Matapeli QNET



Ukimleta mtu mmoja na yeye akimleta mtu , huku tayari wewe utakua unaingiza laki mbili kwa wiki.

Na kazi hii unaifanya online ata ukiwa nyumbani
 
Mimi mwenyewe nilishangiliwa , jamaa aliye ileta aliniambia Kuna mchongo nikafika kwenye hio nyumba waliokodi tukawa tunaangalia live kwenye Tv mkuu wa Qnet akihutubia .

Nikakaribishwa vizuri na nikapangiwa siku ya kuja tena , jamaa aliyenileta aliniambia at least niwe na laki 2 Faida nje nje , nilivyorudi tu jamaa nikawa sipokei simu zake niliona kama mchongo wa kitapeli
 
Lakini si tayari wanajulikana kuwa ni matapeli.sasa kwanini serikali ina waangalia tu bila kuchukua hatua zozote.?
 
Wajinga wengi ni wasomi na walipigwa hasa
Mkuu darasani unafundihswa phloem na Xylem ya kwenye mmea,

Ukifunika daftari hilo anaingia mwalimu mwingine anakufundisha Mass flow, coral reef, na contour za geograph,

Ukifunika daftari unakusanya anaingia mwingine anakufundisha Mean,Mode na Meridian

Akisepa anaimgia mwingine anakupa taarifa za tabia za elements za group seven, mara hallo, hellena, lile, beberu, bora, sijui chinja n.k, anasema mm ni mwalimu wa Kemia anaondoka.

Anaingia mwingine anasema tufungue ukurasa wa 40 tuelezee madhara ya Mapenzi kwa jamii ukizingatia alichokifanya Ngoswe na Mazoea

Hujakaa sawa unaambuwa ni kipindi cha Historia na leo tujadili Ngoni Movement and Effects of Shark Zulu

Unamalizia na mwalimu wa Physics anakuambia Density ni Mass per volume

Je katika Masomo yote hayo wapi umefundishwa kuhusu mambo ya utapeli wa Duniani?
Wapi umekuwa xposed na hali kama hiyo shuleni?
Kwanza shuleni unafunzwa kuaminiana, utii na heshima muda wote.

Kwa hiyo ndio maana hata maprofesa walilizwa kwa maana hayo mambo ni elimu ya kitaa sio shule.

Na ndio maana hao unosema wasomi wamekuwa wahanga zaidi.
 
Qnet ni matapeli kama Forever Living walivyo matapeli.

Ukiitwa kwenye issue ambayo wanakwambia ni DILI basi jua wewe uliyeitwa ndiyo DILI lenyewe.
 
Kuna hawa wamepiga watu juzi juzi, kama sio 2022 basi 2023, walikuwa wana mpaka App zao, withdraw ikagoma, ikaishia hivyo
 
Hata iwe mchana utasikia
Good morning future millionaire
Mi kuna mwanangu alikujaga na huo mchongo sijamchelewesha hata sekunde kama hao ni matapeli kama matapeli wengine kuwa makini daslam hapa ni uwanja wa fursa
Eti Good Morning future millionaire 😂🤣🤣
 
Enternal na madawa Yao. Wanatupiga haswa kupitia wazee wetu. Kidogo tu tuma laki nne ya dawa, na bima anayo kumbe enternal.
 
Na wanajua kuongea hatari, wakianza kuongea unajua hela hizi hapa, kuna mwanangu alinipeleka pale makumbusho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…