Matapeli wa simu mtandaoni

Oct 20, 2019
61
76
Jioni ya Leo nimetapeliwa na mtu anasema yuko Tigo Pesa Makumbusho katuma kimakosa kwangu Tshs 240000.00 akaomba nirudishe kwa namba 0718 89 56 66 na namba 0768 53 61 39 majina ni Beatrice na Lucy Sawa. Baada ya hapo kutuma Ile hela sikuwapata tena.

TCRA kama kusajili namba kwa njia za kisasa, hawa MATAPELI wanatoka wapi tena?
 
Hivi bado kuna watu wanatapeliwa kwa njia hii pole..

Kuna mmoja alinipigia kuniambia habari kama hizo nikamjibu mbona tunafanya kazi moja halafu tunaingiliana magepu inamaana tumeanza kupigana wenyewe kwa wenyewe na wakati tunafanya kazi moja akacheka akanijibu ah! Sikujua tunawapata watu wengi tofauti basi twendelee kupiga kazi inakawa imeisha hiyo!
 
Kimsingi wewe ndio umejitapeli.Utamtumiaje mtu pesa bila kuhakiki kama ni kweli? Uliona ana namba mbili hushtuki halafu hata kumdodosa kidogo.
kimsingi ni kwamba nimeweka fedha kwa ajili ya kununua umeme,nikiwa kwenye harakati msg unaingia ya muamala mara simu inaita kupokea huyo mtu anasema mteja wake katuma fedha kimakosa na tigo wamefunga line yangu siwezi toa fedha hadi nimerudisha hiyo fedha.kufanya hivyo ndiyo nimeibiwa jamani.
 
Kwahy mkuu sms kutoka tigo na sms kutoka kwa mwenzio hujui hahaha nawe ni mshamba kwel kwel hongera kwa kuwapa ada wenzio hahaha
 
Hata hukuangalia salio? Kuna watu mna hela aisee
Hata haja ya kucheki balance haikuwepo.Message za miamala kwenye simu yako zinaingia kwa jina la M-pesa,Tigopesa,AirtelMoney n.k.Ila mtu akikufanyia huu mchezo hiyo SMS ya muamala itaingia kwa namba ngeni kwenye simu yako.
 
Back
Top Bottom