Matatizo uliyowahi kukutana nayo kwenye daladala

Matatizo uliyowahi kukutana nayo kwenye daladala

sky walker

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2018
Posts
1,160
Reaction score
834
NAZUNGUMZIA BASI NA DALADALA KWA UJUMLA:

Mimi binafsi nimekutana na majanga kibao na sio moja kama:

1.Kusafiri kutoka Dar kuja Arusha tumbo lilinisubua sana.

2.Kuibiwa mp3 ya bei kiasi enzi hizo.

3.Kupanda gari kwa kujiamini kumbe nimesahau wallet nyumbani na Konda alikuwa mtata vibaya.

4.Kushikwa nyeti na mama mmoja kimya kimya baada ya kupiga story mbili tatu na ilikuwa usiku na ni baada ya kumuwekea mkono begani na ku msogelea huku tukiangalia video za insta (kisa kaniuliza umeoa nikasema hapana bado bado nakula bata)

5.Kupitiliza kituo.

6.Nilikunywa bia nyingi siku hiyo nikaanza safari na gari ndo ilikuwa ya mwisho mkojo ukanibana nikashindwa kuvumilia nikashuka kukojoa konda bila hiana akagonga gari isepe nikabaki uchira. DHAA
 
Halafu sipedagi mtoto aliyevalishwa hirizi,,,siku Niko kwa gari nikamsaidia mama mtoto kumbe kavaa bonge la hirizi bana mkononi,,,weeee nilihaha ili watu wajue sio wangu,,kila saa najisemesha mama yuleeee,,,huku nazuia niliniguse,,
Hahahaha..



Hahaha ila una vituko. Afu hapo ndio ukute toto limekupenda halimtaki mama yake tena.
Mimi mtu akinipa mwanae ambaye ana hirizi simbebi labda nimshike kwa sekunde tu.
Na wanangu hiriizi nope
 
Nakumbuka zamani fulani nimekaa siti ya kati afu nyuma yangu wamekaa wadada 2 wamevaa ninja, basi mmojawapo akanipa simu yake nikataka kuuliza kitu nikasita kwanza!kuangalia ktk skrin ameandika naomba namba yako. Nikamuandikia nikampa simu yake! Baadae ananipigia hiyo sauti sijawahi iskia toka dunia imeumbwa!

Duuuhhh akaniambia njooo sehemu fulani tuongee hata hajakata simu nimeshafika!aseee sijawahi kuona limama bomba kama hilo huo wanja na mahina yamepakwa kila mahali.

Duuuhh yaani tunaongea mi nimedisa tu mda wote!asee lile limama kesho yake likanipa mzigo!si nikaliganda aseee nikawa km nimechanganyikiwa vile!siku hiyo akaniambia anasafiri nikamuuliza wapi!eti yeye anaishi baharini mi nikajua bahrain kule arabuni.likaniambia mi ni jini!!!aseee usain bolt chamtoto!nilipotea kama mzuka vile.dissapear like ghost
 
Halafu sipedagi mtoto aliyevalishwa hirizi,,,siku Niko kwa gari nikamsaidia mama mtoto kumbe kavaa bonge la hirizi bana mkononi,,,weeee nilihaha ili watu wajue sio wangu,,kila saa najisemesha mama yuleeee,,,huku nazuia niliniguse,,
Weweee jamaaa hayaa bana!!!!
 
Nakumbuka zamani flani nimekaa siti ya kati afu nyuma yangu wamekaa wadada 2 wamevaa ninja.basi mmojawapo akanipa simu yake nikataka kuuliza kitu nikasita kwanza!kuangalia ktk skrin ameandika naomba namba yako.nikamuandikia nikampa simu yake!baadae ananipigia hiyo sauti sijawahi iskia toka dunia imeumbwa!duuuhhh akaniambia njooo sehem flani tuongee hata hajakata simu nimeshafika!aseee sijawahi kuona limama bomba kama hilo huo wanja na mahina yamepakwa kila mahali.duuuhh yaani tunaongea mi nimedisa tu mda wote!asee lile limama kesho yake likanipa mzigo!si nikaliganda aseee nikawa km nimechanganyikiwa vile!siku hiyo akaniambia anasafiri nikamuuliza wapi!eti yeye anaishi baharini mi nikajua bahrain kule arabuni.likaniambia mi ni jini!!!aseee usain bolt chamtoto!nilipotea kama mzuka vile.dissapear like ghost
hahahahaha UONGOOOO we jamaa
 
Kipindi hicho kuna hiace za kutoka mwananyamala kwenda posta.

Nikapandia pale mwembe jini, hapo gari imeshajaa. Nikaingia wa mwisho mpaka mlango kufunga ilikuwa shida.

Kumbuka hapo ni asubuhi na mbele kuna foleni. Ghafla mdada aliyekuwa mbele yangu akajigeuza na hamadi makalio yake yakaja sambamba na dushe.

Dah ile safari ilikuwa ndefu sijawahi kuona. Nikaja kugundua ni kwanini wanaume wengine humaliza mambo kabisa kwenye daladala. Yule Dada alikuwa na makusudi mpaka leo huwa namwaza alikuwa anataka nini.
 
Kuna siku bado kidogo nipigwe..gari ilikua nyomi nataka kushuka naomba kupita watu kama hawasikii vile..hakuna hata wa kusogea..nilichofanya nilipita kinguvu uku nawasukuma na kuwakanyaga na nlivyo bonge walijuta
 
Kuwekewa kwapa kwenye pua

Ukiwa mfupi ni tabu kuna siku mbaba ameniwekelea kwapa lake kwenye pua yangu,yaaani nilikuwa naona kiza kama nakata roho,

Siku nyingine daladala za gongola mboto nikaingilia dirishani kuna mkaka akanivuta kwa ndani....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom