Hujanielewa mkubwa!
Mimi naongelea matangazo ya kila siku ya makampuni ambayo kila iitwayo leo yanaboreshwa kufikia kiwango cha kimataifa ingawa yanawalenga watanzania asilimia sabini na zaidi wenye umasikini...ni kiasi gani wanatumia kwa mwaka kwenye matangazo ukilinganisha na misaada wanayotoa au kodi wanayolipa?
Jingalao, kwa mtazamo wangu ni kwamba serikali inaweza ku-intervene kwa upande wa
faida lakini, sidhani kama Serikali inaweza kuingilia
expenditure ya makampuni binafsi (e.g. Tigo, Voda e.t.c) kwa namna yeyote ile....nasema hivi kwa sababu kuu mbili: Kwanza kabisa,
Marketing/Advertising ni moja kati ya nguzo kubwa kabisa katika uwekezaji ambao unafanywa na kampuni hizi.....jitihada zao katika ku-advertise huduma au bidhaa wanazozalisha ndiyo zinawawezesha kushawishi wananchi waweze kuzifahamu, kuzipenda na hatimaye kutumia huduma/bidhaa za makampuni haya na hivyo ndivyo faida inavyopatikana......kwa ufupi ni kuwa, "
The more these companies advertise their products or services, the higher the chances of attracting more customers hence high profit"....na ndiyo sababu unaona wanawekeza kiwango kikubwa cha fedha katika component hii ya Marketing.
Kwa upande mwingine, hizi kampuni ni entity ambazo zinajitegemea kwa kila kitu including namna wanavyopata mitaji na namna ya kusimamia na kuendesha shughuli zao; hata hivyo,
kila kampuni inawiwa kuzingatia sheria katika operation zake zote.....na katika hili la kuzingatia sheria inajumuisha kulipa kodi (
Ambayo ndiyo inapaswa kutumika na serikali katika kuhudumia wananchi wake katika elimu, afya, miundombinu e.t.c.), vilevile
**kisheria kampuni hizi zinapaswa kukidhi their
corporate social responsibility (
e.g. Kujenga shule, kuchangia madawati, kuhudumia makundi yenye mahitaji maalum e.t.c.) kwa jamii inayozunguka maeneo huduma inapotolewa.
Kwa mantiki hiyo Serikali ina jukumu la kusimamia sheria na kuhakikisha kuwa kampuni hizi zinalipa kodi stahiki kwa wakati na pia kuhakikisha kuwa zinadumisha na kuchangia maendeleo ya jamii zilizo karibu na eneo huduma inapotolewa.
Hapa kwenye kui-enforce
Corporate Social Responsibility (CSR) ya makampuni ndipo penye tatizo kwa sababu, hadi kufikia mwaka 2014, Tanzania haikuwa na sheria zozote ambazo zinaweza kutumika kuzibana hizi kampuni ili ziweze kuchangia maendeleo ya jamii zinazowazunguka. Uamuzi wa kuchangia ama kutokuchangia maendeleo ya jamii husika umeachwa mikononi mwa kampuni zenyewe. Kipindi cha nyuma kidogo (
Kati ya 2014/15) kulikuwa na mazungumzo ya chinichini kuwa huenda serikali ikaanzisha sheria ya kusimamia CSR ili kuwezesha wananchi waweze kunufaika na uwepo wa kampuni hizi kwenye maeneo yao....hata hivyo sina updates zozote kuhusiana na hilo...wenye ufahamu zaidi kuhusu hatua iliyofikiwa na serikali katika mjadala wa kuanzisha
Corporate Social Responsibility Act waje hapa watujuze zaidi.
Sheria hiyo ikiwepo, itaiwezesha
serikali kuwa na uwezo wa kufanya tathmini ya faida za makampuni kwa mwaka na
kulinganisha na michango yao katika kufanikisha maendeleo ya jamii inayowazunguka. Vilevile, CSR Act, itaiwezesha serikali iweze kuweka mikakati ya muda mrefu ili kuweza kuimarisha mahusiano baina ya makampuni na jamii kwa ujumla.