Matatizo ya Tanzania na mapendekezo ya wana JamiiForums | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matatizo ya Tanzania na mapendekezo ya wana JamiiForums

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tafiti then jadili, Sep 11, 2006.

 1. t

  tafiti then jadili Senior Member

  #1
  Sep 11, 2006
  Joined: Aug 24, 2006
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naam inaonekana kuna maendeleo kiasi ingawa safari bado ndefu sana, tunahitaji kasi mpya manake hii ya sasa haitufikishi tunakotaka kwa haraka:

  Source: The Guardian la tarehe 11-09-2005

  A new global business survey by the World Bank has discovered that the cost of registering new business in Tanzania has dropped by 40 percent.

  This rare plus comment from the Bank cites reduction in licensing requirements, introduction of an electronic customs clearance system and implementation of risk-based inspections of cargo at ports as factors which have jointly worked to improve the country’s business image.


  ”As a result, customs clearance times dropped from 51 to 39 days for imports, and 30 to 24 days for exports” the report says.


  Recently, Tanzania also cut fees associated with transferring property by 3 per cent and revisited its company law to improve the situation.


  It ranks Tanzania as one of the most reforming countries which have succeeded in reducing red-tapes and other bottlenecks which discourage business growth.


  This year the country ranked 147th country in comparison to its last year position of 175, this being an improvement of 8 points.


  The survey, which was conducted across 175 economies, has come out with Tanzania and Ghana as being the 10 top reformers on the ease of doing business.


  According to the report, the 10 top reformer countries in order are Georgia, Romania, Mexico, China, Peru, France, Croatia, Guatemala, Ghana and Tanzania.
   
 2. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2006
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Go and tell that to millions of hungry and hopeless poverty-stricken people in Buzebazeba, Ngara, Namtumbo, Malinyi, Kibugumo,etc and they'll wonder whether you're from Tanzania or another country.

  And by the way, who's doing business in the country?
   
 3. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2006
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Tafiti samahani sana sijui wewe unafanya kazi gani, lakini kama uko serious tuwekee yale ambayo yamo kwenye www.cia.gov and click Tanzania fact book. uone huo uozo! Hivi wewe kuona Tanzania, China, Mexico,... group moja ukaona kuwa basi is a step? Let me tell you one thing we are 100 years behind China economically. Please do not bring those datas to soothe our minds; first go and put that house (which is tainted of graft) clean.
   
 4. t

  tafiti then jadili Senior Member

  #4
  Sep 12, 2006
  Joined: Aug 24, 2006
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bwana Interested Observer:

  Hata wewe ungeweza kuleta hizo za CIA, mimi sijafurahia kabisa hii kasi ya maendeleo kama nilivyoweka katika utangulizi, tafadhali read between the lines.

  Sasa unapodai haya unayodai inaonyesha hufuatilii michango yangu, kuna submission ya China nimeweka humu nenda kaisome upate mwangaza kuhusu my fair comparison baina yetu na China.

  Unao uhuru wa kucounter argue my arguments kama mwingine yeyote ninavyoweza kuchangia lakini usiweke hapa ati nimeweka data hizi kusoothe our minds!
   
 5. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2006
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Why was it that so many Tanzanians jumped up and down, jubilantly, when all these tapeli cohorts were elected into office? Why do Tanzanians continue to believe, against all odds, that they have a very good president? Only in Tanzania could you have a people whose government can supply neither water nor power, and yet is considered ari mpya, kasi mpya, and nguvu mpya.

  As long as people continue to be so easily hoodwinked, they will disown themselves of their gas, minerals, Mt. Kilimanjaro and even wild life. It is all coming!

  You can go to Tanzania with no money of your own, take their money (from their CRDB), use it on gas that was previously theirs (before another investor convinced them to let him have their gas on the understanding that he would give them 12.5% of it - they easily forgot that it was 100% theirs), and sell them the resulting power?

  We are, I submit, harvesting the fruits of many decades of under-funding education. This will not end anytime soon, for we continue to spend less than 10% of our budget on Education. Our much smatter neighbors in Kenya are spending 27% of their 2006/2007 budget on Education.

  Augustine Moshi
   
 6. M

  Mwanagenzi JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2006
  Joined: Sep 11, 2006
  Messages: 690
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Mlalahoi,
  Mi naona we ndo umemiss point yangu ambayo ni kuwa habari ya mwanzo kama ilivyotolewa na Daily News inaungwa mkono pia na THISDAY! Sina shaka na THISDAY na nawajua waandishi kadhaa wanaofanya hapo, pamoja na Mhariri wao ambaye aliwahi kuwa Afisa wa juu pale Maelezo.
  Ninachosema ni kuwa tuwafuatilie kina Richmond na hao Songas wao ambao mitambo inaharibika kila siku!

  By the way, mmoja wa wakurugenzi waanzilishi wa hao jamaa waliotaka kujenga bomba la mafuta, alikuwa akiitwa Athumani Mfutakamba(?), si ndiye huyo huyo aliyegombea ubunge wa Afrika Mashariki akakosa, na pia alichukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM (2005), akachujwa? Je, ndiye huyo sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo huko Iringa? Wazee leteni data!
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2006
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwalimu Moshi,
  Nakubaliana na wewe lakini nadhani tatizo si "underfunding of education." Kumbuka wote waliosaini mikataba hiyo na matapeli wamesoma sana tu. Ni ukosefu wa uzalendo, kutojithamini na ubinafsi wa kukubali visenti vya 10% ndivyo vilivyotupelekea hapo tulipo. Mimi, kama wewe, vile vile sina mategemeo makubwa na serikali ya awamu hii. Ni wale wale
   
 8. m

  mTz JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2006
  Joined: Aug 20, 2006
  Messages: 283
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Jasusi,

  Hapo umenena, sio kuwa hawana uelewa wa kuchambua mambo hawa technocrats na bureaucrats wetu, ni ukosefu wa uzalendo as if nchi hii itajengwa na watu wa nje
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2006
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mimi nasema Kidumu Chama cha Mapinduzi na
  kasi za JK na washirika wake mtaziona safari hii maana mlishindwa kuhoji mbiu zake za kasi zilikuwa za aina gani .Kazi iko tuendelee
   
 10. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2006
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,722
  Likes Received: 1,213
  Trophy Points: 280
  Wandugu
  Tanzania tuna kazi kweli kweli. Mimi naona nimuunge mkono Augustine Moshi kwa hoja yake ya under-funding kwenye elimu. Kwanza ni kweli ndugu Jasusi kwamba huu utapeli unafanywa kwa kukosa uzalendo kwa hao culprits.

  Lakini huo utapeli unapata nguvu na mazingira mazuri(conducive environment) mbele ya public isiyoelimika. Nyinyi mnadhani Kikwete angepata kura zote hizo kwenye uchaguzi kutoka kwa watu walio huru kielimu?

  There are too few enlightened people in this land. And so follows....ignorance among wabongo is rampant.

  Mzee Moshi you have a point!
   
 11. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2006
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mzee Invicible,

  Great points bro!
   
 12. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2006
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Wandugu,

  Si rahisi kuwaonea watu wenye elimu ya kutosha. Juzi, Barrick Gold wameamua watatupa RUZUKU ya $7 million kwa mwaka, na wananchi wakashangilia sana. Mtu anachukua dhahabu yako ya kama $500 mil kwa mwaka, anakupa ruzuku ya $7 mil unashangilia! Ni kutokana na kukosa elimu. Ilitakiwa wananchi wakasirike na kuandamana kwa kudharauliwa. Tanzania inapashwa iwe na majority share kwenye hizo kampuni, sio ipate makombo.

  Wanaotia sahihi kwa niaba yetu wanajua tunaibiwa, lakini kutokana na wenyewe kuwa wezi, wanagawana na wezi wa nje. Tungekuwa tumeelimika vya kutosha, hatungeshangilia tunapoibiwa; tungepinga na kufukuzia mbali wezi wa nje na washirika wao walioko kati yeu.

  Inasikitisha kuona waandishi wa magazeti yetu nao wana uelewa finyu sana. Ukiondoa walifunguka macho kama Lusekelo, wanabaki wachache sana. Wanamshangilia JK kama vile mtu unavyoshangilia mpira! Lowasa anatangaza atajaza Bwawa la Mtera kwa mvua za kutengeneza, na magazeti yanatangaza kwa furaha!

  Due to many decades of underfunding of our education, we now find ourselves surrounded by buffoons!

  Augustine Moshi
   
 13. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2006
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kwa kitendo kile magazeti yakaandika kama kawaida misifa .JK aanza kufanya kweli .Mimi nikashangaa na wananchi wakasema kweli jamaa anafanay kweli .Pale ndiyo JK kamaliza sasa anahamia kwa Bush na mikataba Msabaa anaingia nayo sasa .IKo kazi kamaliza kwenye madini mimi nasema sasa kahamia kuuza na kutishia kurudishia nyumba.Mimi siamini kama atarudisha .JK si mkweli alikuwa kanunua nyumba akakana na kukaa kimya sana .Baadaye anasema na yeye anayo nyumbani , baadaye hatachukukua nyumbani leo kimetokea nini akachukue nyumba hizo ? Madini yana historia bwana Mtandao mzima uko naye na wana mkono mkubwa kwenye madini kweli anaweza kusema lolote kama serikali yake inatetea IPTL ?Tungojee Ziara za Thailand na Vietnam na huko Malasia kuwaita wezi waje kutumaliza tuuuuuuu hakuna la zaidi hapa
   
 14. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2006
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nimekupata Mwanagenzi
   
 15. t

  tibwilitibwili Senior Member

  #15
  Sep 23, 2006
  Joined: Sep 12, 2006
  Messages: 181
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bongo yatangazwa au yamalizwa?
  Tunaomba kupigia pande maoni haya juu ya ziara ya Rais JK na ujumbe wake wa watendaji kibao na wafanyabiashara kiduchu wanavyoitangaza Bongo nchini Marekani.

  Maoni yametokana na stori ya uduni wa bidhaa za Bongo baada ya malalamiko kutoka Shirika la Viwango nchini Kenya

  Haya Sasa hapo ni Kenya je huku UESIEI [USA] bidha hizo zitauzika kweli?

  Sambamba na Stori hii ya shirika la viwango kuidhinisha bidha zenye uduni na uhafifu kwa kila kipimo kuna tatizo la kujinadi.

  Wafanya biashara kadhaa katika msafara wa Rais Kikwete hapa majuu nchini Marekani wamewashangaza wenyeji wao kwa kusafiri maelfu ya maili na kufika hapa wakiwa hawana cha kunadi.

  Aidha msafara huo wa Rais kwa nia ya kunadi bidha za Tanzania na Tanzania kwa ujumla nchini Marekani umeingia kasoro kwa kuweka lolongo zito la watendaji wa serikali ambao kazi yao kubwa imekua kujitetea kwamba hawakuwa na maandalizi ya kutosha na mabo mengine yanayowaonyesha kwamba matako yao wanayatumia vizuri kukalia viti vya serikali.

  Kwa mujibu wa mfanya biashara mmoja nchini Tanzania mabaye nimeongea naye kwa simu na hakutaka jina lake litajwe.

  Msafara huo umekuwa na dosari kwa sababu serikali kwa makusudi ilichelewa kuwatangazia wafanya biashara kuhusu safari hiyo ya kuinadi nchi na bidha zake ili nafasi hizo zijazwe na watendaji hao.

  Ambao wamekuwa na usongo wa kukita hapa USA kwa sababu binafsi.

  Kitendo hicho cha serikali kutoa taarifa kwa kuchelewa ni kitendo cha kihuni ambacho hakitakiwi kurudiwa na serikali ya CCM kwani kimeleta aibu kubwa sana na zaidi kuikoseha nchi nafasi ya kufanya biashara na Vibopa hawa.

  Mbali na mafanikio kadha ambayo yamepatikana katika msafara huu kumekuwa na wafanyabiashara wengi amabo wamejikuta wakigwaya kujinadi mbele ya vibopa wa Marekani kwa kutoa maelezo muflisi yasiyo na sura kibiashara na sababu kubwa ikiwa ni kutojiandaa kwa vile muda wa kujiandaa ulikuwa ni mfupi.

  Pia unyonge wao wa kuwa na uzoefu wa kufanya biashara za magendo huko mafichoni ambazo zinahitaji kuongelea chemba kwa kuteta.

  Vilevile kutojua utamaduni wa Wamarekani ambao kwa asili yao kama unashindwa kujieleza juu ya kitu unachodai unakijua vizuri wanakuchukulia kwamba wewe ni mbabaishaji, mwizi, mzushi au pengine ni mtu ambaye huko serious.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo wafanyabiashara wengi baada ya kupewa nafasi ya kuongea mbele ya wakuu wa makampuni mbali mbali ya huku Marekani ili kunadi bidha zao walionekana wakisema watatoa maelezo zaidi baadaye katika maongezi mengine yasiyo rasmi.

  Bila kujua kwamba kushindwa kuutumia muda uliopewa ni kujinyonga mwenyewe kimaslahi, unakufa kibudu.

  Hapa Marekani ukipewa dakika 15 za kujieleza kuhusu biashara yako inabidi kuhiti point bila kusita. Biashara inanadiwa hadharani si mafichoni kwa hiyo ukishindwa kuzitumia dakika ulizo pewa wanakuweka kapuni na huo ndo mwisho wako.

  Katika dakika hizo 15 ukijieleza vizuri vibopa hao watakufuata na kutaka kuingia mkataba na wewe na kazi inazaliwa.

  Watendaji wa serikali ya CCM wamechemsha kwa kutowapa black and white ya utamaduni wa biashara na hawa jamaa wa Marekani.

  Taarifa inaendelea kusema baada ya Wafanyabiashara wetu wazawa kushindwa kujieleza juu ya biashara zao za madini, nafaka na nyinginezo, mabosi waliowaandalia msosi wa kujuana kibiashara walisimama na kuwapakazia moja kwa moja kwamba;

  �Mmekuja hapa kunadi bidhaa zenu siyo kutueleza matatizo yenu.

  Ili mfanye biashara na sisi ni lazima bidha zenu ziwe bora kuliko za watu wengine na si vinginevyo. Hapa hatuuzi maneno wala porojo za aina yeyote ile.

  Tunataka biashara. Biashara yenu iko wapi? Tatizo la mitaji si tatizo letu benki zipo kwa sabau ya kukopesha watu ni ajabu kwangu kusikia kwamba katika karne hii ya 21 mtaji ni tatizo�

  Hivi hawa watendaji wa serikali wamejazana katika msafara huu kwa madhumuni gani?

  Wanabidha gani za kuuza?

  Hii ni karne ya 21 bado tuna watu ambao wanajichomeka kwenye misafara ya kwenda nje ili wawanulie wake au waume zao *&%$#&*# za huku Unyamwezini?

  Uwiano wa watendaji na wafanya biashara ulikuwa 6:4.

  Nilidhani katika kila mtendaji mmoja wa serikali wangekuwako wafanya biashara 4 na kuleta uwiano wa 1:4.

  Wafanya biashara wazalendo ndiyo wanaoweza kufanya biashara na kupata faida itakayoijenga nchi.

  Watu wa serikali kazi yao ni kuweka mazingira mazuri na kuwatambulisha wafanya biashara wao na pengine kuwahakikishia Wazungu hawa kwamba Azimio la Arusha limekufa kifo cha asili na ikiwezekana wawaonyeshe picha za kaburi la Azimio la Arusha kama wanazo.

  Mimi nimesoma Digrii yangu hapa Marekani. Pamoja na watu wengi huko nyumbani kutupakia kwamba Digirii za huku ni feki bado ninaweza kusema zimetufundisha mengi ambayo mitaala ya kwetu haijayaweka.

  Kuna Somo linaitwa CRITICAL THINKING. Hili somo ni muhimu sana hasa katika mambo ya mahusiano.

  Kama umesoma somo hili unaweza kujifunza haraka haraka juu ya nini cha kufanya unapofika mahali ambapo hujui wenyeji wana utamaduni gani .

  Pia linasaidia kusoma vitu ambavyo katika mahusiano havitamkwi ila vinaonyeshwa katika hali ya implication vitu hivyo vinaweza kukueleza kwamba umewini au umelala ngoma.

  Kwa mfanyabiashara yeyote ni vizuri kujua utamaduni wa mtu unaye ongea naye hasa akiwa ni taifa au utamaduni tofauti na wako.

  Kuongea biashara na Mmarekani ni tofauti kabisa na kuongea biashara na Mjapan. Mjapani hataki direct hitting angependa mfahamiane kwanza.

  Lakini Mwamerika anataka uhit point kufahamiana zaidi ni baadaye kwa nini umcheleweshee muda wake wakati huko tayari au mambo yako ni valuValu?

  Watendaji wa serikali na serikali kwa ujumla inapofika suala la kuinadi nchi kibiashara wanachemsha sana.

  Elimu yao inawasaidia kusoma Daily News na kuandika taarifa nzuri zenye mbwembwe za kisiasa zinazotetea mambo ambayo wakipigwa maswali mawili mimacho inawatoka mithili ya panya aliyenaswa na mtego.

  Hili la bidhaa duni ni udhaifu wa serikali na watendajiwake na hili la kushindwa kuinadi Tanzania hapa UESIEI ni tatizo la serkali na watendaji wake.

  Safari ijayo naomba watendaji wa serikali watumie nafasi hiyo kuwaandaa wafanya biashara na pengine kuhakiki taarifa zao ili wasitutie aibu.

  Hata hivyo kwa ujumla safari ya kuinadi Tanzania hapa Marekani ni hatua moja kubwa ambayo serikali yetu imechukua katika harakati za kujenga uchumi wa nchi.

  Mafanikio yaliyopatikana yawe chachu kwa wale waliokuja bila kujiandaa.


  Ndelanzali Hingi
   
 16. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #16
  Sep 24, 2006
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mambo makubwa haya Mzee uko na hawa watu huko hebu tupe habari za huko
   
 17. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #17
  Sep 25, 2006
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Wafanya biashara za kimataifa wa Tanzania ni akina nani? Ukiondoa Mengi na labda watu wengine wawili au watatu, unabaki kweli na wafanya biashara za kimataifa?

  Kwa sasa, mfanya biashara wa kawaida wa Tanzania ni mtu mwenye kitu kama lori la kubeba kifusi na labda daladala moja, au ni mtu mwenye baa inayouza masanduku kama 10 ya bia kwa siku, au ana mahali anauza wali kwa ng'ombe, au ana duka ambalo ukitaka kitu unakinyoshea kidole kisha yeye au mke wake au mtoto wake anakuchukulia na kukuonyesha.

  Naomba Tibwilitibwili ututajie hao wafanya biashara walikuwa kina nani. Inaeleka umetaja ombaomba waliodhani wangepata mtaji toka kwa wafanya biashara wa Marekani.

  Augustine Moshi
   
 18. A

  Aljazeera Senior Member

  #18
  Sep 28, 2006
  Joined: Jun 27, 2006
  Messages: 125
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Wananchi tumechoka, viongozi hawajitambui

  Ni kihoja na vituko kuwasikiliza sembuse kuwachukulia viongozi wetu wa nchi serious. Ninaposema viongozi namjumlisha rais, waziri mkuu mpaka mwenyekiti wa kijiji.

  Swala ambalo kila siku nimekuwa najiuliza hasa baada ya hii Serikali ya Awamu ya nne ni je Nchi yetu Tanzania tunaongozwa au kutawaliwa na wagonjwa wa akili au akili zenye ugonjwa. nasema hivyo kwa sababu ukitafakari yanayofanya na hawa wavivu wa kufikiri (viongozi) sidhani hata kama hospitali ya Mirembe itaweza kutupa majibu kamilifu.

  1. Rais wa Tanzania: Kwa mara ya kwanza nchi imekuwa na rais msanii wa kimazingira. Afadhali angekuwa msanii wa kimaudhui kuliko alivyo sasa. Ni rais gani wa Taifa gani ambaye ndani ya miezi nane ametembelea Mabara tano kati ya saba, au ni rahisi gani alitembelea nchi 16 karibia ya nusu ya nchi alizotembelea John Paul II kwa miaka 25 ya Upapa. Ni rais gani atakayetumia milioni 600 kwenda kutafuta mkopo wa bilioni moja? Ni rais gani asiyeweza kukaa ofisini zaidi ya wiki moja bila kusafiri.
  Kama siyo kuchanganyikiwa ni raisi gani au mtu ye yote mwenye akili timamu anaweza kwenda kutafuta mtu wa kupangisha nyumba angali hiyo nyumba hujajenga sembuse kiwanja huna. JK anatembea Dunia kutangaza na kuvutia wawekezaji kama anavyodai, je kama angekuwa nazo zote au hao washauri wake wasingekuwa wavivu wa kufikiri, wangejiuliza ni mtu gani anaweza kuwekeza sehemu ambayo haina Umeme au miundo mbinu. Ni wapi amewahi kuona mtu akihifadhi mali kwenye stoo isyo na mlango au mlinzi.
  Hizi huyu rais wetu anajifahamu na kujiheshimu kweli, binafsi siamini kama anajitambua kwani kama alikuwa anajitambua basi asingefanya vioja hivi.

  2. Waziri Mkuu: Huyu ndiye wala sina usemi kabisa, nadhani kama angeweza kusimama na kutuambia angalau faida moja tu ya safari yake na familia nzima Thailand na Vietnam basi tungejua anazo zote. Tangia Tanganyika ipate uhuru wake hajawahi kutokea waziri mkuu mwenye matumizi mabaya wa mali za umma kama huyu. Pamoja na PM aliyepita kuitwa zero nadhani huyu wa sasa itabidi atafutiwe jina kwani hii staili yake inanifanya nifikiri labda karuka madarasa ya shule na ya kijamii hasa darasa la "critical thinking"

  Ndugu EL hivi una washauri na kama unao je wewe binafsi huwa unafikir kabla ya kutemba hasa unapotoa kauli kwenye kampeni zako. Tangia uchaguliwe sijaona hata siku moja umesema jambo lenye mbolea, naomba ujaribu kufikiri angalau kidogo haa unapotoa kauli kuhusu UMEME

  3. Mawaziri: Masha, Msabaha, Mramba etc, mnatia aibu siyo wizara zenu tu bali hata mnajiletea aibu peke yenu. Mambo mnayofanya sidhani kuna mtu mwenye akili anaweza kufanya hivyo vioja. Kama hamwezi kufikiri au mmechoka tafadhalini ondokeni kwani mnazidi kurudisha gurudumu la watanzania nyuma. Kwa mnayofanya nadhani ni Rais wa Tanzania tu anaweza kuwapa madaraka na si mtu mwingine.

  Ningependa kuendelea lakini nadhani ni muda wa kujiuliza

  Tufanye nini kuondokana au kubadili fikra za hawa viongozi wavivu wa kufikiri
   
 19. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2006
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Topic muhimu! Uvivu wa kufikiri!!! Nilkuwa naumia kichwa kwenye IPTL, Madini etc etc, na sasa zile privatation za Tazara, TRC na NIC: Kweli viongozi wetu hawana ufikiri:
  1. Rite of India: Wana proven track record iko wapi? Mie kila siku naona kule India train ziko-congested na watu wako juu ya mabehewa sasa sijui kwa akili yangu ndogo sana hii naumia kichwa, hawa wata-add value gani?
  2. China - Nasikia wanapewa TAZARA kwa sababu wamejenga, lakini matatizo ya management ya wachina yanaeleweka kote, siyo kwao tu hata hapa, Urafiki, na viwanda vinginevyo, zambia mgombea urais ashasema akipata urais ataangalia upya Chinese investors. Hawa jamaa hawana labour laws defined kwao hata safety records - Kichwa kinaniuma
  3- sasa leo napata kizunguzungu niliposikia ati Nigeria wanaweza kuchukua NIC, lo, hivi jamani tunaenda wapi? Tunajua zile 419??

  Hivi hawa viongozi wanafikiria??
   
 20. E

  Eric Ongara Verified User

  #20
  Sep 28, 2006
  Joined: Sep 19, 2006
  Messages: 165
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huu mjadala una hamasa zaidi,ikukumbukwe kwamba serekali ya awamu ya nne haikuahidi kufikiri wala kuleta upya! Wao walisema wanaongeza kasi,nguvu na ari. Ndio kasi yenyewe!

  Kungekuwa na neno badiliko ingeonyesha dalili ya ya kufikiri. Zipo njia mbili za kuwaondoa! Demokrasia,kwa kuimarisha vyama vya upinzani,kuvisaidia kukuza rasilimali fedha na watu ama njia ya pili ambao sikubaliani nayo sana ya mwendo wa "mahema". Ni kweli wanakera sana
   
Loading...