Chiqa
Member
- Jul 19, 2017
- 80
- 171
Salaam,
Baada ya kuwaza sana na kuwazua bila kupata suluhisho la changamoto ninazopitia kwa sasa nikakumbuka kipindi nipo kambini JKT, nakumbuka afande mmoja mnoko alituambia maneno ya ajabu sana siku hiyo ila mwishoni akamalizia kwa kusema " mimi siwajui nyie, sijui mlipotoka na hata sijui mtakapokua kesho tumekutana kambini hapa na mtaniacha sina sababu ya kumchukia mtu na wala sina kinyongo na yeyote yule ila mazoezi tunayotoa ambayo nyie mnaona ni adhabu ni kwa ajili ya kuwaandaa muwe wakakamavu na wavumilivu pindi mtakapo kuwa vitani ama mkirudi uraiani msiwe waoga wa kujaribu na msiogope kushindwa" baada ya hapo akatupiga nua na doso la maana.
Nilichoelewa ni kwamba ukiwa jeshini wanakutengenezea mazingira ya vita ili utakapokuwa vitani usishangae wala kuzubaa maana ni mazingira ambayo kwa kiasi fulani unayafahamu.Hii pia inafanana kabisaa na maisha tulionayo.
Matatizo yanafanana kwa kiasi kikubwa sana kwa mfano; Kwa sasa mimi sina ajira najua kichwani kwako unaweza kwanini nisijiajiri lakini mpaka hapa nilipo nimeshajaribu kila njia kupata mtaji wa biashara au kujiajiri kwa njia yoyote ile ninayoona inafaa imeshindikana, najua kuna mtu mwingine anatatizo kama langu ama ameshapitia na kulitatua, kuna wengine wanauwezo mkubwa sana wa kutatua changamoto zinazowakabili bila tabu ila kuna wenzangu na mimi inakua ngumu sana kutatua changamoto fulani.
UZI HUU ni maalumu kwa yeyote yule atakaeguswa kutoa ushuhuda wa jambo lolote ama changamoto yoyote aliyowahi kukumbana nayo kwenye maisha ya kila siku na jinsi ambavyo alitatua changamoto ile ili iwe msaada kwa vijana wengi tunaokua bila malezi ya wazazi wa kutushika mkono kutuongoza ama watu wa kutupa ushauri tunapokumbana na matatizo.
NINGEPENDA TUZUNGUMZIE CHANGAMOTO ZA KIUCHUMI kwa mfano nini ulifanya ulipokosa ajira, Jinsi ya kukabiliana na stress za umaskini, KIELIMU kwa mfano ni changamoto gani ulipitia wakati unasoma, KIJAMII kwa mfano. Matatizo ya akili kama msongo, sonona na jinsi ya kukabiliana nayo, Changamoto za kimahusiano n.k.
Karibuni jamani