Mategemeo yangu 2010

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
MATEGEMEO YANGU 2010

Kwa miaka michache iliyopita kampuni nyingi za habari Tanzania zilianzisha tovuti zao ili habari zao mbalimbali ziwe zinaingizwa katika tovuti hizo watu wasome lakini ikaja kuonekana kwamba watu wengi sasa wanakimbilia kutoka habari kwenye tovuti hawanunui magazeti kwa wingi kama zamani kwa sasa baadhi ya vyombo vinaweka habari kidogo sana au kwa ufupi au wanaweka habari baada ya masaa au siku kadhaa ili kulinda maslahi ya magazeti yao .

Nategemea mwaka kesho kampuni hizi zitaweza kuwekeza pesa zaidi katika masuala yao ya Tovuti na mawasiliano ili wapate tovuti ambazo watu watakuwa wanajisajili kwa ajili ya kupokea habari na kusoma ila kwa njia ya kulipia kama zilivyo kwa baadhi ya sehemu , wakiwa na tovuti zenye mfumo mzuri kama kawaida zitatembelewa na watu wengi zaidi pia watapata matangazo ya kuweka kwenye tovuti hizo ambayo inaweza kuwa ni pesa nyingi hata zaidi ya kuuza magazeti .

……….

Kuja kwa mkonga wa mawasiliano baharini kulipokelewa kwa shangwe sana na baadhi ya wadau wa sekta za mawasiliano hata wale ambao wanataka kuingia kwenye sekta hiyo huko mbeleni sasa wamepata kitu fulani cha kuongelea .

Mkonga uliingia bila kujiandaa vya kutosha pamoja na majadiliano ya wazi kati ya wadau wa sekta mbalimbali badala yake ni watu Fulani tu walijadili na kuafikiana masuala ya kitaifa hichi ni kitu ambacho kinapigwa vita sana sehemu mbalimbali

Ndio umetua kwa sasa unafanya kazi hongereni kwa hilo lakini nategemea kuanzia mwaka kesho kuwe na mijadala ya kina ambayo itashirikisha watu wa sekta mbalimbali kabla ya kuamua kupitisha vitu vikubwa kwa taifa sio kushtukizwa .

Kwa sasa hatuna sheria Maalumu za masuala ya Mitandao wala nchi haijafikiria kuchukua sheria zozote za sehemu zingine ziwe kama mfano kwake manake sisi ni wanachama wa jumuiya ya madola , sadc kuna nchi kwenye jumuiya hizi zina sheria hizo kwanini inashindikana kuwasiliana nao kuona jinsi inavyoweza kufanyika .

Kukosekana kwa sheria hizo kunaweza kusababisha hawalifu kuweka vituo vyao nchini kwa ajili ya kushambulia sehemu zingine au kutumia mitandao ya nchini kwa shuguli hizo hizo pia wimbi la utumiaji wa programu bandia nao limeongezeka sana na hakuna anayejali .

Naamini mwaka kesho tutaweza kuwa hata na sheria ndogo za mitandao kuweza kudhibiti hali hii nchi yetu isiwe mbingu ya uhalifu wa mitandao siku moja au hata kutajwa tu .
……
Kwa muda mrefu pia baadhi ya kampuni za mawasiliano zimekuwa na mtindo wa kuficha baadhi ya taarifa za wateja wao hata kama ni haki kwa mteja huyo kutaka taarifa hiyo .

Mfano unaweza kupigiwa simu ambayo ni private ukaenda kwenye kampuni husika kuomba taarifa ile unaweza kulazimika kula kiapo kwa kusaini karatasi maalumu .

Au wale wateja wanaotumia vifaa vya kampuni Fulani ya mawasiliano ya internet wanapofanya kitu kibaya kutumia vifaa hivyo na ukaweza kupata anuani zao ukifika kwenye kampuni hizo utaambiwa hawana utamaduni wa kuhifadhi taarifa hizo .

Naamini kuanzia mwaka kesho kampuni hizi zitakuwa na taarifa zote muhimu na za kweli kuhusu wateja wanaowahudumia pamoja na vifaa wanavyoviuza kwa wateja wao wanapotumia huduma zao , pia mteja akiwa anataka taarifa hizo hata kama anataka kuhakiki taarifa zake apewe uhuru wa kubadilisha au kuondoa kitu Fulani kama kuna mabadiliko yoyote kwenye taarifa hizo .

……
Kwa muda pia baadhi ya taasisi za serikali zimekuwa hazina sera za masuala ya ICT au zile ambazo ziko basi zinasimamiwa na watu ambao sio wahusika kwenye suala la ICT hawafanyi kazi kwenye sekta hiyo au wahusika ambao hawana uwezo wa kuweza kufanya shuguli hiyo .

Hii imetokana na kwamba hatuna chombo kinachojulikana rasmi ambacho kinaweza kutoa sera hizo kuhakikisha zinasimamiwa ipasavyo na matunda yake yaonekane , naamini kuanzia mwaka kesho basi kile kitengo kilichopo chini ya wizara ya sayansi na technologia , taasisi ya sayansi na technologia pamoja na mamlaka ya mawasiliano Tanzania wataweza kuja kwa pamoja kuanzisha chombo kingine ambacho kitakuwa huru katika suala hili .

……..
Na vituo vingi vya masuala ya ICT vimeonekana kuzorota kwa mwaka huu sana au kupotea kabisa kama kile cha lugoba Napendelea serikali kupitia wizara husika iwe inafuatilia vituo hivyo kujua vinavyoendelea pamoja na kupata ripoti za kila baada ya miezi kadhaa itasaidia sana kujua nini kinavisibu .

Pia vituo viwezeshwe kwa njia ya fedha na wataalamu wa fani husika katika tafiti na uundaji kwa kushirikiana na vyuo vingine nchini kwenye idara zao za technologia

Hayo ni mategemeo yangu kwa mwaka kesho naamini kuna mengine yameanza kufanyiwa kazi kwa utekelezaji .

Pamoja tutaweza
 
Back
Top Bottom