwa ni Habari Nyingine... Nikamuangalia Kisha Nikamuuliza....

'''Unaitwa Nani???

Akaniangalia kwa Jicho lake legevu kisha Kwa Sauti Ya Kilio Akanijibu

'''''Naitwa Atoto'''!!!!!!

ITAENDELEA KESHO

NB NITATUMIA MAJINA YA BAADHI YA WANAJUKWAA HILI ILI KULETA KITU KILICHO BORA
 
Ekotitee!!!!!!!
Listening good music !!! ibra87 story yako mbaya sana hujui kutunga umeniboa natamani nikupige mbata...
Wadau nataka kujua christian bella yupo wapi nikaserebuka mood ya leo ni kukata mauno tu !!!!
 
Last edited by a moderator:
Ekotitee!!!!!!!
Listening good music !!! ibra87 story yako mbaya sana hujui kutunga umeniboa natamani nikupige mbata...
Wadau nataka kujua christian bella yupo wapi nikaserebuka mood ya leo ni kukata mauno tu !!!!

Umaarufu utafute kwenye jukwaa la Watu maarufu.. Nashukuru kwa comment yako
 
Last edited by a moderator:
Umaarufu utafute kwenye jukwaa la Watu maarufu.. Nashukuru kwa comment yako

Yoooooo amu long time kitambo na nitazidi kuwepo!!!!!
Inaonesha we ni kinjuka!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Yoooooo amu long time kitambo na nitazidi kuwepo!!!!!
Inaonesha we ni kinjuka!!!!!

hahahaha!!!!! Sinunuagi bhana jaribu kwingine
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom