Matatizo ya Tanzania na mapendekezo ya wana JamiiForums

Watanzania wenyewe kwanza ni lazima wabadilike,ndio mambo yote yaliyotajwa hapa juu yatabadilika.Hakuna mtu atakuja kutawala nchi hii akajali maslahi ya watu kuliko yake,hayo alifanya Mwalimu tu.Hii ni hali halisi.

Precedent has been set,we just have to live with it.Sisi tufanye kama hivi,lakini lets be honest,hata mwaka 2015,tukapata rais kutoka Jambo Forums,mambo yatakuwa ni yaleyale.
 
Zanaki

Nakubaliana na wewe mkuu, tukisubiri uongozi bora tutaendelea kuumia, uongozi bora unajengwa na watawaliwa, kama watawaliwa ni mambumbu, waoga wa kuuliza na kutaka ufafanuzi hakuna kitu.

nitawapa mfano kwanini makampuni ya wawekezaji yanafanikiwa, hawa jamaa wanapenda sana critics, mara nyingi tukiwa kwenye vikao, ni mwendo wa hoja, una uhuru hata wa kumkosoa MD kwa hoja, mwisho wa siku maamuzi yanapitishwa na kampuni inasonga mbele.

kwa utaratibu uliojengeka Tanzania, ukiwa mtu wa kuuliza maswali na kutaka ufafanuzi unaonekana msaliti.

Tubadilike ndugu zangu,tusisubiri[/B] uongozi bora[/B]
 
Zanaki na Mgumu,

Ngoja niwape ka shule kadogo ya maana ya uongozi bora. Mahalu kaiba, anapokelewa na karandiga mahabusu mpaka apate dhamana kesi inaendelea. Richmonduli kaharibu, kazi hana, msabaha kaharibu kazi hana. Huyu anatuhuma kazi anasimamishwa. IPTL, walihusika wanasimamishwa kazi uchunguzi unaendelea. Aliyesema wananchi hata ikibidi wale majani, anawajibishwa = Benchi. Kwamtindo huo hata sisi wananchi tutabadilika , tutaona kuwa kumbe ukifanya hivi yanakukuta yale....

Sasa leo ukiharibu unahamishwa wizara au unapandishwa cheo, we unategemea wananchi watabadilikaje???!!!!

Anahitajiwa kiongozi bora sio bora kiongozi ili awabadilishe wananchi kwa kutoa mifano hai na kuchapa kazi!!!

Mmmeeelewa???????, aje kiongozi abadili culture ya ufanyaji kazi serikalini. Ukiunganisha na vitu tulivyo navyo nilivyovitaja hapo juu basi ndoto zenu nyoote mlizotaja zitakuja tuuuu.

HOPE MMELEWA AU NAOMBA MPIGA KURA SAIDIA KUWAELEWESHA.

fd
 
Fikiraduni

Nakubaliana na mawazo yako. Nilitoa mfano katika mada moja hapa: http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=1629

Huwezi kuwa kiongozi bora i-hali unawaogopa baadhi ya wale uliowachagua wakati wanaboronga, na miiko ya uongozi haifuatwi. Leo hii umeharibu huku au kule baada ya mwaka moja au kipindi fulani wanakupa ulaji tena maana yake nini hasa? JK lazima aanze na mtendaji wake mkuu wa serikali na aendelee huko chini kusafisha. Kama hawezi sio lazima kwani nani alimlazimisha aombe urais, sio yeye aliyekuwa anajitangaza anataka kuongoza? Hebu tuone uongozaji wake sasa, mwaka umepita tayari.
 
FD nakubaliana nawe . Tanganyika ina kila kila aya utajiri kuanzia madini ya kawaida hadi uraniamu,mafuta nk . Uongozi wenye kuijali Tanzania ya leo na Tanzania ya kesho basi .
 
Dua, That was a relevant piece of information!

BTW: Nimependa pia "The Western world loves liberalisation, provided it doesn't affect them. But that's the case with all countries all over the world - liberalisation is a great word if it doesn't affect you."

...na nikaihusisha na mambo ya muungano (Jumuiya au Shirikisho la AM) kwamba ushirikiano huo utakuwa mzuri kwa wale wanaojua watanufaika zaidi; na ndiyo hao wanaotushawishi tuungane ili tuwe soko lao na watutawale vizuri.
 
Tunahitaji nchi yetu iwe na amani kama ilivyo na kuwa nchi iliyoendelea nadhani ni nini maendeleo wote tunajua,sasa tutafanikisha vipi hilo ikiwa sisi ni wagema ulimbo???
 
FD na Mpiga kura

Bado sijawelewa kuhusu uongozi bora, Uongozi bora hujengwa na nguvu ya umma, kama umma umelala labda malaika ndio aweza kuwa kuwa kiongozi bora, Hawa binadamu waliopo wataendelea kuoneana aibu, ili kuwa wafanisi[bora] viongozi wanataka kusukumwa na umma.

FD hebu fikiri, wadanganyika wa mkoa wa Dar es salaam, waizingire ikulu na waahidi kuwa hawataondoka mpaka wale wote waliohusika na kashfa fulani waondolewe, na kuhakikishia wataondolewa kwa manufaa ya umma

Na hili litakuwa funzo kwa kiongozi, hata subiri watu wamlazimishe atachukua hatua muafaka kabla mambo hayajaariba, na huu ndio msingi wa uongozi bora 'hofu kwa umma' viongozi wetu hawana ofu wafanya watakalo
 
Hi Mgumu**
Swali lako kuhusu uongozi bora linamaanisha ya kwamba umeelewa, umejijibu mwenyewe bila kujua maana haiwezekani kuwe na uongozi bora bila kuwa na nguvu ya umma otherwise itakuwa ni udikteta (Ubabe wa viongozi).

Ndo maana tulisema ''UONGOZI BORA WENYE KUJALI MASLAHI YA WANANCHI NA UWAJIBIKAJI"
Just resembling to your latest post, isn't it? Naamini tulipishana kidogo tu sasa tuko pamoja!
 
Mgumu,

Mambo mengine ya elimu, maji, ni upuuuzi maana yapo na utajiri tunao. Kiongozi bora ni yule anayetenda kazi zake kwa kufuata miiko na maadili ya kazi yake. Hapo ina maana atakuwa akiwasikiliza wananchi wanachotaka na atatumia utajiri na maliasili ya nchi kwa faida ya nchi na wananchi. Kiongozi kama hao wapo wamejaa tele hapa nchini wanachokosa ni wasaidizi walio thabiti kuwasaidia.... Muungwana nampa benefit of doubt ..nahisi anaweza kuja kuwa kiongozi bora... time will tell..

Mugumu asante kwa kuelewa, maana ikiwa kiongozi anafanya kwa kuogopa wananchi, ni hatari,maana akina CUF wakiandamana anayumba, wakiandamana NCCR anayumba tena! No. we dont need wa aina hiyo. Anatakiwa kiongozi anayejali wananchi toka rohoni.

Yes ..guyz we need good leadership! Period!

FD
 
FD,nakubaliana na wewe 100% kuwa kiongozi anatakiwa kuwajali wananchi toka rohoni,period!
Hizi nyimbo za kusema uongozi bora tumeanza kuzisikia toka enzi za uhuru,i.e,watu,siasa safi,uongozi bora...Wako wapi? Tunaambiwa wapo,watajitokeza lini??
Wote tunajua hii nchi inahitaji nini,lakini how do we get it?It has to come from us.Sisi wabongo hatuwezi kubadilishwa na viongozi wetu hata siku moja.Sasa hivi kuwa kiongozi imekuwa ni short cut to riches.Kiongozi mlarushwa siku hizi sio siri tena kama zamani,tokea Azimio la Zanzibar mambo yamekuwa waziwazi kabisa.Sisi wananchi kila siku humu tunawataja viongozi wala rushwa,tena kufuatana na dili zao,sio mambo ya kukisia tu kama zamani.Hata madereva wa taxi utawakuta wanaongelea rushwa za viongozi,utasikia dereva anakuonyesha ghorofa na anakwambia hii ni ya Anna Mkapa,huyo ni dereva wa taxi,yaani imekuwa ni kitu cha kawaida.
Siku zinapita anakuja kiongozi mwingine na dili nyingine,labda RICHMOND,na soon tutasikia ya National ID Cards.Hizi dili kubwa zote viongozi wamo.Kuna mtu atasema nchi hii katika miaka 20 na zaidi ijayo mtu anaweza kuwa raisi bila ya kutumia pesa za ajabu?SAsa hao ndio viongozi wa kuwabadilisha wananchi? Mifano si tunayo?
Mwananchi wa kawaida anazidi kuzama kwenye despair,na huko tunapoenda hakuna dalili ya mambo kubadilika.
Hii ni nchi masikini inayotawaliwa na maskini.Njaa is the worst enemy! Viongozi wetu wanaingia wana njaa sana,na wanaona miaka 10 ni michache sana.Richmond happened barely a year after the new gvt came to power.

Sisi wananchi wa kawaida ndio tunatakiwa tubadilike ili uongozi ubadilike.Viongozi hawa wanatoka humuhumu amongst us.
Leo hii,majority yetu humu tukipewa platform tuseme tunachoandika humu hakuna atayejitokeza,labda tutampata Freeman Mbowe pekeyake!Do we need a kiongozi to change us even for that?
 
Yes!

1: UONGOZI BORA
2: UWEZO WA KUONA MBALI (VISION).

Nchi yetu naamini ina branch tatu za serikali. Kama wewe kiongozi wa nchi, raisi unaonea watu aibu eti wana mtandao, hakikisha KATIBA YA NCHI inabadilishwa kulinda maslahi ya wananchi wote na kujenga sheria na kanuni zinazoeleweka. Sasa hivi naona viongozi wetu wanabadilisha sheria kwa mdomo tu kunufaisha matumbo yao na ya wachache wakati nchi na wananchi wanaibiwa rasilimali na mabilioni mengi tu ambayo mali za wananchi. Bado sijaona kiongozi mwenye VISION ya kuwakomboa watanzania.
 
Kwa nini tunaweka UMASIKINI mbele? Kwanini tusiseme hawa viongozi ni mbumbumbu? Mbona hawa watu wa kawaida wakiwa na biashara zao ni wakali katika matumizi na uendeshaji mzima wa shughuli zao? Ninachoona mimi ni kwamba hawa viongozi wakishapewa haya madaraka, wanaona ni tiketi ya kwenda kubomoa na sio kujenga nchi.
 
Wanabodi hadi hapa tulipofikia tumesoma mengi ambayo sote kwa pamoja tumechangia ktk kuitazama Tanzania yetu ambayo sisi wote tunaitaka. lakini yote haya hayawezi kufikiwa ikiwa hakuna utekeleza wa sheria - SHERIA pekee ndiyo inayoweza kuwafunga kamba za shingo viongozi wetu hasa ktk kipengele cha Accountability.

Ebu tuyatazame mapendekezo ya Mwenyekiti wa GOPIC alipotembelea Tanzania, kisha akalinganisha mfumo wetu na nchi za magharibi - kisha akaziweka wazi tofauti zetu kwa maelezo mazito sana! hapa chini nakuwekeeni yale yaliyozungumzwa na huyu baba natumaini wengi mtaweza kuziona tofauti hizi na pengine tujadili jinsi ya kuzifikia.

ACCOUNTABILITY:- The simple notion that we are held accountable for our deeds and actions. Respect the rules or pay the price for breaking them.
Accountability can be defined as ’forces beyond our control that cause us to think and act in a certain way’, with the emphasis on ’forces beyond our control’.

Accountability in the developed world Williams says is built into their daily lives.
Their performance at work must be satisfactory in order to keep the jobs.
’We must pay our bills on time if we want to enjoy good credit’.
He points adding that ’We respect traffic lights and speed limits if we want to avoid traffic tickets and demerit points on our licenses’.

What Williams wants to tell us here is that, in each situation, when they break the rules there is a reaction by someone whom they do not control, but who has the capacity to pass judgment and apply a penalty on them.

These are only three examples of a complex web of accountabilities which we have developed to build a prosperous society founded on ethical behavior.

In developed countries the private sector is held accountable by its competition and by government regulation.

While the competitor is beyond the control of the business manager, we cannot say that government regulation is always beyond the control of the business manager.

If a company can influence government regulation to provide it with a special benefit, e.g. government tenders written to meet the specifications of the company\’s product, then government regulation is no longer a force beyond the company\’s control.

For governments, however, there are no competitors and their own regulations are obviously not beyond their control. So where is the accountability for government?

In a democracy, governments are accountable to Parliament.

Parliamentarians are elected by their constituents to publicly oversee the government.
Every political party seeks to form government and obtain a majority in Parliament at election time to support its agenda.

That, coupled with rules designed to reward support of government and punishment for individuality ensures that Parliament is not a force completely beyond the control of government.
In developed countries Parliaments have evolved as the democratic overseers of government with four specific responsibilities:-
1. To publicly debate and approve legislation granting the government authority to manage society and deliver services.
2.to publicly debate and grant authority to government to raise necessary funds through taxation (the budget),
3 Publicly debate and grant authority to the government to spend money in specific services and programs for society (the estimates) and
4. That government report to Parliament in a public way.

The key lesson from the GOPAC Chairman is that, when Parliament is independent, that’s beyond the control of government, it acts for the benefit of the electorate to ensure that government delivers focused programs, lower taxation and a growing healthy economy.

While all parliaments are influenced by government, the question is to what degree? How independent is Parliament?
How well are the electorate informed by a free and open media, and are elections fair and honest to keep Parliamentarians accountable?

I do not want to dwell on takrima issues here, which for sure I know has facilitated many MPs to become MPs, Thanks for the court for the ruling that takrima is corruption.

In the developed world, parliaments are a reasonably independent, open, and transparent check on government, hence their prosperity.
For the rest of the world, parliaments are dominated by their governments - one-party states being a common example of a compliant parliament.
Bribery and coercion of parliamentarians often ensure that parliament is not a force beyond the control of government.
Intimidation of parliamentarians including (jail or assassination guarantees the lack of accountability, in other developing countries).
A compliant Parliament according to Williams may be a wonderful thing for those in power, but it produces an impoverished society.

’When people in government steal their nation\’s taxes with impunity, there is no accountability,’ points Williams adding Parliament has failed to exercise democratic oversight and society fails.
’It would therefore seem that foreign aid should focus on instilling the concepts of democratic oversight by well-functioning and independent Parliaments in the undeveloped world.

Building domestic accountability of a government will make the government listen to its citizens,’ says
No one votes for poverty, infant mortality, illiteracy, inadequate health care, sub-standard housing and non-existent municipal services, but when corruption is out of control that is what the voters receive.

Lack of accountability of government ensures that corruption is alive and well. Theft of state assets by people in power continues unchecked, and the impoverished masses have little hope of their governments being responsive to their needs.
Without criticizing the good intentions behind slogans like ”Make poverty history” foreign aid by itself is laudable, but aid by itself is not sufficient.
Improved governance and accountability of governments must be part of the solution.
Finally for developed countries to realise the envisaged results from donor aids, proper accountability should be enforced, it is through accountability when office bearers will understand that they are accountable to the citizen.

- The Global Organization of Parliamentarians Against Corruption (GOPAC) is an international network of parliamentarians dedicated to fighting corruption by enhancing the effectiveness of parliaments as institutions of oversight for their governments.
 
Mkandara,

Tupo pamoja mkuu. ukiwajali wananchi na kuwajibika kwao ndio accountability, maana utakuwa unafuata maadili na sheria za nchi.

FD
 
Mkandara, mchango mzito huo. Tuahitaji sana uongozi bora, uwajibikaji katika mihilimi yote mitatu ya utawala, ifanye kazi kwa uwazi, uhuru na ufanisi.

Bunge letu ni mhuri wa serekali, ni aibu kuwa na chombo kinachoendeshwa kwa mtindo wa sasa. Uimara wa bunge umekuwa kuangalia wabunge wanasema nini bungeni na sio kuangalia muenendo wa shughuli za serekali. Hali bunge limekuwa mzigo mkubwa, kisagio cha kodi zetu.

Kuna haja ya kuwa na kipengele cha power of recall, kuwapa nguvu zaidi wananchi kuwajibisha viongozi hata kama muda wa uchaguzi haujafika.
 
Hizi nyimbo za kusema uongozi bora tumeanza kuzisikia toka enzi za uhuru,i.e,watu,siasa safi,uongozi bora...Wako wapi? Tunaambiwa wapo,watajitokeza lini??
Wote tunajua hii nchi inahitaji nini,lakini how do we get it?It has to come from us.Sisi wabongo hatuwezi kubadilishwa na viongozi wetu hata siku moja.Sasa hivi kuwa kiongozi imekuwa ni short cut to riches.Kiongozi mlarushwa siku hizi sio siri tena kama zamani,tokea Azimio la Zanzibar mambo yamekuwa waziwazi kabisa.Sisi wananchi kila siku humu tunawataja viongozi wala rushwa,tena kufuatana na dili zao,sio mambo ya kukisia tu kama zamani.Hata madereva wa taxi utawakuta wanaongelea rushwa za viongozi,utasikia dereva anakuonyesha ghorofa na anakwambia hii ni ya Anna Mkapa,huyo ni dereva wa taxi,yaani imekuwa ni kitu cha kawaida.

Sisi wananchi wa kawaida ndio tunatakiwa tubadilike ili uongozi ubadilike.Viongozi hawa wanatoka humuhumu amongst us.
Leo hii,majority yetu humu tukipewa platform tuseme tunachoandika humu hakuna atayejitokeza,labda tutampata Freeman Mbowe pekeyake!Do we need a kiongozi to change us even for that?

Mzee Zanaki, Heshima yako,

Ni kweli, viongozi wetu sasa hivi wanafanya juhudi za kuitamadunisha rushwa. Wanataka tufikie mahala kama Zaire ambapo mtu asiyepokea rushwa au kuiba ndiye anaonekana tofauti na anaweza kuhadhibiwa. Tumekwisha anza kuzoea ntaratibu. Mtu anaiba, akitekenywa, anasema wanamuonea wivu kwa sababu anataka kugombea uraisi na watu wanakaa kimya. Hivyo, sifa ya kugombea uraisi lazima kwanza uwe fisadi.

Hata hivyo, binafsi, siamini dhana ya kuwa kuna kundi fulani la watu wachache ndani ya jamii ya Tanzania, ambalo miongoni mwao wapo watu waliozaliwa na sifa kamilifu za kuongoza. Kana kwamba kazi yetu, ni kuainisha hao watu na kuwakabidhi dhamana ya taifa letu ili watuongoze. Hata hivyo, naamini kuwa nchi nzima, au jamii yote ya watanzania kwa ujumla wake, ni bwawa ambamo kuna watu wana vipaji mbalimbali na bongo bora kiasi kwamba tunaweza kuvua mawazo ya busara ambayo yanaweza kutuendeleza na mwishowe tukawa na taifa tunalotaka kulijenga.

Ni kweli, mojawapo ya matatizo yetu ni ukosefu wa viongozi bora, lakini hili siyo tatizo pekee, na si kweli kwamba tukipata viongozi bora tutapiga hatua muhimu. Kuendelea kuamini hii dhana ni kupalilia mazishi ya umuhimu wa nafasi ya watu wote ndani ya jamii yetu katika ushiriki wa kulipia gharama za maendeleo. Kimatendo, kuna tofauti kubwa baina ya cheo na uongozi. Binafsi naamini kwamba uongozi si cheo, na wala cheo si uongozi. Kushindwa kupambanua hizi tofauti ndiko kumetufikisha mahala ambapo watawala wetu wanaamini kwamba siku wanapopata cheo, busara zinakuja “papo kwa papo”, hivyo kututaka tuwatambue kuwa wao ni viongozi.

Hakuna mwanadamu aliyemkamilifu. Binadamu asili yetu ni wadhambi na wala sio malaika. Tumeumbwa na karama mbalimbali ambazo ni tofauti, kama unavyoona mtu mwembamba, mnene, mpuuzi, mjinga, mwelevu, kimo cha kati, mrefu, mfupi, au mbirikimo, mwaminifu, mwizi, mwema, mwenye tama, kipofu, kiziwi, kilema, mdokozi, na mrembo. Hakuna mwanadamu aliye na karama zote katika ukamilifu wake. Si haba kumkuta aliyejaliwa na akili nyingi, lakini ana udhaifu wa kudokoa jikoni. Mwingine anaipenda sana nchi yake, lakini hana busara, ahambiliki, hashauriki, au ana udhaifu wa kidikiteta.

Bahati mbaya, karama na baadhi ya tabia zinabadilika kutoka na mazingira, malezi, vichocheo vya kibaiologia ndani ya mwili, au umri. Ndio maana watu wengine wanapopata madaraka wanalewa au wanakuwa limbukeni. Wengine wanapopata fedha ndipo tabia zao zinajitokeza (true color). Mwingine hajijuhi tabia yake mpaka anapokuwa masikini. Hivi ndivyo mungu alivyotuumba. Katika sehemu iliyokubwa ya maisha ya kijamii, kuungana kwa karama zote ndani ya mtu mmoja hakutokei. Hata watu mithiri ya Nyerere ambao wanasifika kuunganisha busara na cheo, ingawa pia alikuwa na udhaifu mwingine, hawazaliwi kila mwaka.

Lazima tutambue kwamba hazina ya uongozi wa jamii yetu haiko katika uongozi rasmi tu, kwa maana ya wale waliochaguliwa na ambao wamekalia vyeo, au wale walioteuliwa kufanya kazi za utendaji. Katiba ya nchi yetu inagusia umuhimu wa wananchi kwa ujumla wao katika maendeleo ya nchi. Hakuna mbadala wa maoni ya wananchi na utashi wao. Viongozi wote wa kisiasa wanawajibika kusikiliza wananchi wanasema nini na kuyatia maanani hayo yanayosemwa na wananchi. Wananchi ndio chimbuko la madaraka na nguvu ya watawala na wote wanaotarajia kuzungumza kwa niaba yao.

Utamaduni tunao ujenga wa kujiaminisha kuwa tatizo letu ni ukosefu wa viongozi bora, na wala si ukosefu wa wananchi wenye uwezo wa kuwajibisha viongozi wao, unajenga mazingira ya kuwatenga wananchi katika nafasi ya uwajibishaji na kuwafanya viongozi waamini kuwa wao peke yao ndio wanaweza kuleta maendeleo na kuiacha jamii nzima usingizini ikiwa inasubiri hayo maendeleo. Ndio maana viongozi wetu wanajiaminisha kwamba wanajua matatizo ya wananchi kuliko wananchi wenyewe wanavyoyajua. Binafsi naona tuachane na huu utamaduni kwa sababu unawafaa wale waliomo madarakani kwa sababu tu ya kupata maslahi ya muda, na hawajali nini kitatokea wakiisha kuondoka madarakani au kufa. Ni utamaduni ulioangamiza tawala nyingi katika historia ya mwanadamu.

Hivyo basi, naamini msingi wa maendeleo ni watu, ardhi, siasa safi, na uongozi bora. Kupigwa kaputi kwa sifa mojawapo katika huo mlolongo kuna athili mpangilio mzima wa maendeleo. Vyote vinategemeana kama ifanyavyo kazi milango ya fahamu ya mwili wa binadamu, na si rahisi kuvitenganisha. Nadhani ni makosa kuweka mustakabari wa maisha ya watanzania wote chini ya fadhila za kiongozi mmoja au kundi la watu (viongozi) tukidhani kwamba wao ni wakamilifu wa sifa zote. Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tunapingana na sheria ya asili au ya yule aliyetuumba.

Imekuwa ni kawaida ya mwanadamu kunyoosha vidole au kumtafuta “mchawi” pindi mambo yaendapo mrama. Tunaliengua neno “watu” kwa sababu linatutaka na sisi tuwajibike. Neno “watu” halimaanisha wale wanaovaa Sketi na Blauzi, au Suluali na Shati tu. Si wakulima ambao mazao yao yanakopwa na wajanja bila malipo, alafu wao wanalidhika. Si wafanyakazi wanaonyanyaswa na baadae kila mmoja akaamua kuchukuwa chake mapema. “Watu” maana yake ni wale wabunifu, wanaohangaika kuyabadili mazingira yao. Wasio kubali kuonewa, kunyanyaswa, kutapeliwa, kupuuzwa, kutokusikilizwa, kuibiwa, kudanganywa, na kufanywa vichwa vya wendawazimu. Ni wale wanaoiwajibisha serikali, waliopita shule na shule ikawapitia.

Ingawa idadi ya watanzania imefikia milioni 35, lakini sio lazima yawepo mahusiano kati ya hiyo idadi ya watu, na idadi ya watu wa kuleta maendeleo. Kamwe, katika maendeleo, neno “watu” halina maana ya namba (interms of quantity). Lina maana niliyoielezea juu. Hivyo basi, tuna uhaba wa watu pamoja na viongozi. Hakuna nchi yoyote duniani iliyowahi kupata maendeleo thabiti na ya muda mrefu bila ushiriki wa watu katika kuiwajibisha serikali yao. Vivyo hivyo, hakuna nchi iliyojikomboa kutoka katika ukandamizaji wa aina yoyote bila watu wake kujitoa muhanga. Si mara nyingi viongozi wakawajibika kwa hiari yao. Makabulu wa Afrika Kusini waliachia ngazi kwa sababu nyingi, lakini mojawapo kubwa ni kuwa nchi ilifikia mahala ikawa haitawaliki. Philippines wananchi walichoka na mauzauza wakauzingira mji wa Manila mpaka Raisi wao akaamua kuingia mitini.

Ni udhaifu huu wa mwanadamu uliyoyafanya mataifa yaliyoendelea duniani yawe na mfumo wa “checks and balance”. Hakuna kumwachia kiongozi mambo yote, bali jamii nzima inawajibika katika kuangaliana na kukosoana. Si kweli kwamba viongozi wengi wanaotawala nchi zilizoendelea wana moyo wa kuipenda nchi yao kuliko wanavyojipenda wao. Wengi ni wabinafsi kama walivyo viongozi wa nchi yetu. Majuzi, Bob Ney ameingia kwenye daftari kama mbunge wa 40 kutoka katika bunge la Marekani, kufungwa jela kwa sababu ya vitendo vya rushwa.

“lobbyists” waliotembeza rupia katika mikataba ya IPTL na RADA nchini kwetu, hawana tofauti na wale walioko Marekani. Kuna mtu anaitwa Jack Abramoff ambaye alipokea $9 milioni kutoka kwa Raisi wa Gabon bwana Omar Bongo ili amfanyie mpango wa kukutana na Bush (New York Times 10, 2005). Rafiki zake wakubwa ni Newt Gingrich, Dick Armey, George Bush, na Tom Delay. Hata hivyo huyu jamaa amehukumiwa miaka 5 na ushee jela kwa sababu ya vitendo vya kuwaonga viongozi wa Marekani. Hajaanza kifungo chake kwa sababu wanataka atoe ushahidi against Tom Delay aliyekuwa spika wa bunge la Marekani.

Clinton anaeleza katika kitabu chake jinsi marafiki zake wa Arkansas walivyosekwa jela wakati anapelelezwa na alikuwa anaogopa kuwapigia hata simu ili asije kumbwa na “obstruction of justice”. Bush alimuona rafiki yake kipenzi Ken Lay akiendeshwa puta na vijana machachari wanaowakilisha maslahi ya wananchi bila msaada pamoja na kwamba alikuwa ni Raisi wa nchi. Raisi Nixon alikimbia miiba kwenye kiti chake cha enzi iliyowekwa na wananchi wanaoiwajibisha serikali yao. Matendo ya hawa viongozi yanatokana na woga waliono juu ya wananchi, na wala sio kutokana na moyo au uzalendo wa nchi zao.

Ni rafiki gani wa Kikwete, Mobutu, Gadafi, Banda, Mkapa, angeweza kwenda jela kwa sababu ya vitendo vya rushwa? Ni viongozi wangapi wa nchi za Afrika wako jela kwa sababu ya rushwa? Ni Raisi gani wa Afrika alijiuzulu baada ya kukiuka miiko ya uongozi?. Tatizo la Tanzania ni kuwa na Raisi mwenye nguvu kubwa kikatiba hivyo, kufanya wananchi wategemee fadhila zake. Katiba yetu imempa Raisi madaraka makubwa kiasi kwamba wananchi hawana huwezo wa kuthibiti matendo yake.Mfano, wananchi wakiamua kuwakilishwa na wabunge NCCR-Mageuzi, alafu wakamchagua Raisi kutoka CCM, Ibara ya 90 (1) (e) ya katiba ya nchi yetu inampa mamlaka Raisi kulivunja Bunge na kuitisha uchaguzi mpya hata kama kufanya hivyo, nikupingana na utashi wa wananchi.

Wabunge wetu ambao ni wawakilishi wa wananchi, hawana uwezo wa kikatiba wa kukusanya mawazo ya wananchi wanao wawakilisha na kuyapeleka bungeni kama muswada ili yapigiwe kura na wabunge wote. Mfano mzuri ni issue ya madawa ya kulevya iliyosimamiwa na Amina Chifupa. Kikatiba, Amina hawezi kukusanya mawazo ya watu ambao wanakelwa na tatizo la madawa ya kulevya, alafu akawashawishi wabunge ili itungwe sheria kutokana na mapendekezo ya watu. Anachoweza kufanya ni kuiomba serikali ianzishe muswada. Mfumo huu unaweza kuwa kizingiti kama tuna viongozi wa serikali wenye moyo wa kuipenda nchi yetu lakini wako “addicted” na madawa ya kulevya.

Tanzania tumejaliwa kitu komoja tu Ardhi, vingine inabidi tufanye juhudi za makusudi kuvipata.
 
Back
Top Bottom