Bata batani
JF-Expert Member
- Nov 11, 2011
- 3,256
- 3,892
wakuu kama kichwa cha habari kinavyojieleza mara nyingi nikipata wasaa wakusikiliza radio one hasa mida ya mchana, kwenye matangazo ya vifo kinachonishangaza ni kwamba majina na watu niwasikiao wamekufa ni wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha tu. Tena hasahasa kilimanjaro.
Sio kwamba lazima wawe wanaishi huko bali hata kama wanaishi mikoa mingineyo. mathalani jana nikiwa kwenye daladala mwanzo hadi mwisho wa matangazo hayo ni watu wa jamii ya huko.
Maswali:
1. Watu wa kanda nyingine hubaguliwa wakipeleka matangazo yao?
2. kuna gharama nafuu/priorities kwa jamii ya huko?
My take:
Si kuleta mgawanyiko, matusi au kebehi. Tujadili kwa amani na kuelimishana.
Nawasilisha.
Wadau kama kuna mtu huwa anasikiliza kipindi cha matangazo ya vifo cha Redio One kinachorushwa saa saba na saa kumi baada ya taarifa ya habali ila kinachonishangaza kila siku watu wanaotajwa wote wafiwa, marehemu na misiba ni watu wa Kaskazini.