Matatizo ya Tanzania na mapendekezo ya wana JamiiForums

DrWHO umenena kilimo ni jambo la msingi sana juu ya hapo ni elimu, nchi nyingi za kiafria hatuna kilekitu wazungu wanaita 'country comparative advantage' kukosekana kwa vipaumbele kunasababisha tukose mwelekeo.

Kilimo
Kima tutaweka mkazo kwenye kilimo cha kisasa kwa kuwapa ruzuku wakulima wadodogo, kwa hili tutafika mbali ' wakulima wakubwa si muarubaini bali ni matatizo' kama wawekezaji serikali inawapa ruzuku 'msamaha wa kodi' kwanini wakulima wetu wasipewe.

soko la mazao ni kubwa sana ndani na nje ya nchi, ila hapa umakini unahitajika, hawa madalali wa kiindi lazima wamulikwe wasiendelee kunyonya wakulima uandalia utaratibu mzuri wa soko la mazao.

ni mara ngapi mmesikia wakuu wa mikoa wakipiga marufuku uuzwaji wa chakula nchi za jirani, soko ni kubwa sana ndugu zangu tutie shime, kwa hili zitatengenezwa ajira nyingi vijijini na wimbi la wazururaji mijini litapungua.

Elimu
Nchi ikiwekeza kwenye elimu matunda yake ni dhari, kwa sasa masoko ya ajira duniani yamuanza kufunguliwa kwa wale wenye elimu, kama nchi itasomesha watu wake, itakuwa ni rahisi kwa nchi kukusanya mitaji na itapelekea utehgemezi wa nje upungue, mfano tunaambiwa waandisi wa tanzania wasoko sana kusini mwa afrika, nchi ya Botswana ikiwa mfano, kwanini wasisomeshwe waandisi wengi zaidi na taaluma nyingine wakafanye kazi nje ya nchi na watakao baki waendeleze taifa, hawa jamaa wataleta pesa nyingi sana nchini.

Nawauliza wanaforum 'what should be tanzania copmarative advantage'
 
Kwa mambo yoye wanayofanya tusije tukaiga kutengeneza counterfeit drugs, counterfeit spare parts (even aircraft spares!!), software piracy, counterfeit electrical appliances, counterfeit everything.... Mnakumbuka ile documentary ya BBC kuhusu matumizi ya fake drugs from India ambayo zilileta kizaazaaa Nigeria??



hiyo ya kutengeneza generic drugs na kuwa na viwanda vingi haina maana kama serikali haiwezi kuwalisha watu wake

kwanza tuwe na chakula na akiba ya kutosha then tuanze kuwa wajeuri katika negotiating table na jamaa wa WORLD BANK na vile vile tusiwe wajinga wa kupaamia tuuu kila Bilateral agreement tunayoletewa ama sivyo yatatukuta kama haya ya rada


inahitajika kuiga mfano wa Malaysia na Vietna katika kilimo kisha tuone kama hatutofika
 
Kichuguu

Swali zito mzee ngoja tutafute data pamoja na yale ya general knowledge.
 
kwa niaba ya blogu ya MAGGID aliwahi kukutana na huyu mzee...sasa imagine tungekuwa na kilimo cha sayansi tungekuwa wapi?

mhando.jpg
 
KICHUGUU

Kwa kifupi tu nataka kuweka baadhi ya mambo ambayo yanaweza kuwa sio wazi kwa haraka haraka tu. Tuendeleze mjadala

Japan na Korea – Washiriki wakubwa wa USA kutokana na chokochoko ya vita na North Korea ya Kim Jong hivyo makampuni mengi makubwa yaliweza kufanya investment bila kuulizwa maswali na kufuata cheap labour. Japan inaendelea kutesa katika nyanja hii kutokana na kuweza kufanya kazi kwa bidii na kukumbatia technology ya nchi za magharibi ambazo ni wawekezaji wa hali ya juu.

Mpaka sasa USA wameweza kuendelea kutoa upendeleo wa wazi wazi kwa wajapan kwa kutengeneza machine mabalimbali ili wasiweze kuleta chokochoko tena kama ilivyokuwa kwenye vita kuu ya dunia wakati waliangushiwa bomu la Horoshima. Ili kuweza kuweka balance katika Asia wamarekani vilevile waliweza kuanza kutafuta washiriki wengine huko Asia na kupata kwa kiwango kikubwa ushiriki wa nchi za Singapore na Taiwan ambayo mpaka leo wana matatizo na China kwani wachina wanadai ni kati ya taifa lake (still pending) Hivyo utaona misaada mingi ya uwekezaji ilifanikiwa kwa sababu za kisiasa na security ya nchi hizi kuwa katika wasiwasi na cold war.

Ni sawa vilevile kwa nchi kama Kenya ambayo imekuwa ikipewa misaada na UK pamoja na USA kutokana na hofu ya hizi nchi za magharibi kwamba Tanzania ambayo ilikuwa inafuata siasa za ujamaa kuwekwa mkumbo mmoja na nchi za Urusi na China. Ndio sababu kubwa ambayo iliifanya Kenya kutotoa msaada wowote bayana kwa nchi za kusini mwa Afrika katika ukombozi n.k. Kulifika kipindi nchi za magharibi kuzifanya nchi majirani kuwa maadui mtakumbuka vizuri zaidi wakati mpaka kati ya Kenya na Tanzania ulipofungwa na Nyerere (R.I.P.) kutokana na kuvunjika kwa jumuiya ya Afrika Mashariki na Tanzania iliendelea kupigwa vita hivi wazi wazi kutokana na msimamo wake wa kuwasaidia wenzetu wa kusini ili wajitawale gharama yake ni kubwa ambayo ku-quantify ni vigumu. Hadi leo hii habari za Tanzania ukisoma kwenye vyombo vya habari vya UK, USA ni kuhusu jambo ambalo sio muhimu sana kwa maendeleo ya Tanzania. Utaweza kuliona hili kwa kulinganisha nchi za Kenya, Zimbabwe na south Afrika kutokana na heavy investment za mataifa haya kwenye nchi hizo.

India imeweza kutumia raia wake ambao wengi walikwenda nje ya nchi kwa ajili ya ajira na sasa wengi wanarudisha mali nyumbani kwao. Matajiri wengi wa kihindi wamejikusanya na kuweza kuweka investment kule walikotoka. (Angalia kampuni za chuma kama vile Corus ambao wamenunuliwa na matajiri wa India ambao wamesoma ulaya n.k. sasa hivi chuma kinatawaliwa na Indian Co.) Mfano miaka ya nyuma kabla India haijapata uhuru waingereza walijenga vyuo mahsusi vya kuwafundisha madaktari wa India ili wapunguze shortage waliyokuwa nayo hivyo waliweza kuweka kiasi cha wanafunzi madaktari kutoka India na kwenda UK kufanya kazi, walipata matatizo mwanzo lakini baada ya miaka 50 na ushee matunda yanaanza kujitokeza wengi wao ni matajiri na wanainvest nyumbani kwao. Hivi leo vyuo vya India vinatoa wanafunzi wanaofanya technologia ya computers ambao wanatakiwa worldwide na hawa ndio wasomi wanaoendesha gurudumu hili la maendeleo kule kwao. Sisi bongo wameamua watoto wa masikini wasisome bali watoto wa viongozi ndio wasome kwenye vyuo vya nje na kulipiwa na walipa kodi ambao wengi wao hufeli na hawana maendeleo yoyote bali kutumia mali ya walipa kodi.

Uingereza wakati walikuwa (masikini wa kutupwa) uchumi wao ulikuwa na matatizo katika miaka ya 1980 walipewa billion 100 ili wajikwamue kwenye uchumi wao, sisi Afrika ni nchi gani ambayo ilipewa hata mara moja 10% ya hizo pesa? Lakini tusisahau vilevile kwamba IMF na World Bank zilianzishwa kukidhi maslahi ya nchi za magharibi hivyo misaada ambayo kila siku wanaipigia kelele kutusaidia ni kiini macho kwani ni kwa ajili ya kuwakwamua wao na sisi tuendelee kuwategemea wao. Kwa kuwaona ni bora zaidi. Kitu cha kusikitisha ni viongozi wa kiafrika ambao kila waambiwalo na nchi za magharibi ni zuri la kulifuata bila kuhoji kama lina maslahi kwa nchi zetu. Ulimbukeni wa kuwadharau wasomi wetu ambao nchi za magharibi zinawatumia katika nyanja mbalimbali kwa maslahi yao.

China – walikuwa wanatengeneza kila kitu feki miaka hiyo ya 1960’s lakini sasa hivi wameweza kuperfect huduma zao kutokana na investment ambayo inaongozwa na Hong Kong ambayo ilikuwa chini ya UK (kwa muda wa miaka 100 ambayo ilikwisha 1996), wamekumbatia technology kutoka nchi za magharibi na cheap labour ambayo inawasaidia, pamoja wameweza kufungua Shengzen ambayo inasaidia kuuza bidhaa mbalimbali nafuu kokote ulimwenguni kutokana na investment za makampuni ya nchi za mgharibi. Vilevile kila nchi ambayo ukienda utakuta kuna china town hawa ndio baada ya miaka kadhaa wanainvest China na kuuza kwa wingi bidhaa zao. Call centres zinapelekwa India hivi sasa kutoka UK kutokana na wahindi kutawala sehemu nyingi za maamuzi (Board of directors) wasomi wengi ni wahindi, sisi Afrika kazi kuwazuia raia wetu kwenda nchi za nje – angalia Balozi za UK na USA jinsi wanavyoweka vikwazo kwa wananchi wanapotaka kwenda kwenye nchi zao.

Kwa bahati nzuri nimefanya kazi na wahindi wengi hapa UK walio-forge vyeti na wengine walio kwenda shule za maana lakini wanabebana sana, hata wazungu wanawafahamu lakini wanawakubali, lakini ukiwa mswahili hawakubali kwa sababu wanawafahamu wahindi kama ma-daktari wao au nanny wao wakati bado wadogo kwa hiyo nyie waswahili mmeanza kuja huku ulaya juzi juzi tu ni lazima msikubalike kwa wakati huu lakini hapo baadaye litakuwa jambo la kawaida kwa sababu waafrika wengi hasa kutoka Nigeria, Senegal, Ghana, Zimbabwe, Somalia na nchi zingine wanaingia kwa wingi na kazi wanazozifanya wengi ambao kisomo chao ni kidogo pamoja na wanafunzi kutoka Afrika watabadilisha mwelekeo wa hawa wazungu baada ya miaka kadhaa.

Afrika tuna cheap labour lakini hakuna makampuni makubwa ambayo yanataka kwa uwazi kupeleka call centres na kazi nyingine kwa sababu hatua god-father. Jamaicanas waliletwa UK kufanya kazi za nyumbani kwa wazungu lakini tatizo lao hawakutaka kwenda shule hivyo wamebaki nyuma sana wengi wao. Wahindi wengi ni wasomi ukiondoa wale ambao ni jadi yao ambayo ni biashara hawakubali watoto wao kwenda vyuo vikuu na wamekomalia biashara. KITU KINGINE KIKUBWA WACHINA NA INDIA WANALETA VIJANA WAO WENGI SANA KUSOMA HAPA UK AMBAKO NI CHEMCHEM YA EDUCATION (KWENYE VYUO VIKUU). KWA HESABU YA HARAKA HARAKA TU KILA CHUO HAPA HUTAKOSA WAHINDI NA WACHINA AT LEAST 60% KWENYE KILA FANI; SASA HAWA BAADA YA MIAKA KADHAA UTAONA TOFAUTI NA SISI. ELIMU NI MSINGI WA MAISHA BORA
Tanzania tuna nafasi kubwa sana ya kuwa Giant within 20 years kama Wizi na rushwa itaondolewa na kutumia raslimali zetu vizuri i.e. tuna kila kitu mafuta ndio hayo tena, madini, ardhi, pamoja na watu ambao itabidi kuwasomesha vizuri na kuweka mikakati ya kuweza kuilinda nchi yetu na wageni ambao wengi wana nia ya kutuvuruga. Mfano ni Nigeria nchi yenye mafuta na tajiri lakini kila siku wana matatizo wenyewe kwa wenyewe. Ni jukumu la serikali kufanya kila jitihada kuwarudisha wasomi wa kitanzania kutoka nje na kuja nyumbani kufufua mfumo wetu na kuondoa wageni uchwara ambao wanakuja kujifunza kazi kwetu. Unakuta anaajiriwa mtu ambaye ana degree moja halafu mnamwita ati ni mtaalamu aliyebobea kwa pesa ya walipa kodi na kumwacha kijana wa Tanzania mwenye miaka kadhaa kwenye fani yake na muelewa wa mazingara.

TUBADILIKE JAMANI! KAMA TUNGEWEZA KUWEKA BAJETI YA KUWASOMESHA WATANZANIA KWENYE VYUO VYA UK KWA MIAKA 20 MFULULIZO NA KILA MWAKA AT LEAST WAJE 1000 HATA KAMA WENGINE HAWATARUDI NYUMBANI TUNAWEZA KUBADILI MWELEKEO NA KUINUA NCHI YETU.

(Nimejaribu kidogo na wengine kazi kwenu)
 
Hii ni mada ya kufikirisha na si rahisi kuijadili na kuimaliza (exhaustively). Nami nichangie kidogo, kwani haba na haba hujaza kibaba!

Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa wenzetu. Nitataja baadhi ya mambo yaliyowasaidia kufika hapo, ambayo sisi tumeyakosa au kuyapuuzia. Nikiri kuwa baadhi ya masuala haya yanaingiliana na huenda huwezi kupata moja bila jingine

1. ELIMU
Wenzetu hawa wamejitahidi kusomesha watu wengi ndani ya nchi yao na duniani kote tena katika fani nyingi iwezekanavyo, zote za asili (mfano tiba-acupuncture) na za kisasa/Kimagharibi (Generic ARVs).

Wamepeleka watu wao Marekani na Uingereza hata kuiba teknolojia fulani, ambazo huzipeleka nchini kwao na kuzitumia kuundia vitu vinavyofanana na/au kunakili/kughushi vitu vya wagunduzi halisi (piracy).

Kwa hiyo licha ya elimu kuwa "suala la mtu binafsi", serikali zimekuwa zinawasaidia watu wao au asasi za elimu za watu binafsi ili kuwawezesha watu wao wengi kupata elimu na kwa asasi hizo pia faida. Nimewahi kuambiwa kuwa hicho chuo kikuu cha tiba hapo Mbezi (IMTU) ni cha watu binafsi lakini serikali ya India imekuwa ikikisaidia kwa namna moja au nyingine ili "kiwekeze" hapa Tanzania. Kwa hiyo wahitimu wa hapo, ambao wengi wao ni Wahindi, wakitoka hapo ndiyo hao wanaajiriwa Hindu Mandal na Aga Khan. Na hata sasa Muhimbili (MUCHS) Wahindi (wanafunzi wa udaktari) wameongezeka kwa vile kwao gharama za kusomea Tanzania ni nafuu. Nao wakimaliza ndiyo hivyo Aga Khan na Hindu Mandal zinawasubiri. Tusipoangalia hata hapo Temeke watakuja wao maana sisi watoto wetu wazawa hatuna uwezo wa kuwalipia 40%.


Wachina nao wana mkakati maalum ambapo wamepeleka watu wao nchi za Magharibi kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo uchumi wa kibepari na teknoloji mbalimbali. Watu hawa hurudi nyumbani na kusaidiwa na serikali kufungua makampuni yao binafsi. Huo ndiyo uwezeshaji wa kweli ambao sisi tunaupigia hekaya!

2. UTAMADUNI
Utamaduni una nafasi kubwa sana katika maendeleo ya jamii. Nadhani utamaduni wao, inapokuja katika maslahi ya umma/jamii, hawana unafiki. Sisi tuna mambo ya kuoneana haya, hatuambiani ukweli "mwenzetu" anapoharibu. Hata ukiangalia vyombo vya habari vya India ni wakali kweli kweli. Ndiyo maana pia wanasifika kwa Investigative Journalism.

Pia hawaonei haya, na hakika wanajivunia utamaduni wao, wanapokuwa nje ya mataifa yao. Si wepesi wa kuiga mambo ili waonekane "wajanja" au "si washamba". Nadhani uhafidhina huu unawasaidia. Angalia mavazi yao, vyakula vyao. Wamejitahidi. Binafsi naona Wamasai hapa kwetu wana "elements" kama hizi za uhafidhina. Kama mtu amewafuatilia Wamasai (iwe Ngorongoro au Loliondo) atajua jinsi walivyo wakali inapokuja kwenye maslahi yao kama jamii. Wako mbele sana kujua na kudai haki zao. Kwa ujumla wetu Watanzania tu wepesi wa kuiga na mara nyingi kupenda ukuu, ufahari, ubosi. Tofauti kabisa na Waasia hao. Angalia viongozi wetu ukiwaita NDUGU wanasema umewadhalilisha! Wanataka UHESHIMIWA! Angalia nguo wanazovaa bungeni au hapa Dar wakati kuna joto kali! Misuti ya Kimagharibi.

Tuje kwenye lugha. Fahari yetu iko wapi kwenye lugha? Mzungu hata akiolewa na Mswahili lazima atajitahidi mwanae azungumze kikwao (iwe Kijerumani au Kifini). Watanzania walioko Ulaya (siku hizi hata hapa Bongo watoto wanaosoma "ACADEMY") sana sana watazungumza na watoto wao kwa Kiingereza. Vyakula navyo ndiyo hivyo: twapenda kushabikia "vyakula vya Kizungu". Haya mambo yanaweza kuonekana madogo na labda si ya msingi lakini yanatuelezea sisi kama taifa tu watu wa namna gani. Yanahusiana na suala lingine muhimu, UZALENDO.

3.UZALENDO
Wenzetu wana uzalendo sana. Wakati mwingine uzalendo huu unapitiliza na unajitokeza kwa sura ya ubaguzi wa rangi nk. Haya yako kwenye ajira na huduma nyingine za umma. Wenzetu hata wakiiba wanajenga kwao. Sisi tunajenga Ulaya (Geneva ndiyo maarufu). Ukitaka kujua uzalendo huu ambao nauzungumzia angalia hapa kwetu ambapo baadhi ya makabila kama Wachagga na Wahaya ambao wanasemekana kuwa wakabila: wakipata mali mjini (maana pia ni watafutaji) huenda kujenga kwao kwenye vihamba nk kijijini kwao.

4.UJASIRIAMALI
Kwa vile maendeleo haya tunayojaribu kuyaangalia yanaangukia pia kwenye uchumi kuna suala la Ujasiriamali. Wenzetu hawa wa Asia (kama Wachagga na Wahaya) wanajituma sana. Tunawaona Mtaa wa Kongo wakiuza vitambaa na maua na ashkrimu (ice cream) na ubuyu. Si ajabu baadhi yetu tunawadharau. Lakini wao wanatafuta pesa. Na wanafanikiwa. Sifa hii ya mtu mmoja mmoja na jitihada kama hizi ukizitafsiri kwa taifa utaona ni hatua gani inaweza kuwa imepigwa.

"SIDO" wao waliijua zamani (cottage industry). Wameanza kidogo kidogo na hatimaye wengine wamefikia kuwa na viwanda vikubwa. Wenzetu wanawezesha wajasiriamali wao na wauzaji nje na kuwapa ruzuku sisi tunawakatisha tamaa! Na sisi kwa kukosa uzalendo na utamaduni wa kutothamini vyetu tunapapatikia vya nje. Nani atanunua bidhaa zetu? Matokeo yake viwanda vyetu haviuzi (of course, kuna sababu nyingi za kushindwa viwanda vyetu-gharama za uzalishaji, teknolojia duni, umeme, wenzetu kupewa ruzuku, nk). Sijui "BUY TANZANIAN" iliishia wapi! Tuna sera kibao, iwe SME, Viwanda, Vijana, Mifugo, Madini (nasikia Tanzania inaongoza Afrika kwa kuwa na sera katika sekta nyingi ) lakini hamna kitu!


5. TEKNOHAMA (IT)
Kwenye IT au ICT wenzetu waliwekeza vilivyo. Na katika zama hizi za utandawazi hilo ni eneo muhimu. China sasa hivi ndiyo wamezidi kuja juu kwenye IT na mambo ya kompyuta mpaka jamaa wa magharibi wanababaika.

6. RUSHWA YENYE UTU
Wenzetu hao wanakula rushwa yenye utu. Nakumbuka Mwalimu aliwahi kusema kuwa tofauti ya mkandarasi wa Tanzania na India ni kuwa atakula pesa na daraja atajenga lakini yule wa Tanzania atakula pesa na daraja hatajenga (sana sana atanunua gari la kifahari na kuongeza nyumba ndogo!)

Ngoja nipumzike...tuendelee kuchangia...
 
Sijui kama hili limewahi kujadiliwa humu maana mimi memba mpya! Kama limewahi basi naomba nipewe LINK

Kutokana na kuona upeo mkubwa wa kuelewa mambo wa wana JF na pia kuona nia njema waliyonayo kwa nchi yetu basi nimeshawishika kuanzisha mjadala huu. John Mnyika amefanikiwa kunirudishia imani, hapo kidogo, kwamba Tanzania yenye neema inawezekana kwa kusema kwamba, katika nchi nchi, pale ambapo watu walikuwa wameshakata tamaa, kundi dogo la watu lilikuja na kuwakomboa.

Basi naomba, wana JF, badala ya kila siku kunyooshea vidole watu, na viongozi wetu, tujadiliane hapa kwa hoja. Ni Tanzania ya namna gani tunaitaka? Kila mtu anaweza kuwana mawazo yake na kwa pamoja tunaweza kujikuta tunapata kitu kimoja ambacho kinaweza kutupa dira ya mwelekeo ambao taifa hili linatakiwa kuufuata!

Historia inaonyesha karibu nchi zote zilizoendelea, na zinazoendelea kwa kasi sasa hivi kama Indonesia na China zimefanya kitu kama hiki! Kutengeneza falsafa ya mwelekeo wa taifa...Nami napendekeza tuuite Tanzania Tunayoitaka!

Karibuni!
 
hoja ni nzuri,
bila ya kuzunguka zunguka, nianze kuelezea ninachokitaka kwa tanzania yetu
MAHITAJI YA MSINGI
1.TUNAKA MAKAZI BORA
2.HUDUMA BORA ZA MAJI SAFI NA SALAMA
3.HUDUMA BORA ZA AFYA
4.UMEME WA UHAKIKA
5.AJIRA ZA UHAKIKA

MAHITAJI MUHIMU
1.TUNAHITAJI HUDUMA ZA USAFIRI AMBAZO NI ZA UHAKIKA NA SALAMA, TUNAHITAJI KUONA BARABARA ZOTE TANZANIA ZINAPITIKA KWA KIPINDI CHOTE CHA MWAKA,KWA LUGHA NYINGINE TUNAHITAJI KUONA KUNA BARABARA KUBWA ZA LAMI ZINAUNGANISHA KILA MKOA NA WILAYA NA MPAKA VIJIJINI
TUNATAKA KUONA USAFIRI WA TRENI UNAFIKA KILA MKOA TANZANIA NA TUNAHITAJI KILA MKOA PIA UWE NA KIWANJA KIKUBWA CHA NDEGE

UCHUMI
TUNAHITAJI KUWA NA VIWANDA VINGI VYENYE UWEZO WA KUZALISHA BIDHAA MBALIMBALI ;
MFANO VIWANDA VYA NGUO,VIWANDA VYA KUTENGEZA NA SUSINDIKA VYAKULA,NA IKIWEZEKANA HATA VIWANDA VYA KUTENGENEZA MOTOKAA

MAKAMPUNI
TUNAHITAJI KUONA MAKAMPUNI YETU KAMA AIR TANZANIA LIKIFANYA KAZI KWA UHAKIKA, LIKIFANYA SAFARI NDANI YA TANZANIA, AFRIKA NA HATA NJE YA AFRIKA

TUNAHITAJI KUONA SHIRIKA LA RELI LIKITOA HUDUMA TANZANIA NZIMA NA HATA NJE YA TANZANIA

TUNAHITAJI KUONA USAFIRI WA UHAKIKA ,SALAMA NA HARAKA KWA MIJI YOTE YA TANZANIA NA HASAHASA MIJI MIKUBWA KAMA DAR ES SALAAM
KILIMO
TUNAHITAJI KUWA NA KILIMO CHA UHAKIKA.
KATIKA MAZAO YA BIASHARA NA MAZAO YA CHAKULA
TUNATAKA TUWE NA UWEZO WA KUZALISHA CHAKULA CHA WINGI NA KUUZA NJE YA NCHI NA KINGINE KUWASAIDIA WENZETU WAKIKUMBWA NA JANGA LA NJAA:

ELIMU
TUNAHITAJI KUWA NA VYUO VIKUU VINGI KARIBU KILA MKOA
TUNAHITAJI KUWA NA SHULE BORA NA ZA KISASA KUANZIA SHULE YA MSINGI NA SEKONDARI
TUNAHITAJI VYUO VYA UFUNDI, VYUO VYA KILIMO NA VYUO VYA SANAA,
TUNAHITAJI KUONA KARIBU ASILIMIA 80 YA WATANZANIA WOTE NI WATU WALIOELIMIKA NA WANAWEZA KUFANYA UPEMBUZI YAKINIFU

MICHEZO
TUNAHITAJI KUONA TANZANIA IKISHIRIKI KATIKA MASHIDNANO MAKUBWA KAMA VILE KOMBE LA DUNIA NK

HAKIKA YAPO MENGI TUNAYOTAKA KUONA KWA TAIFA LETU HILI NA MPAKA SASA SIJAONA HATA KIMOJA!
 
Masaki,

Kinachotakiwa ni uongozi bora na bila ya hilo hata tufanye nini, tutakuwa tunacheza tu. Uongozi bora sio lazima uwe wa demokrasia, hata ukiwa
uongozi kama wa Mwalimu enzi zake lakini uwe ule unaojali maslahi ya watu wake.
 
Quarz

TUNATAKA KUONA USAFIRI WA TRENI
UNAFIKA KILA MKOA TANZANIA NA TUNAHITAJI KILA MKOA PIA UWE NA KIWANJA KIKUBWA CHA NDEGE

VIWANDA VYA KUTENGENEZA MOTOKAA

KUWASAIDIA WENZETU WAKIKUMBWA NA JANGA LA NJAA

Machache tu niliyochukua kwenye mawaidha yako, Je cha msingi ni kipi hapa? Ukiwa na usafiri wa treni mzuri huhitaji viwanja vikubwa vya ndege kila mkoa. Hata nchi zilizoendelea hazina maviwanja makubwa kila mahali, unataka kuongeza pollution tu. Umefanya tathmini ya yale unayoandika? Tuwe na viwanda vya kutengeneza magari ili hali tuliuwa hata vile vya baiskeli, usafiri ukiwa mzuri wa treni sio lazima kila mtu awe na gari.

Unaongeza la kuwasaidia wenzetu, nafikiri umekurupushwa na hii mada hebu fikiri kabla hujachangia ndugu yangu, nafahamu una uwezo mkubwa wa kuweka mambo.

Mambo mengine yatatokea moja kwa moja kama misingi iliyowekwa ni imara, sasa hiyo misingi ndio tuitafakari na swali la Masaki.
 
namie nichangie kidogo

Tanzania tuitakayo, iwe na watu wenye uchungu zaidi na nchi yao, wawe tayari kuweka mbele maslahi ya nchi yao kuliko ubinafsi.

wananchi wenye kupenda kujituma na kuwa na uwezo wa ubunifu wa jinsi ya kutumia maliasili tulizonazo na kutufikisha kwenye uchumi wenye kujitegemea.

Tanzania inayoheshimu kweli mawazo na fikra za watu wake, sio kundi fulani kuwa wao ndio wenye maamuzi na wengi waburuzwaji.

Tanzania isiyoyumba kisiasa wala kiuchumi, Tanzania isiyo ombaomba.

naomba niwasilishe haya kwanza.
 
Nashukuru kwamba mjadala unakwenda katika mwelekeo mzuri sana!

Ila ningependa pia tunapochangia, tuwe tunashauri/pendekeza na njia au mikakati ya kuifikia hiyo Tanzania Tunayoitaka!
 
Tanzania tunayoitaka sisi ni ile inayotangazwa na vyama vyote ktk ilani zao, malengo yao na hata mwelekeo wao...
Tatizo kubwa la nchi yetu ni UONGOZI ukifuatiwa na SHERIA... Kukosekana kwa vitu hivi nchi imekuwa haina nidhamu hata kidogo na ndio maana tutakwama kila hatua sawa na kaa (crabs) waliokuwa kapuni!

Kila kukicha ahadi ni zile zile tanzania ya kesho kuwa na mwanga kuliko ya jana lakini kila kukicha hadithi hii haibadiliki. Jua halichomozi toka magharibi hata siku moja na ikitokea basi jua kiyama kimefika!

Wakati tukitangaziwa zoezi la Ubinafsishaji mwaka 1992 kila Mtanzania aliamini yale yote yaliyozungumzwa ama kuandikwa kusifia zoezi hili. lakini Tukitazama leo hii baada ya kumaliza kubinafsisha mashirika karibu yote wananchi wamepata nini?...hakuna hata ahadi moja iliyotimia hadi leo bado wananchi hawana uwezo na serikali juu ya kutowatajirisha wananchi kama ilivyoahidi miaka hiyo ndio kwanza inawanyooshea vidole kuwachamba kuwa hawana uwezo!

Kulikuwepo na mashirika ya Umma yasiyopungua 390 ambayo tuliambiwa kila linapouzwa shirika kuna asilimia itawekwa ktk mfuko wa Privatization Trust Fund (PTF) ili kuwawezesha wananchi kukuza mtaji. Na kila zuri liliandikwa na kutiwa nakshi na udi juu yake kiasi kwamba ukisema haiwezekani utaonekana mchawi na huna elimu... but the fact is Hakiwezekani kitu chini ya Utawala uliopanga kukuza mtaji wao wenyewe ili ktk Kizazi kipya wao wazee viongozi ndio wawe matajiri wa taifa jipya la kibepari.

Tanzania tunayoipenda, haikuwa na wala haitakuwa kwa sababu tunapewa ahadi hewa, ahadi ambazo zipo ktk vitabu tu na haiwezi kufanya kazi ktk mazingira tuliyokuwa nayo. Leo hii serikali inakopa Benki ya dunia ili kuendesha mikakati ambayo mwanzo tuliambiwa kuwa fedha zingetoka ktk ubinafsishaji. Zaidi ya USd 800/m kama sio Billioni zimekwisha uzwa nje na bado wanaendelea kubinafsisha lakini hakuna anayefahamu matumizi ya fedha hizo na wala usiulize.....KOSA!.

Miundo mbinu bado mibovu, mabarabara yamechokaa hata yale yaliyotengenezwa wakati wa Magufuli yameanza kuchoka. Maji shida kiasi kwamba leo tunasaidiwa na NGO za watu binafsi walokole..MAJI imekuwa issue Tanzania kweli bado kuna tumaini la kuuliza Tanzania tunayoitaka?

Nchi nzima, leo karne ya 21 hatuna Barabara kuu hata moja yenye hadhi ya kuitwa barabara kuu. Yaani kifupi barabara za mjini Dar zinaweza kuitwa highway kuliko hizo highway zenyewe. Haya reli mtumeee ndio toka Mjarumani, leo kapewa mhindi aliyeshindwa kuendesha ya kwao kwa sababu ya rushwa. Wao wanachohakikisha ni kwamba treni linakwenda, ubora wake utajiju!

Binafsi kinachonisikitisha zaidi ni kwamba hawa wanaotuibia leo hii hawana utamaduni wa kuwekesha ama kurithisha. Ni utajiri ambao utakufa baada ya wao kuondoka duniani kwa sababu viongozi wetu ni wezi na huficha machafu yao hta kwa watoto wao, familia zao na wake zao pia. Wizi na uhujumu uchumi ni sifa katika taifa letu. Sifa inazidi kuwa kubwa kila unapoiba fedha nyingi zaidi hata kama zilikuwa za watoto yatima. Uzalendo ni Upumbavu, Mjinga na aliyekunywa maji ya Ujamaa. You will die poor ndiyo fear kubwa kuliko kufa bila imani ya Mungu.

Investment zao zote ziko nje ati wananunua hisa nchi za nje! badala ya kuwekesha ndani ama wao kuvumbua makampuni ya uzalishaji ndani ya nchi na pengine wao kuuza hizo hisa baadaye. At least umerudisha kitu kwa yule uliyemwibia.

Kifupi hatima ya Tanzania ndio ina sura kuliko ile tunayoitaka na haiwezi kupatikana kwa mtaji huu.
 
Mtanzania na Mkandara,

Heshima zenu sana wakuu. Hakuna maneno mengi, tuna makaa ya mawe, tuna Gesi, tuna bahari, tuna mlima mrefu kuliko yote Africa, tuna lake victoria, Nyasa na tanganyika, tuna Mbuga za wanyama kila sehemu nchini, tuna unutilized/occupied land,ON TOP of all tuna Tanzanite!!, tuna dhahabu na almasi kidogo, na pia tuna Mafuta ambayo hayajaanza kuchimbwa....

Tunahitaji nini tena bandugu?, hamuoni kuwa tupo wengi sana wajinga na wapumbavu, umasikini wetu ni wakujitakia. Hata Mungu aliyetupa yoote hayo atakuwa anashangaa.

So we need only one thing: So far hatujakipata na wala in the next 20 years hatutakipata, Thats UONGOZI BORA WENYE KUJALI MASLAHI YA WANANCHI NA UWAJIBIKAJI KWA WANANCHI.

Andikeni weee lakini tunahitaji hilo tu!!! with that we can say Kwaheri donors! kwaheri Bush na siasa zako, ugaidi umeleta wewe! Je Muungwana ni kiongozi bora? je anasifa hiyo hapo juu? jibu ni MI SIJUI. kwa sababu utakuwaje kiongozi bora uwajibikae kwa wananchi halafu umezungukwa na wala rushwa na opportunists???!!??

Yangu macho

FD
 
Kwa upande wangu ningependa tazania iwe na,

Utaratibu na nidhamu
Hii ni kwa upande wa watawala na watawaliwa, kadri siku zinavyokwenda utaratibu na nidhamu vinazidi kuporomoka, matokeo yake wala ruswa wanazidi bila hofu, kwani mfumo uliopo ni dhaifu unawalinda, kwa upande wa watawaliwa barabarani hakuna utaratibu kila mmoja anafuata sheria zake, angalia tunavyogombania dala dala kama ng'ombe wanatoka zizini, hivi ni vitu vidogo lakini vinamadhara kwenye mustakabali wa wataifa.

Elimu
Ningependa kuona watanzania waliolemika, na sio watanzania wenye vyeti lukuki, watanzania watakao toa michango yao kustawisha taifa, na ambao watakuwa tayari kupiga kelele na kuchukua hatua kuliokoa taifa lao, hii itawafanya watawala waongoze kwa uangalifu kuepuka reaction kutoka kwa wenye nchi.Kwa sasa karibu nusu ya watanzania ni wajinga, kundi hili linajumuisha walio na shahada, stashada, vyeti, na ambao hawakenda shule kabisa, kundi hili ni hatari, halitafakari jambo bali ni kufuata upepo.

Chakula
Ningependa kuona Tanzania yenye chakula cha kutosha, hili linawezekana kwani Mwenyezi Mungu katujalia ardhi kubwa, vijito mito na maziwa, tukiwa na chakula cha kutosha tutakuwa ni taifa lenye watu wenye nguvu na afya njema, na taifa litapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi, kwani maradhi mengi yanayoambatana na njaa yatapungua. Njaa ni kitu kibaya sana, watu wamediriki kuuza uhuru wao wakati wa chaguzi kwa ajilia ya sahani ya pilau.

Uongozi bora
Uongozi bora unategemea watawaliwa, kama watawaliwa watakuwa wameelimika, na nchi inanidhamu na utaratibu, watawala watashika adabu, lazima uongozi bora utakuwepo.

Pressure groups
Tunahitaji pressure groups zilizo huru, ambazo zitasimama kidete kutetea maslahi ya kundi lake, mfano tunahitaji vyama imara vya wafanyakazi vitavyosimama na kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi, tanzania inahitaji vyama imara vya siasa vitakavyokuwa vikipokezana madaraka kwa matakwa ya watawaliwa[ kura], tunahitaji vyama imara vya ushirika vitakavyowakomboa wakulima kutoka kwa unyonyaji wa walanguzi.

naomba kutoa hoja
 
Hi there!**
Naungana na wote kwenye hii mada sensitive, lakini action plans ni zipi? What are strategical plans to meet the goals?
 
Kwa hali ilivyo sasa katika nchi hii, nionavyo mimi tuchohitaji ni Tanzania yenye watu walio na Hofu ya Mungu ndani yao.
Siongelei dini please..hata mpagani anamwogopa Mungu..hakuna dini wala dhehebu linalohubiri wizi, ubadhirifu, rushwa,uongo, tamaa, and the like...I mean the fear of God..with that the rest will follow.
 
Mpiga kura

naona unakwenda mbali sana, swali la msingi hapa ni kujua Tanzania gani tuitaka, startegical plan process ina stages, na kitu cha kwanza ni mission/vision

kitu cha msingi toa mawazo ya tanzania unayoitaka, baada ya hapa tutakenda mbele zaidi na kuumiza vichwa ni jinsi gani tutafika huko tunakotaka kwenda.

kuna mwanafalsafa mmoja alisema 'If you dont know where you are going, it doest much which way you will take.'

lazima tuangalie wapi tunakwenda kwenda alafu, ndipo tutajua njia gani tupite.
 
Kwa Kuongezea Nnataka Tanzania Inayoweka Sheria Kali Kwa Wahujumu Uchumu, Wala Rushwa Na Wasaliti Wa Maendeleo Ya Nchi Na Si Nyingine Ila Ikithibiti Ni Kunyongwa Mbele Ya Halaiki Na Irushwe Kwenye Vyombo Vya Habari. Nnategemea Hii Itasaidia Kuondoa Haya Matatizo Ya Mikataba Feki, Na Kusaliti Nchi Kwa Kutanguliza Maslahi Binafsi
 
Weewe MGUMU**
If it's about vision/mission then mimi nina comply na summary ya FikiraDuni kwamba what we need is ''UONGOZI BORA WENYE KUJALI MASLAHI YA WANANCHI NA UWAJIBIKAJI"
 
Back
Top Bottom