Rejea mada yangu viziri...wewe unaona ni sawa kutumia milioni kumi kwenye matangazo wakati kuna watoto wanakaa chini?halafu matangazo yenyewe yanamlenga mtu anayelala njaa?
Hwezi kuweka chombo cha kudhibiti matangazo ya kampuni binafsi.Kampuni bila kumarket product zake haziwezi kujulikana wala kununulika.Serikali kuwa na chombo cha usimamizi haimaanishi kuingilia kampuni binafsi.
Sio Sawa mkuu?ni lini niliwahi kusema haya ni sawa?Mkuu kama kila mmoja anesimama vizuri kwenye nafasi yake wala hali isingekua mbaya kiasi hiki.
Wewe unaona sawa kampuni kulipwa zaidi ya asilimia 90 kwa kazi ambayo haikufanyika tena kwa ukiukwaji mkubwa wa kanuni za manunuzi?
Unaona ni sawa tuhuma kubwa kama za escrow na epa kuendeshwa kisiasa zaidi kuliko kujali maslahi ya wananchi? Unaona ni sawa kivuko kibovu kununuliwa kwa bei kubwa isiyona tija na wahusika wapi kimya?
Huko unakopendekeza pesa za makampuni zielekezwe kusaidia kumeoza, pesa zitaenda na zitapigwa tu. Hayo mambo yanawezekana tu kukiwa na uwajibikaji na uzalendo. Acha makampuni yafanye kazi zao mkuu.
Nami bado nashangaa maana ya hili bandiko lakini siipati.!Yaani Kuna watu wengine wanaanzisha uzi humu, unajaribu kupata picha ya huyo mtu yukoje na akili yake inafanya kazi kweli? Na elimu kweli anayo? Yaan mm Nina biashara yangu, kampuni yangu, hela zangu! Halafu eti uje unipangie eti nisitangaze? Kwa lipi? Labda kama hayo matangazo yanakikuka maadili. Lakini vinginevyo hamna....
Sawa.!Utakuja kuielewa siku mamlaka hii itakapoundwa
Dah! Mkuu wangu Richard cjakusoma, it's a if nimeamka na hangover!Mimi nakuelewa kamanda Chige, sidhani kama mleta mada atakuwa nawe.
Na hata ukitaka uwafikie Wahadzabe kuna mambo mengi kama logistics na malazi, chakula na vingine.
Lakini yeye ameoanisha kati ya matumizi ya hiyo pesa na kodi inayolipwa.
Sifahamu lengo lake hapo.
Ila matangazo yako ya aina nyingi ila yanayowika Zaidi ni haya ya matangazo ya kupitia media au "advertising messages" yaani kuanzia magazeti redio, runinga mpaka blogs na text messages.
Halafu kuna haya matangazo ambayo nafikiri ndiyo yanawika sana nchini kwetu ya commercial ads abayo yana lengo la kuongeza idadi ya wateja kwa kupanua huduma na na bidhaa yaani unafungua duka la na hapo hapo unagawa simu mbili tatu za bure na hii ndio inaitwa "Branding" yaani mteja anatumika na anatumiwa hapohapo kukuza jina la kampuni.
Sasa mara nyingi kunakuwa na sponsors kwa hii shughuli je sponsors huyu anafahamu gharama halisi ya shughuli za matangazo haya.
Nafikiri utanielewa kamanda maana wewe unaonekana unao utaalam wa hili eneo.
Hizo ni private sector.Zipo kwenye ushindani wa kibiashara
Lakini hizi fedha za matangazo si ni za kampuni husika?
Hizi fedha hazihusiani kabisa na fedha za walipa kodi.
Kwanza, mfano wa huo mtambo wa simu hapa haungii cuz' one is illegal practice and another ni legal practice! Ingekuwa mada ya possible practices za ukwepaji kodi tungeenda pamoja-- for instance, ikiwa unaona wanafanya massive contributions kwenye useless issues!Una utaalaamu kwenye hii field ...huko siji...labda nikuulize swali ...je ulisikia lile sakata la kuzimwa mtambo wa kutambua idadi ya miito au huduma za simu?
Ilionekana jambo hilo limefanyika makusudi ili kuidanganya serikali na hivyo kukwepa kodi.
Mada yangu inalenga huu ukwepaji kodi halafu tunashuhudia a lot of investment kwenye matangazo ambayo kwa maoni yangu hayana kiwango cha thamani inayolipiwa.
Ni kweli wajibu wa kwanza wa kuhakikisha madawati yapo shuleni unamuhusu serikali lakini pia wajibu huo upo kwa wadau mbalimbali makampuni haya yakiwemo....yaani makampuni haya yarudishe sehemu ya faida ya uwekezaji kwa jamii.
Kuboreshwa kufikia kiwango cha kimataifa au kutengeneza matangazo bora? Listen, people invest money to design yale matangazo kwahiyo lazima uhakikishe una design catchy ads ili ku-grab attention!!
Na hiyo unayoita matangazo ya kila siku; ningekushauri jiongezee maarifa kwenye kitu kinachoitwa Product Life Cycle! And am telling you, endapo kampuni za kibiashara zingekuwa na namna ya kukwepa marketing basi wangeshukuru ile mbaya cuz' marketing ni very expensive sema ndo vile haikwepeki in competitive environment!!
Halafu hizo habari za madawati na hospital kukosa dawa zinawahusu nini business firms? Provision of social services ni purely kazi ya serikali lakini sio ya Tigo wala Vodacom! Serikali si wanakusanya kodi? Hata hayo mapesa mengi yanayotumika kwenye matangazo si yanaenda kwenye other business entities ambako pia serikali inakusanya kodi?! Sasa how come tena ionekane uhaini mimi kuwafikia wateja wengi niwezavyo kv tu wewe serikali ( don't take it personal) umeshindwa kutimiza wajibu wako wakati wajibu wa kwangu mimi wa kukulipa kodi nimeshautimiza! And probably, on top of that nina corporate social responsibility program na kujitwisha majukumu uliyotakiwa kufanya wewe! Kama kodi haitoshi, the smart way sio kuniambia ni namna gani niwafikie wateja wangu bali nI wajibu wako wewe mwenyewe na timu yako kubuni vyanzo vingi zaidi vya mapato!
Naona unataka kuhamishia lawama kwenye Broadcasting na media companies ...nashukuru umeikumbusha serikali kuhusu kuifuatilia hii aina ya kodi ambayo naamini haitozwi na ndio maana makampuni haya yanajiachia.....Kwanza, mfano wa huo mtambo wa simu hapa haungii cuz' one is illegal practice and another ni legal practice! Ingekuwa mada ya possible practices za ukwepaji kodi tungeenda pamoja-- for instance, ikiwa unaona wanafanya massive contributions kwenye useless issues!
Lakini linapokuja suala la marketing, that's another issue. Unachosema ni kwamba wanafanya investment kubwa kwenye matangazo wakati matangazo yenyewe hayana kiwango cha thamani inayolipiwa! What are you insinuating here? Kampuni za simu kwa mfano zinategemea communication channels owned by other business entities! Ikiwa umeenda na tangazo lisilo na viwango pale ITV that's your problem lakini ITV watakupa quotations za gharama za matangazo kwa majira mbali mbali throughout the day-- kwa sababu, gharama ya tangazo linalorushwa saa 5 asubuhi ni tofauti na gharama ya tangazo linalorushwa saa 2 usiku; keeping airtime ya tangazo constant! Hizi gharama haziwekwi na Tigo au Vodacom bali na ITV au Clouds FM! Sasa utasemaje wanatumia gharama kubwa? Ndo maana tangia mwanzo nimekuambia labda useme watumie media chache zaidi badala ya tangazo hilo hilo kupeleka in more than 1 radio stations kwa vipindi mbali mbali hali kadhalika iwe hivyo upande wa tv! Hata hivyo, narudia... lengo lao la awali hapo ni kufikia audience kubwa zaidi kwahiyo huwezi kumwekea barriers za kufanikisha goal yao ya awali! But all in all, kama issue ni kodi mbona hili jambo lipo wazi kabisa... Kampuni X (say) inakwepa kodi kwa kutumia 5 billion kwenye matangazo ambazo wanazilipa kwa Kampuni Y! Sasa tatizo lipo wapi? Zifuate hizo 5 billion kwa kampuni Y ukazitungue kodi ambayo ingelipwa na X... simple!