Matatizo ya Meno | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matatizo ya Meno

Discussion in 'JF Doctor' started by kholo, Sep 30, 2012.

 1. kholo

  kholo JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 411
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ndugu wana jf, habarini za kutwa nzima! kwanza kabisa naomba niwapongeze kwa majukumu ya uelimishaji humu jamvini. ama baada ya salam naomba msaada wako wewe mdau wa jamvi hili namna n'takavyoweza kutatua hili tatizo;
  Tatizo kuu nililonalo in "MENO", yanatoboka pia yanauma hivyo naomba mnisaidie nifanyaje ili kurecover maana mengine
  yamechimbika kiasi kwamba hata kung'oa haiwezekani, ama unamfaham daktari au hospitali ye yote spesho kwa magonjwa ya meno basi naomba unifahamishe. Natanguliza shukrani wakuu wangu
   
 2. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,862
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Dawa ya Meni ni Kung'oa Muone Dr. Akim 0754-262280

  Ana huduma nzuri sana yupo Msimbazi Street karibu na kituo cha mabasi yaendayo Muhimbili niling'oa na sikusikia maumivu na alinipa dawa kila baada ya masaa sita nameza kwa siku mbili zote sikusikia hata tone la maumivu... yaani maumivu niliyopata ni yake ya sindano ya ganzi tu....

  Meno yote yanangoka hata kiwe kipande... ila nilisikia Meno ya Juu yakitolewa vibaya unaweza poteza hata maisha....
   
 3. Victor Kisanga

  Victor Kisanga Member

  #3
  Sep 30, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna tunda linaitwa ndulele wengine wanaita ntulantu ukilipata hili yachukue kama kumi hv yaliyoiva(njano) then yachemshe upate supu yake kisha changanya na matone matano ya mafuta ya taa baada ya hapo safisha meno yako vizuru uhakikishe hakuna mabaki ya chakula kwenye matobo then sukutua hyo dawa, fanya asubuh na jioni na uhakikishe meno yako hayashindi na mabaki ya chakula ndani ya cku tatu utaona mabadiliko makubwa sana hata mimi nimesumbuliwa sana na meno ya kutoboka ila baada ya kutumia hyo dawa nimepona kabisa huwez amini
   
 4. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Kuna dawa nzuri sana ipo pale Natural Therapy Center(adjacent na Hindu mandal) inaitwa RANOS.Ni Nzuri sana kwa meno na mie nishawahi kuitumia na sisumbuliwi na meno.Nakushauri ijaribu..
   
 5. M

  Mjasiriamali1 JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,318
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Meno kutoboka. Au kupata ganzi,ukipigwa upepo meno yanauma, maji ya baridi yanauma,maji ya moto yanauma. Kitaalamu ni tatizo linalosababishwa na kuondoka kwa tabaka la juu la meno. Inayosababishwa na sumu iliyopo ktk dawa nyingine zilizo na floride. Hii inaweza mtokea mtu yoyote anayetumia dawa za mswaki zenye floride. Nilimshauri mama angu mzazi aliyekuwa na tatizo hili pamoja na mdogo wangu. Wameacha kbs kungoa meno. Nilipatia absorbent c na aloe brightooth gel. Ka unahitaji ushauri call me 0713297066. Sina mda wa kuandika hapa sana.
   
 6. M

  Mundu JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Nilitumia Aloe bright tooth gel na meno yangu yalikuwa meusi kama ninaye vuta fegi... Kama mwezi umepita natumia Sensodyne..yaani yanang'aa kama fedha!! Ila nakubali kuwa aloe b toothgel ni kiboko ya meno mabovu na ganzi ...Tatizo ni hilo tu la meno kubadilika rangi
   
 7. kholo

  kholo JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 411
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ahsante mkuu kwa ushaur wako japo n'likuwa nahitaji namna ya kutibu na c kung'oa maana nimeng'oa mpaka yameisha sasa
   
 8. kholo

  kholo JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 411
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ahsante kwa kunidadavulia maana nilishawahi isikia hii kitu ila sikuwa najua formular ya kutengeneza. Je, kila siku utakuwa unachemsha mpya au?
   
 9. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,862
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Ok Mkuu Huyo Dr. anahuduma zote za meno unaweza ngoa na kuweka ya bandia mkuu... ila hiyo ya Ndulele ndio leo naisikia kwani na mimi ningekuwa nishaijarubu b4.... yaani tanzania hatuna watu wakaithibitisha kisha kuipaki vizuri kama Colgate...

  Mkuu pia nimekumbuka Dawa ya kusafishia meno ya Sensodyne naypo ni kiboko ila kwa bei ipo juu... ila inamatokeo mazuri sana
   
 10. k

  kingmajay Member

  #10
  Oct 2, 2012
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Tiba ya jino ni kung'oa", huo ni msemo ambao huko mtaani na hauna maana yoyote. Jino linaweza kutibiwa bila ya kung'olewa, kuna hospitali hapa Dar (kwa mfano Muhimbili, Temeke, Ilala, Agakhan) zinatoa huduma/tiba ya meno bila kung'oa. For more information, tembelea hospitali, onana na daktari wa meno (dentist), atakushauri nini cha kufanya.
   
 11. kholo

  kholo JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 411
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  ok! ahsante, ngoja nikamtafute kisha nitakuja na majibu
   
Loading...