Matapeli QNET

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ duh
 
Huwa nafurahi sana wasomi wanapotapeliwa kindezi. 😁
Enzi za chuo kuna manzi alitoa $ kibao sijui kwa kampuni gani, aliachiwa mavipodozi, masabuni sabuni, madawa dawa kibao auze, sisi tukawa tunamchora tuu. Mara semina, warsha, makongamano, safari za huku na kule huko kote wanamkamua hela tuu. 😊
Mwisho wa siku yeye mwenyewe akaja kuona wazi alitapeliwa.

Kanuni; Mtu akiwa anatapeliwa (anapagwa) usimsanue/kumstua atakuchukia sana. Hapa JF wakati watu wanapangwa na Ontario tuliwasanua ikafika kipindi mpaka wakatu ignore humu. Wakaja kulizwa hawana hamu. Wamebadiri na IDs. 😊
 
Duuh
 
Sijui kwanini mtu akiwa anatapeliwa ukimshauri huwa mkali sana
 
Huyo dada hakutapeliwa mana aliachiwa bidhaa πŸ˜‚

Acha watu wanyooshwe, sasa wngn wataishi vp
 
Sijui kwanini mtu akiwa anatapeliwa ukimshauri huwa mkali sana

Mtu anaetapeliwa ni sawa na mfia dini (martyr). Ukijaribu tuu kumshauri kwamba anapoelekea sipo, basi atakuchukia hatari.

Kuna maza mmoja mwalimu kitaani, miaka ya 2014. Alianza kuwa beneti na madogo ambao mimi najua ni madii (maprofesa). Kila siku wanamshusha na gari home kwake, na home lazima apite maskani kwetu. Kuna siku nikamkuta benki, nikamuuliza mama wale vijana unakua nao una biashara gani nao?
Mama alinifokea sio kidogo, alinisuta pale benki mpaka nikaona aibu. Bahati ilikuwa nje ya benki.
Kumbe maza alikuwa yupo mwishoni kustaafu. Wale madogo walikuwa wameanza kumpanga, wakijua bimkubwa anaenda kupata hela.
Nikasafiri, nilivyorudi home nikakuta stori kwamba, mama alistaafu akapewa karibia milioni 80, akawapa watu wamnunulie gari ya kutembelea na kumtafutia nyumba kama madalali.
Walimpiga kama 30m hivi ya kumuagizia gafi na kumtafutia nyumba ya kununua. Wakatembea na mji wakahaman mpaka leo kimya.
 
Na sijawahi sikia wakikamatwa kwa kutapeli watu!

Utapeli huo unakuwa ni wa kuaminiana. Ni ngumu sana polisi kufungua jalada mahali ambapo ulitoa hela kwa ridhaa yako na mwisho wa siku watu wakatokomea. Mtu anakuja anakuonyesha mawe anakwambia no dhahabu, unatoa hela unabaki na mawe. Siku unaenda kuyauza unapigwa makofi. Utaenda polisi kufanya nini hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…