Matangazo CNN: Tumelala? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matangazo CNN: Tumelala?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mfalme, Jun 30, 2009.

 1. M

  Mfalme Member

  #1
  Jun 30, 2009
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku hizi naona sana kwenye CNN watani zetu (wakenya) na nchi nyingine za Afrika kama vile Angola na Afrika ya kusini wakijitangaza sana tu kwa matangazo waliyoyatayarisha maalum na mazuri sana kama lile Tangazo la "Malaysia truly Asia". Wakenya wanasema "The magic of Africa".
  Sisi sijui viongozi wetu wanasubiri kudra za mwezimungu?.
   
 2. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wanasubiri Nyerere aje atwambie kama kupata watalii ni lazima uitangaze nchi yako.

  Maneno yako ni kweli TZ imelala, mie natokea visiwani hapo zama za kale nilidhani mlima Kilimanjaro uko Kenya jinsi tulivyolala jinsi na jinsi Kenya walivyoutangaza na kuingiza hela kibao kupitia mgongo wa mlima huo.

  TZ haswa bado ina usingizi wa Nyerere, na sijuwi lini tutaamka...labda kiama :confused:

  Maana mambo ni mengi ambayo tumelala, likiwemo na suala zima la kiswahili, TZ haitakiwi kutumia English mashuleni inatakiwa kutumia kiswahili...lakini iyo iko nje ya maada ....ooops:rolleyes:
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,386
  Likes Received: 22,266
  Trophy Points: 280
  Usingizi wa uzuzu magic ndio adui wetu mkubwa.
   
 4. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuitanganza tanzania sio kupitia CNN tu mkuu.Kuna njia nyingi sana za kuitangaza mimi na wewe ndio hasa tuna paswa kuitangaza nchi yetu sio swala la kusubiria serikali ifanye hivyo.Wananchi Wakenya wamejitolea sana kuitangaza nchi yao kila kona ya dunia,kwa njia tofauti zikiwepo kwa njia ya Internet n'k...sasa sisi tunapo hiachia serikali kila kitu na kuitupia lawama lukuki kwamba imelala ingali sisi wanachi wenyewe ndiyo tulio lalal.  Bonyeza hapahttps://www.jamiiforums.com/habari-hoja-mchanganyiko/30869-tuitangaze-tanzania-yetu-kwenye-mitandao.html
   
 5. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  wakiweka tangazo moja kwenye london taxi wanajipiga na picha wenyewe....
  hizo hela zinatolewa na zinaliwa tuuu
  wakenya wameanza kujitangaza siku nyingi na magical kenya, nilikua naona matangazo yao kwenye TV uk miaka 6 iliyopita
   
 6. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nimemwona MiNISTER of tourism wa kenya leo on CNN..Yupo busy kuuza nchi yake!
  sIKU ZA NYuma Iliniuma sana niliposikia for world cup 2010 kuna tourists watalala mauritius and will be jetted to and from the games...TANZANIA TUPOOOOOO???
   
 7. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Usiwe na wasi mkuu, jamaa nafikiri wanatafuta "muwekezaji" wa kutoa matangazo hayo, maana siku hizi ndio fashion serikalini.
  Na atakapopatikana huyo "muwekezaji" si ajabu kupata madudu mengine kama ufisadi katika vitalu vya uwindaji
   
 8. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu ulisoma chini ya mwembe upi hadi kutojua elimu simple ya jiografia ya Tanzania
   
 9. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuna kipindi nilisikia kwamba serikali imetenga fungu la pesa kwa jili ya matangazo CNN,na kwa kuanza walianzia na CNN local (abayo inaonekana marekani tu) sijui imekuwaje mpaka leo wameshindwa kuyatangaza upande wa CNN International,ambayo ndio inatizamwa na dunia nzima.
   
 10. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  imepita mwaka sasa tangu nilipo soma hii habari.
   
 11. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dhana kuu ya fikra zangu, iko katika namna tunavyoweza kutumia rasilimali yetu ya uwanja mpya wa michezo uliopo jijini Dar es Salaam kwa manufaa ya kuendeleza utalii nchini.
  Hapana shaka katika ukanda huu waAfrika Mashariki, uwanja huu ni mkubwa na unastahili kutumika kwa hadhi inayostahili kuvuta utalii. Kwa maana hiyo tulicho nacho ni mali.
  Naamini tukioanisha suala la michuano ya kombe la dunia kufanyika nchini Afrika Kusini, zipo timu za soka zitakazofika nchini kufanya mazoezi na watakapokuwa humu watabaini vivutio vilivyopo.
  Cha muhimu kwa wadau wa michezo wa kigeni watakapofika nchini kufanya mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo ya kombe la dunia ambayo iko usoni, tunahitaji kuwekeza mikakati yetu humo humo nasi tufaidike.
  Kama ilivyokuwa katika mkutano wa Sullivan uliofanyika mjini Arusha mwaka huu, nasi tulitakiwa kuelekeza mikakati kwa wageni hawa wanaofika kufanya mazoezi nchini, kuhakikisha tunapata faida ya kujitangaza katika utalii.
  Sasa hivi si haba. Nilifurahi nilipomsikia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alipotamka Bungeni kwamba juhudi za kujitangaza zimechukua sura ya mafanikio.
  Mfano mojawapo aliyoutoa ni kwamba, nchini Marekani vivutio vya kitalii vimetangazwa katika televisheni maarufu ya CNN na matokeo yake yanaonekana, kwamba kuna watalii wengi wanaomiminika kutoka huko.
  Nionavyo, hiyo ndio namna hata kwa wageni watakaofika kufanya mazoezi katika viwanja vyetu kwa ajili ya michuano ya kombe la dunia, mambo ya namna hiyo tutayashuhudia na utalii wetu ukawa na manufaa kwetu sote.
  Inastahili sasa hivi wadau wakakuna ubongo juu ya aina gani mikakati wanayopaswa kuweka na aina yote ya fursa zilizoko kutumika na hatimaye hatua iliyopigwa ionekane.
  Hebu tuthubutu ili tuweze.
   
Loading...