Habari za mida ndugu wadau wa maendeleo, mazingira, ma siasa, ma teknohama, mahusiano na mapenzi.
Huwa najiuliza sana kuhusu wapigaji picha hapa nchini. Ni kwamba hawana camera za ukweli ama lenzi zao ni za kichina ama ni kwa nini ni lazima wajichomeke katikati ya tukio mbele ya uso wa mtu ndio wachukue picha?
Ukienda nchi za watu utakuta mzungumzaji/ msanii/ mwanasiasa etc. anaongea labda kwenye uwanja wa wazi na picha zinapigwa kutokea maili moja across, huoni mtu aliyemkalia usoni kumpiga picha.
Hapa kwetu hata ukienda kwenda kiukumbi kidogo cha kanisa kwa mfano, kukiwa na tukio kama harusi basi hata mchungaji humuoni wala hao wanandoa huwaoni kwa sababu wanazibwa na msururu wa wapiga picha pale mbele, kitu ambacho kinawapa priority watakaoangalia hizo picha baadae - kama zitaangaliwa anyway - kuliko sisi tulioko eneo la tukio kuwezesha ifanikiwe.
Tatizo hapa kwetu ni nini? Vyombo ni vy Kichina au wana matatizo gani?