Matangazo ya makampuni ni anasa katika nchi yetu masikini!

Matangazo ya makampuni ni anasa katika nchi yetu masikini!

Sidhani kama kuna umuhimu wa kuendelea kudanganywa kupitia kitu kinachoitwa matangazo since that matangazo mengi yamejaa chumvi nyingi za uongo na hadaa.
labda mamlaka zipige faini kampuni zinazotangaza uongo.
 
Faini inaweza kuwa approach nyingine yakupata hizi fedha...kiukweli matangazo haya hayaendani na gharama zinazotumiwa...hili ni jipu jingine!
 
Rejea mada yangu viziri...wewe unaona ni sawa kutumia milioni kumi kwenye matangazo wakati kuna watoto wanakaa chini?halafu matangazo yenyewe yanamlenga mtu anayelala njaa?

Labda ni simplify hivi ... Ukienda bank Kwa mfano au mikusanyiko ya watu unakuta Alama za NO SMOKING, Kwa akili ya kawaida unaweza hisi jamaa wanazuia uvutaji fegi, but the reality is wameweka pale ku market cigarettes na basically kumkumbusha mvutaji kwamba akitoka pale avute.. Ndo maana nikasema marketing is cross cutting function ..

Nirudi kwenye mada , suala la madawati ni la serikali na Kwa kuwa makampuni mengi na NGO nyingi zinajua serikali imeshashindwa basi wanatumia mwanya huo kujulikana kwenye jamii Kwa kutoa misaada ya madawati huku waki attract attention ya media, celebrities na viongozi wakubwa.. Hii ni marketing tosha... Lengo Lao ni marketing na ukisema watoe tu kimya kimya hawatakubali maana kwao itakuwa haina maana
 
Sasa Kuna jipu moja linaitwa "BAHATI NASIBU" kunasiku litatumbuliwa tu.kwa wale mliobahatika kufanyakazi kwenye kampuni zilizopigiwa mfano hapo juu n.k,alafu ukawa kwenye idara ya masoko,matangazo au promo utakuwa unaelewa naongelea nini.
wenyewe wanaita "siri ya kambi".
 
Labda ni simplify hivi ... Ukienda bank Kwa mfano au mikusanyiko ya watu unakuta Alama za NO SMOKING, Kwa akili ya kawaida unaweza hisi jamaa wanazuia uvutaji fegi, but the reality is wameweka pale ku market cigarettes na basically kumkumbusha mvutaji kwamba akitoka pale avute.. Ndo maana nikasema marketing is cross cutting function ..

Nirudi kwenye mada , suala la madawati ni la serikali na Kwa kuwa makampuni mengi na NGO nyingi zinajua serikali imeshashindwa basi wanatumia mwanya huo kujulikana kwenye jamaa Kwa kutoa misaada ya madawati huku waki attract attention ya media, celebrities na viongozi wakubwa.. Hii ni marketing tosha... Lengo Lao ni marketing na ukisema watoe tu kimya kimya hawatakubali maana kwao itakuwa haina maana
Hujanielewa mkubwa!
Mimi naongele matangazo ya kila siku ya makampuni ambayo kila iitwayo leo yanaboreshwa kufikia kiwango cha kimataifa ingawa yanawalenga watanzania asilimia sabini na zaidi wenye umasikini...ni kiasi gani wanatumia kwa mwaka kwenye matangazo ukilinganisha na misaada wanayotoa au kodi wanayolipa?
 
Nimejaribu kuangalia uwekezaji wa baadhi ya makampuni hasa haya makampuni ya simu nikaona kuwa yanatumia gharama kubwa sana.

Hii inanifanya nifikirie kuwa kuna umuhimu wa kuwa na regulatory body ya kufuatilia gharama hizi zinazotumiwa na makampuni kufanya matangazo ambayo hayana thamani na fedha inayorumika...

Ushauri wangu ni kuwa hizi fedha zinazotumika kwenye matangazo ni vyema zikaelekezwa kwenye ununuzi wa madawati ambapo tumeshuhudia kuna upungufu mkubwa.

Isitoshe makampuni haya yanawezekana kuwa yanatumia fedha nyingi sana katika matangazo badala ya kulipa kodi stahiki.

Hebu wabunge watunge sheria ya kudhibiti matumizi yasiyo na tija kwa makampuni haya ambayo yanalipa kodi kiduchu kulinganisha na wanachokipata.

kama kawaida utakuwa umepiga kitwanga maana naona mada ya kilevi
 
Huu ni mjadala wa kitaifa kwa wadau wote

Nimesema hivyo kwasababu kati ya hawa ni Vodacom amekuwa mstari wa mbele kujishughulisha na kusaidia jamii na nafikiri umeona wakiwa katika maeneo mbalimbali.

Kwa mfano walitoa machine ya photocopier kule Shimbwe Sekondari kule Moshi (mpyaaa), wanatoa mikopo isiyo na riba.

Kikubwa zaidi wana programme kubwa ambayo inaitwa Vodacom foundation ambayo inajibu suali lako la matumizi ya fedha.

Sera ya TTCL kwa hii sifahamu wamesimamia wapi.
 
Hujanielewa mkubwa!
Mimi naongele matangazo ya kila siku ya makampuni ambayo kila iitwayo leo yanaboreshwa kufikia kiwango cha kimataifa ingawa yanawalenga watanzania asilimia sabini na zaidi wenye umasikini...ni kiasi gani wanatumia kwa mwaka kwenye matangazo ukilinganisha na misaada wanayotoa au kodi wanayolipa?

Wewe vipi.hzo pesa ni za kwao wewe unawapangiaje jinsi ya kuzitumia.Na wala hawawajibiki kufanya kazi serikali.Ni utashi wao na mara nyingi wakichangia shughuli za jamii huwa ni kwa ajili ya matangazo!!
 
Hujanielewa mkubwa!
Mimi naongele matangazo ya kila siku ya makampuni ambayo kila iitwayo leo yanaboreshwa kufikia kiwango cha kimataifa ingawa yanawalenga watanzania asilimia sabini na zaidi wenye umasikini...ni kiasi gani wanatumia kwa mwaka kwenye matangazo ukilinganisha na misaada wanayotoa au kodi wanayolipa?

Ok tuwe specific sasa , mfano tangazo gani?
 
Sasa Kuna jipu moja linaitwa "BAHATI NASIBU" kunasiku litatumbuliwa tu.kwa wale mliobahatika kufanyakazi kwenye kampuni zilizopigiwa mfano hapo juu n.k,alafu ukawa kwenye idara ya masoko,matangazo au promo utakuwa unaelewa naongelea nini.
wenyewe wanaita "siri ya kambi".

Hasa mzee Tarimba Abbas akiondolewa pale, maana amekaa sana na hakuna ubunifu wowote mpya.

Watu wengi walozaliwa miaka hiyoo mpaka wanakuwa watu wazima bado wanasikia jina la Tarimba Abbas.

Hakuna CEO mwingine kijana mwenye uwezo kama anavyosema raisi JPM?
 
Nimejaribu kuangalia uwekezaji wa baadhi ya makampuni hasa haya makampuni ya simu nikaona kuwa yanatumia gharama kubwa sana.

Hii inanifanya nifikirie kuwa kuna umuhimu wa kuwa na regulatory body ya kufuatilia gharama hizi zinazotumiwa na makampuni kufanya matangazo ambayo hayana thamani na fedha inayorumika...

Ushauri wangu ni kuwa hizi fedha zinazotumika kwenye matangazo ni vyema zikaelekezwa kwenye ununuzi wa madawati ambapo tumeshuhudia kuna upungufu mkubwa.

Isitoshe makampuni haya yanawezekana kuwa yanatumia fedha nyingi sana katika matangazo badala ya kulipa kodi stahiki.

Hebu wabunge watunge sheria ya kudhibiti matumizi yasiyo na tija kwa makampuni haya ambayo yanalipa kodi kiduchu kulinganisha na wanachokipata.

Nafikiri mkuu, una hoja kwamba labda kuwepo na hiyo regulatory body ambayo itaangalia ushindani wa biashara ya matangazo.

Yaani unadhani kuwa wanachakachua makaratasi ya hesabu zao?
 
Yaani Kuna watu wengine wanaanzisha uzi humu, unajaribu kupata picha ya huyo mtu yukoje na akili yake inafanya kazi kweli? Na elimu kweli anayo? Yaan mm Nina biashara yangu, kampuni yangu, hela zangu! Halafu eti uje unipangie eti nisitangaze? Kwa lipi? Labda kama hayo matangazo yanakikuka maadili. Lakini vinginevyo hamna....
 
Duniani kote marketing costs ni pasua kichwa kwahiyo kama unadhani ni namna ya ukwepaji kodi basi duniani kote kampuni za kibiashara zinakwepa kodi kupitia marketing and advertisement... in short, ni inevitable and you can't tell any business firm to stop marketing!

Mleta mada, nadhani hili eneo la biashara si lako!

Hapana mkuu mueleweshe tu ana hoja ya msingi.

Je tunayo bodi imara inayosimamia ushindani na matangazo?
 
Yaani Kuna watu wengine wanaanzisha uzi humu, unajaribu kupata picha ya huyo mtu yukoje na akili yake inafanya kazi kweli? Na elimu kweli anayo? Yaan mm Nina biashara yangu, kampuni yangu, hela zangu! Halafu eti uje unipangie eti nisitangaze? Kwa lipi? Labda kama hayo matangazo yanakikuka maadili. Lakini vinginevyo hamna....

Mkuu, kila nchi inayo advertising standard authority ambayo inafanya kazi zake sambamba na TCRA, kusimamia Codes za utangazaji wa matangazo hayo kama zipo na kama Codes hizo zinavunjwa basi wao watu wa hiyo bodi wanaku-refer kwa TCRA.

TCRA watakuita shaurini na kama umekiuka moja ya Codes hizo basi utapigwa faini.
 
Sijaongelea kuhusu kusitisha matangazo ya biashara ...naongelea gharama zake zinazotaka kufanana na nchi zilizoendelea ..
My observation ni kwamba makampuni haya yanavuna fedha za masikini na fedha hizi hazitumiki kuwakomboa masikini hawa!
Kwani hizo gharama wanajiwekea wenyewe?! Assume kampuni imezindua new product na ku-design promotion strategy. Target market wanaona wanahitaji kufikia Watanzania wote thus attracting mass marketing! Wanaona the best way ni kutumia tv... wanaona fine but soon wanagundua si wote wana tv kwahiyo watumie radio... bado wanakuta still there's no way unaweza ku-ignore tv... kwahiyo unachanganya tv + radio! Again unakuta kuna wengine hawana muda wa tv wala radio... unaamua ku-include na billboards-- the list continues! Bado pia unatafuta njia ya ku-grab attention... unaamua kumweka Joti au Diamond only because unafahamu mtu akishamuona Joti tu; atakuwa standby kutaka kufahamu what's going on! You do all that with only one goal: to reach the largest block of your target market! Hata huko kwenye radio, unajua c wote wanasikiliza kwa mfano Clouds... so, unaamua kuhusisha na radio zingine... same to tv!

Sasa ukienda tv na tangazo lako yeye tayari ana bei zake... hali kadhalika ukienda radio, billboards na hadi Joti; yeye nae ana bei yake! Yes, you can bargain but still you've small control over it!

Sasa utaiambiaje kampuni inatumia gharama kubwa wakati nae hizo gharama anapangiwa? Labda useme wasi-utilize fully available communication channels... kwamba, ama watumie radio tu au tv tu! Kama ndivyo, hiyo itakuwa ni largest failure in marketing!
 
Mkuu, kila nchi inayo advertising standard authority ambayo inafanya kazi zake sambamba na TCRA, kusimamia Codes za utangazaji wa matangazo hayo kama zipo na kama Codes hizo zinavunjwa basi wao watu wa hiyo bodi wanaku-refer kwa TCRA.

TCRA watakuita shaurini na kama umekiuka moja ya Codes hizo basi utapigwa faini.
Off topic! Ila naomba unijuze TCRA na wenyewe waliwalalamikia coca cola kuhusu lile tangazo au ni Kenya peke yao?
 
Hujanielewa mkubwa!
Mimi naongele matangazo ya kila siku ya makampuni ambayo kila iitwayo leo yanaboreshwa kufikia kiwango cha kimataifa ingawa yanawalenga watanzania asilimia sabini na zaidi wenye umasikini...ni kiasi gani wanatumia kwa mwaka kwenye matangazo ukilinganisha na misaada wanayotoa au kodi wanayolipa?
Mkuu kwanza naomba navyo kujibu nideclare interest

As my avatar suggest, am an Adman

Ni kwamba advertising as advertising ni industry inayojitegemea, ina ajiri mamia ya vijana Wa Kitanzania ktk ajira rasmi na sisizo rasmi

Hapo tayari kuna kodi za kila rasmi zinaingia

Lakin pia hoja yako ya kwamba fedha hizi haziendani na hali halisi ya nchi, na kwamba ni kubwa

Nataka nikukumbushe tu kitu kimoja, kwamba saiv kuna Watanzania takriban M50

Kwa bidhaa ambayo unalenga walau ifikie asilimia 20% ya watanzania yaani kama 10M tu,

Ni lazima hapo utumie gharama, za kuwa shawishi na hapo ndipo advertising industry inapoingia

Hoja ya uhitaji Wa hii industry kuwa regulated ina mashiko ,lakin siyo sana sababu tayari watu Wa Fair competition, na sheria mbalimbali zinazo simamia mfano matangazo ya Sigara zinafanya vizuri
 
Back
Top Bottom