Matatizo ya remote za king'amuzi cha Azam

Matatizo ya remote za king'amuzi cha Azam

Je....!!! Hizo remote munazo zisema,mumezinunua na kingamuzi au ni zile za Kkoo ambazo pia zina nembo ya Azam..???
 
Azam kwenye remote hamna kitu,halafu king'amuzi kaupepo/ mvua kidogo scratchiiiing.Mpaka sasa nategemea kufunga Decoder nyingine nishawachoka hawa
 
Mkuu, ulisolve vipi tatizo la king'amuzi?.... Changu pia button hazifanyi kazi, na remote yake nayo inazima tu na kuwasha button nyingine zote hazibadili kitu.........
daa ata rimoti yangu hivyo hivyo
 
Heshima kwenu wadau

Lengo ka uzi huu si kuwaharibia biashara azam Tv lengo ni kutaka kujua tatizo gani ambalo linafanya hizi remote za kingamuzi chenu kuchanganya mpangilio wake mfano

Unabonyeza button ya kuongeza sauti unashangaa imebadili channel haya unabonyeza button ya kubadili channel unaona inaongeza saut hii kitu nilijua kwangu tu lakini nilipoongea mdau ambaye naye anatumia kingamuzi hicho akasema hata yeye hiyo hali hutokea hivyo sasa jamani tatizo nini mwaka Wa tatu huu ndio naanza kuona mapicha Picha haya nini tatizo

Ni kweli kabisa unachoongea hili ni tatizo

Lakini pia kwa watu ambao wanaishi sehemu zenye mvua nyingi hikikingamuzi hakifai kabisa, kwani wingu tu picha hazionekani. Na shida hii imekuwa yamuda mrefu na imelalamikiwa sijui kwa nini Azam hawatoi majibu au suluhisho. Biashara hii ni ya ushindani, leo kuna DSTV, Star times, Continental , Zuku, n.k. Hakuna mtu atakayelipia fedha zake akawa hapati huduma na akaendelea kuvumilia. Azam wakati wa kuchua hatua ni huu, tusisubiri wateja wakishahama ndiyo mtafute suluhu ya matatizo. Uwekezaji mliofanya ni mkubwa sana na shida ndogo ndogo kama hizi hazitakiwi kuwaharibia biashara
 
Kirimoti changu cha Azam kimetafunwa button zote na mtoto! Hata hivyo kilishaanza kuzingua!
 
Remote mpaka ugusishe kwenye kingamuzi otherwise huwezi kubadilisha chochote
 
Hata mimi nyumbn kwangu tena king’amuzi hakina hata mwezi jamani…Remote haifanyi kazi vizuri
 
Wakuu nahitaji remote ya azam na ya kudumu sio hizi feki nimechoka aisee
 
Heshima kwenu wadau

Lengo ka uzi huu si kuwaharibia biashara azam Tv lengo ni kutaka kujua tatizo gani ambalo linafanya hizi remote za kingamuzi chenu kuchanganya mpangilio wake mfano

Unabonyeza button ya kuongeza sauti unashangaa imebadili channel haya unabonyeza button ya kubadili channel unaona inaongeza saut hii kitu nilijua kwangu tu lakini nilipoongea mdau ambaye naye anatumia kingamuzi hicho akasema hata yeye hiyo hali hutokea hivyo sasa jamani tatizo nini mwaka Wa tatu huu ndio naanza kuona mapicha Picha haya nini tatizo
e
 
Mimi ilinishinda Sasa natumia ya Star times kubadilishia decoder ya Azam
 
Back
Top Bottom