Mateso wanayopata wananchi wanaoishi kando kando ya shamba la mifugo la Utegi

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
388
773
Shamba la mifugo la Utegi kisheria ni shamba la vijiji vinavyoizunguka shamba hilo na walipewa na Serikali baada ya kuilipa Serikali jumla ya Tshs.90,000,000 (millioni tisini). Na kama nasema uongo, naomba kusahihishwa.

Awamu ya Tano ilipoingia madarakani, iliichukua shamba hili bila kukaa na wananchi na kuwaeleza sababu ya kuchukua shamba hilo. Kama ni kushindwa kuliendeleza, kwa nini wananchi hawakuelezwa? Kama kulichukua, basi kuna taratibu zingefuatwa.

Hili halikufuatwa, tuliona tu wanaletwa walinzi wa shamba na ng'ombe kadhaa na majumba kuanza kukarabatiwa na ubabe uliokithiri. Pamoja na kuwa shamba bado ni la wananchi, haturuhusiwi mifugo yetu kukanyaga hata nchi moja ndani ya shamba, na hata kuchunga mifugo yetu ndani ya shamba hilo ni marufuku.

Mifugo inapoingia ndani ya shamba hilo ambalo ni letu kwa ubabe wa walinzi, mifugo inakamatwa na kila ng'ombe anatozwa Tshs.30,000 kama faini, na hakuna risiti ya control number na fedha wanaweka mifukoni mwao.

Tunakueleza Waziri wa Mifugo, suala hili ulifuatilie, na hatukubali uonevu wa namna hii, ukijua kuwa shamba hili ni la wananchi wa vijiji vinavyozunguka shamba hili. Mhe. Waziri, tusipopata muafaka, shauri hili tutalipeleka mahakamani na tujue hatma ya shamba letu.
 
Wananchi walitoa wapi hizo pesa kwa utaratibu gani kuchanga kiasi hicho?
 
Back
Top Bottom