Matangazo ya dawa lishe kwenye 'media' yadhibitiwe

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,681
1,698
Kwa kweli tunakoelekea si pema. Ikiwa tunapiga vita tena kwa nguvu zote ushoga, mavazi yasiyo na staha, madawa ya kulevya na kadhalika ili kujenga jamii yenye heshima, tunachelea kuona baadhi ya matangazo hasa kwenye radio ya dawa lishe hayana staha hata kidogo. Fikiria umekaa na watoto sebuleni, radio ikiwa 'on', mara mnasikia tangazo la dawa hizo na msemaji anasema ana dawa za kutibu tatizo la 'kuchelewa kufika kileleni!' utajisikiaje? inakera.
 
Tiba mbadala: wanakamua limao, karoti.......blah, blah kumbe kwenye hiyo juice wameweka unga wa vidonge vya hospitali na hasa ciprofloxacin, jamaa wamesambaa hadi huku vijijini.
 
Tiba mbadala: wanakamua limao, karoti.......blah, blah kumbe kwenye hiyo juice wameweka unga wa vidonge vya hospitali na hasa ciprofloxacin, jamaa wamesambaa hadi huku vijijini.
Iiiiiiih kuuumbe!
 
Tiba mbadala: wanakamua limao, karoti.......blah, blah kumbe kwenye hiyo juice wameweka unga wa vidonge vya hospitali na hasa ciprofloxacin, jamaa wamesambaa hadi huku vijijini.
Haya mkuu, serikali imeamka.
 
Kuna baadhi ya vituo bado vinapiga matangazo ya Dr. Mwaka. Kama kile kituo cha Maajabu-Magic Fm.Nauliza kama uamuzi wa baraza la tiba asili a wizara umebatilishwa. Maana kuendelea kwa matangazo kunatuchanganya sisi wananchi hasa tunaotaka watoto.
 
Back
Top Bottom