Matapeli QNET

Scott junior

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2022
Posts
3,509
Reaction score
5,192
Mwanangu mmoja alikuwa anasoma Muhimbili MD, yupo mwaka wa pili. Sasa wakati mimi napiga zangu field pale Sinza Palestina, siku moja kwenye pita-pita zangu nikakutana naye. Mawasiliano tukapiga story nyingi, maana kitambo hatujaonana. Nikamwambia, “Weekend moja nitaenda kukusalimia Campus yenu ya MUHAS kule Chole Road.”


Siku hiyo nimeenda, jamaa akaanza kunipa michongo ya ujasiriamali na kampuni wanaiita QNET 😅. Akanipa ramani nzima ya sehemu walipo, akaniambia kesho niende kwa ajili ya interview ya kwanza. Walikuwa wamekodi nyumba fulani pale Sinza Kijiweni.


Kesho yake nimetoka zangu hospitali Sinza, pale mida ya saa 8 mchana. Nikamcheki mwanangu, twende kwenye hiyo interview. Akanielekeza mpaka tukafika eneo la tukio.


Ile nafika tu, napokelewa na “Good morning.” Nikashtuka, sikuelewa nijibu nini 😂. Halafu wananiita kwa jina langu! Mwanangu akasema, “Usiwe na wasiwasi, ndo salamu za kampuni hizo.”


Sasa akanikutanisha na boss wao. Nilipomwona tu usoni nikamkumbuka, kumbe tumesoma naye Pandahill. Basi tukaenda ofisini, akanipa maelekezo kibao. Mara sijui QNET wameidhamini hadi Man City 😂.


Kisha baadaye akaja kusema, “Hii ni interview ya kwanza. Kesho muda kama huu huu uje kwa ajili ya interview ya pili, ambayo ndiyo utasajiliwa na kuanza kulipwa.”


Natoka tu nje, nakuta wananipigia makofi watu kibao pale sebuleni, ambao hata mwanzoni hawakuwepo 😂. Na wengine ndio naanza kuwaona ni watu tuliosoma nao Pandahill. Wanasema, “Hongera sana!” 😂😂


Basi tukatoka na mwanangu ananisindikiza, huku anasisitiza, “Kesho hakikisha unakuja mwanangu.” 😅


Nilivyofika maskani, nilicheka sana nilichoshuhudia siku hiyo. Kesho yake mchana jamaa alipiga simu nyingi sana, sikupokea.


Urafiki ukafa.


Ila cha kushangaza, milima haikutani, lakini binadamu tunakutana 😅.


Mwaka 2023, kipindi nafanya kazi Dodoma, nikaja kukutana naye UDOM. Yupo mwaka wa pili tena MD kule Muhimbili, alifeli 😅.


QNET imeharibu ramani za maisha ya vijana wengi sana.
 
Good morning young millionaires. Jamaa limepiga upatu halafu limesepa)limesepeshwa. Wajanja wamebaki na noti huku wengine wakiugulia maumivu .
 
Hili kampuni huku kwetu sijui inakuaje, kweli kwenye mechi nyingii tu za epl naonaga matangazo kibao pale yanapita na ni miaka nenda rudi huko ulaya ipogoo tu ila huku kwetu pasua kichwaa....mimi jamaa nilipiga nae advance tukakutanaga muhas yeye akiwa hapo mimi nikiwa udsm....hawa walikua pale makumbusho stendi kwa nyuma hivii salamu zao kama kawaida....mchana jua kali ila good morning kama zotee.....sikupokeaga simu zake baada ya hiyo meeting ya kwanza nilivoendaga😰
 
Wao wenyewe wana maisha magumu
Ugali na dagaa za jero mnashindia
 
Sijui hawa jamaa wapoje kwa hapa Tanzania, mbona wanadhamini michuano ya CAF na club ya Manchester City lakini hapa Bongo wanabamizana sana 🤣

Kuna jamaa yangu alitoa 2 milioni akapewa saa ya mkononi sijui kulikuwa na nini kinaendelea behind

Kuna siku jamaa akaniambia mkuu wa QNET kanda ta Afrika anakuja kutakuwa na meeting Coral Beach Hotel Masaki. Cha kushangaza walikuwa wanakula Ma apple na maji tu halafu hata walichokuwa wanaongea ni broken tupu

Vijana wengi walikuwa wamevaa visuti kama vya kina Diamond platinumz na walikuwa wanajiona mamilionea kumbe kanyanga tu 😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…