Matangazo ya Kenya, Uganda na Rwanda Air yanatuvua nguo

Afyayaakili

JF-Expert Member
Sep 12, 2012
923
1,255
Nikisikia matangazo ya mshirika tajwa hapo juu ya ndege ambayo ni ya Africa Mashariki huwa napata msononeko sana moyoni naona kama Tanzania viongozi wake hawapo serious kabisa.

Vitu ambavyo vingekuwa chanzo cha mapato makubwa kwa taifa hasa ambalo lina vivutio vya kutosha vya kitalii ambavyo sina haja ya kuvitaja si ajabu ndio maana Wakenya wanaamua kutuibia sababu wenye navyo hatuna hata muda (yaani kama wanazengo walivyokuwa wanapamba milango yao na Almas ndio maisha tunayoishi kwenye karne ya 21).

Yaani Tanzania kwenye biashara ya safari za anga kwa Afrika Mashariki tunafanana na Sudani ya Kusini na Burundi ambao wako bize na vita WTF...
 
Ni tatizo kubwa muasisi wa Taifa alikua ana malengo mazuri Kulikua na mashirika mengi ikiwemo hilo la ndege lakini walioyatafuna ni hawa viongozi wetu na watendaji tunaowaita wazawa/wazalendo, kikulacho ki nguoni mwako, Nadhani ni muda wa kutoka tulipo otherwise tutabaki watazamaji kwenye shirikisho la Africa mashariki.
 
Tulivyo wajinga tukamponda sana yule binti wa Kenya, binti kapata fursa na kaitumia vyema. Hii fursa imekuja baada ya ujinga wetu watanzania.
Nchi ina kila kitu ina tumetulia tu kama mazezeta, bado tunazidi kuikumbatia CCM .

Kagame japokuwa Dikteta ila alienda Kongo kuiba madini ili kuimarisha uchumi wa Wananchi wake, angepata madini kama ya kwetu je?

Leo hii nchi inaongozwa kwa stori na misisimko, bado mikataba ya Gas haieleweki, madini hovyo. Pesa zilizoibiwa hakuna dalili ya kurudi n.k ila wananchi wake wanakenua meno kila wakisikia mtu katimuliwa kazi, na akitimuliwa utajiri wake upo pale pale.

Kwa tulivyo wajinga, hata leo hii ukiitwa Uchaguzi CCM bado itashinda.
 
Siasa chafu na ukosefu wa vipaumbele. Bongo hii siasa chafu ndo zinatumia mda mrefu kuliko kuwekeza kwenye maendeleo. Tungrkua na ndege zetu utalii ungekua na serikali ingepata mapato zaidi but no one is caring viongozi wanapewa dhamana wanajineemesha.

Ethiopia haina resources nyingi lakini wana shirika LA ndege kubwa zinazozunguka dunia nzima. Tangia Nyerere aondoke madarakani kila kitu kilikufa had viwanda. Tanzania tunaangamia kwa kukosa vision. Chama tawala kina dhamana ya kuongoza nchi ila much time wanatumia kupambana na Ukawa kwa nguvu kubwa. Badala ya kuunganisha watu tuendeleze taifa letu wao ni majanga tu.

Nadhani nchi yetu ina resource curse labda siku tukichange hawa viongozi wachumia tumbo na tutumie wataalamu tutaprogress
 
Viongozi wa hii nchi wamelala na wengi ni wapiga deal tu aisee.
Kila siku mikakati mipya na hakuna kinachofanikiwa mara MKUKUTA mara utasikia MKURABITA mara utasikia MILLENIUM GOLAS mara utasikia BRN mara utasikia KILIMO KWANZA sijui safari hii tutaimbiwa chorus gani tena.
 
Angalau Magufuli ameonesha matumaini alivyosema zile pesa zingenunua ndege kadhaa.... good going, let's be patient...hao majirani wanaweza wakaisoma namba tu na tu-ndege twao
 
Viongozi wamefumbwa macho kwa hili, tuwaombee sana maana ni kama tumerogwa hawaoni kama bila kuwa ndege zetu utalii wetu ni kazi bure yaani mtu kuja Tanzania mpaka apande Ethiopia airline au ndege zingine? Unapoona shirika la ndege linatangaza utalii kwetu sio kuwa wanajipendekeza hapana,

Wanaangalia opportunities ambazo sisi tumefeli
 
Unakuwa na dizaini ya viongozi ambao wapo radhi kukodi ndege kutoka Mwanza kuja dar kumsafirisha mbunge anayetakiwa kuhojiwa na kamati ya maadili ya Bunge. Badala ya kutumia Nguvu hiyo kuburuza mahakamani wezi wa rasilimali za nchi EPA na ESCROW.
 
Angalau Magufuli ameonesha matumaini alivyosema zile pesa zingenunua ndege kadhaa.... good going, let's be patient...hao majirani wanaweza wakaisoma namba tu na tu-ndege twao
Magufuli sawa anania nzuri je wanaomzunguuka wanaimba wimbo mmoja nae???? Nchi hii inatatizo kubwa kuliko vile watu wengi wazaniavyo. Viongozi walio wengi hawapo kwaajili ya kuwatumikia wananchi wapo kwa maslahi binafsi na ndio maana unaona ubadhirifu aliogundua Magufuli ndani ya miezi mitatu tu nikama nchi haikua na serikali.

Sasa watendaji wakuu was serikali waliopo zaidi ya 3/4 ni walewale waliokua kwenye serikali dhalimu iliyoruhusu rushwa, ubadhirifu, ukwepaji kodi, kutokuwajibika na kadharika, Sasa Magufuli peke yake atafanya nini? No wonder kutokana na utendaji kazi wa Magufuli wanaadhirika, wanapoteza fedha (off course walizo tuibia) na hivyo wanamkakati wa chini kwa chini wa aidha kudhoofisha juhudi zake au kusimamisha kabisa.

Kukosekana kwa uzalendo, utu na maarifa ndio chanzo cha kukosa innovation ndani ya serikali juu ya ku-utilise resources zetu kwa manufaa ya nchi. Viongozi wengi hawajui hata kwanini asubuhi wanaenda ofisini. Hawana dira wala hawajui hata objectives za wao kuwa walipo, wanachojua ukiteuliwa tu kuwa waziri, kamishina, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya ,katibu mkuu na kadharika basi ni ulaji tu.

Hawana malengo wala evaluation ya matokeo ya kile wanachosimamia (ni business as usual ) wanafikiri utendaji ni kutoa maagizo na kutisha watu. Objectives nyingi za serikali sio quantified na wasimamizi hawakuelimika (having a degree does not make one educated) kwa ufupi elimu walio nayo ni operation certificate lakini hiwafanyi kuwa proactive na kuleta innovation katika utendaji wa shughuli za serikali hivyo usitarajie matumizi chanya ya rasilimali zetu.
 
Nikisikia matangazo ya mshirika tajwa hapo juu ya ndege ambayo ni ya Africa Mashariki huwa napata msononeko sana moyoni naona kama Tanzania viongozi wake hawapo serious kabisa.
Tuambie umesikia wapi,matangazo kwenye chombo gani..
Acha kuja na stori za kufikirika ..kwa taarifa yako mashirika yote ya Uganda hayafanyi kazi..Uganda Airline la serikali lilishakufa toka mwaka 2001
Uganda Airlines - Wikipedia, the free encyclopedia
...Na Air Uganda walinyang'anywa leseni toka mwaka 2014..kwasababu ya kukosa vigezo na kushindwa kutimiza masharti..
Air Uganda - Wikipedia, the free encyclopedia
Kenya Airways wanaomba ruzuku serikalini dola milioni 500(sawa na trilioni moja ya tanzania) ili wafufuke
MPs Are Promising Action Against Kenya Airways Officials Over Billions In Losses

Kenya Airways needs urgent government bailout

Acha kusifia usichokijua..Taarifa za Rwandair ntakuletea ukizitaka.
 
Magufuli sawa anania nzuri je wanaomzunguuka wanaimba wimbo mmoja nae???? Nchi hii inatatizo kubwa kuliko vile watu wengi wazaniavyo. Viongozi walio wengi hawapo kwaajili ya kuwatumikia wananchi wapo kwa maslahi binafsi na ndio maana unaona ubadhirifu aliogundua Magufuli ndani ya miezi mitatu tu nikama nchi haikua na serikali.

Sasa watendaji wakuu was serikali waliopo zaidi ya 3/4 ni walewale waliokua kwenye serikali dhalimu iliyoruhusu rushwa, ubadhirifu, ukwepaji kodi, kutokuwajibika na kadharika, Sasa Magufuli peke yake atafanya nini? No wonder kutokana na utendaji kazi wa Magufuli wanaadhirika, wanapoteza fedha (off course walizo tuibia) na hivyo wanamkakati wa chini kwa chini wa aidha kudhoofisha juhudi zake au kusimamisha kabisa.

Kukosekana kwa uzalendo, utu na maarifa ndio chanzo cha kukosa innovation ndani ya serikali juu ya ku-utilise resources zetu kwa manufaa ya nchi. Viongozi wengi hawajui hata kwanini asubuhi wanaenda ofisini. Hawana dira wala hawajui hata objectives za wao kuwa walipo, wanachojua ukiteuliwa tu kuwa waziri, kamishina, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya ,katibu mkuu na kadharika basi ni ulaji tu.

Hawana malengo wala evaluation ya matokeo ya kile wanachosimamia (ni business as usual ) wanafikiri utendaji ni kutoa maagizo na kutisha watu. Objectives nyingi za serikali sio quantified na wasimamizi hawakuelimika (having a degree does not make one educated) kwa ufupi elimu walio nayo ni operation certificate lakini hiwafanyi kuwa proactive na kuleta innovation katika utendaji wa shughuli za serikali hivyo usitarajie matumizi chanya ya rasilimali zetu.
Mkuu kweli unachosema ila jamaa ndio maana kasema tumuombee maana anachotaka kukifanya hadi mashetani yanaogopa
 
Tuambie umesikia wapi,matangazo kwenye chombo gani..
Acha kuja na stori za kufikirika ..kwa taarifa yako mashirika yote ya Uganda hayafanyi kazi..Uganda Airline la serikali lilishakufa toka mwaka 2001
Uganda Airlines - Wikipedia, the free encyclopedia
...Na Air Uganda walinyang'anywa leseni toka mwaka 2014..kwasababu ya kukosa vigezo na kushindwa kutimiza masharti..
Air Uganda - Wikipedia, the free encyclopedia
Kenya Airways wanaomba ruzuku serikalini dola milioni 500(sawa na trilioni moja ya tanzania) ili wafufuke
MPs Are Promising Action Against Kenya Airways Officials Over Billions In Losses

Kenya Airways needs urgent government bailout

Acha kusifia usichokijua..Taarifa za Rwandair ntakuletea ukizitaka.

Acha kupuyanga na taarifa zako ambazo hujafanya uchunguzi unajua Kenya wamefanya mipango gani ili wasiingie kwenye hasara waliyopata na unaposema Uganda Air imekufa unafanya nikushangae na taarifa zako za Rwanda hazina mashiko. Ingia kwenye blog kadhaa za East Africa ndio utaona hayo matangazo na baadhi ya redio na vituo vya tv.
 
Weka link..tuone. usilete longolongo..hii ni JF.
 
Tuambie umesikia wapi,matangazo kwenye chombo gani..
Acha kuja na stori za kufikirika ..kwa taarifa yako mashirika yote ya Uganda hayafanyi kazi..Uganda Airline la serikali lilishakufa toka mwaka 2001
Uganda Airlines - Wikipedia, the free encyclopedia
...Na Air Uganda walinyang'anywa leseni toka mwaka 2014..kwasababu ya kukosa vigezo na kushindwa kutimiza masharti..
Air Uganda - Wikipedia, the free encyclopedia
Kenya Airways wanaomba ruzuku serikalini dola milioni 500(sawa na trilioni moja ya tanzania) ili wafufuke
MPs Are Promising Action Against Kenya Airways Officials Over Billions In Losses

Kenya Airways needs urgent government bailout

Kwa hiyo air Uganda ile yenye nembo ya cranes haiku ya serikalI? Na haiko hewani tena? Nakumbuka niliiona one day imekuja bongo. Ila sikumbuki mwaka nikama hiyo hiyo 2014.
 
Back
Top Bottom