Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,703
- 1,724
Kwa kweli tunakoelekea si pema. Ikiwa tunapiga vita tena kwa nguvu zote ushoga, mavazi yasiyo na staha, madawa ya kulevya na kadhalika ili kujenga jamii yenye heshima, tunachelea kuona baadhi ya matangazo hasa kwenye radio ya dawa lishe hayana staha hata kidogo. Fikiria umekaa na watoto sebuleni, radio ikiwa 'on', mara mnasikia tangazo la dawa hizo na msemaji anasema ana dawa za kutibu tatizo la 'kuchelewa kufika kileleni!' utajisikiaje? inakera.